...Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.
...
CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.
...
Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.
...
Nimewawekea link na picha mbali mbali kusappoti uzi.
Boeing 787 Register - Welcome
www.airliners.net/forum/viewtopic.php?t=1335649
www.airportspotting.com/boeing-finding-homes-terrible-teen-787s/
www.boeing.com/commercial/customers/air-tanzania/air-tanzania-787-order.page
Ninaamini WaTz tumefikwa na ugonjwa wa
kusadikika . Ugonjwa wa
kusadikika ni ugonjwa ambao aliyeugua huamini ndoto ni kweli, na akitoka ndotoni anashangaa na kuweweseka, kwa kutambua kuwa siyo kweli ni ndoto tu. Wagonjwa wengine watajisalimisha kwa waganga wanaodai kujua tafsiri za ndoto.
'The Tomorrow People': sina maana na wewe ni mwathilika wa ugonjwa huo!
Sababu kubwa ya kuugua ugonjwa wa
kusadikika ni matumizi mabaya ya habari zilizoko mitandaoni ambazo, kwa sasa, kwa sehemu kubwa WaTz wengi wanaziamini. Lakini, kwa wajuvi wa mambo, huwa habari za mitandaoni na vyombo vya habari, hutiliwa mashaka hadi hapo zitakapohuishwa na taarifa zingine kutoka vyanzo sahihi, hasa kwenye chanzo (cha habari, taarifa, takwimu, nk). Kwa mfano, waandishi wa habari wameshindwa kweli kufika kwenye kijiji cha Kolomije na kupata habari za uhakika Bashite ni nani? Au kwenda kwenye shule/vyuo vilivyotajwa!
Yumkini kila mtoa hoja huwa na lengo lake.
Ununuzi wa 'Boeing 787-8 Dreamliner' ambao sasa umekuwa gumzo kutokana na hoja ya Mh Zitto, unatufumbua WaTz makini, faida na hasara za mitandao katika kujenga demokrasia yenye tija.
Yawezekana kuna ukweli kuhusu hizo ndege, je, Serikali haikulijua hilo, ila Mh Zitto na mitandao? Kama ni kweli Serikali haikulijua hilo, na sasa inalijua, na haijachukua hatua kulinda maslahi ya Taifa, iweje Rais Magufuli, ununuzi wa ndege hiyo, iwe ndiyo moja ya agenda zake kuu kuelekea uchumi wa kati!
Mkuu 'The Tomorrow People', kama ulivyosema
Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Nina imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.. Na mimi nina amini ina watu makini na wazalendo ambao wanaitakia mema nchi hii. Pia namwanini Rais Magufuli kwa kauli, matendo, utashi wa kisiasa (political will) na uthubutu wake kufikia lengo la kuleta mabadiliko ya kweli ya maendeleo kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiteknolojia.