Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

Ukweli kuhusu ATCL Boeing 787-8

CCM ni wakupiga chini tu hawana jipya kabisa wanazidi kutuongezea umaskini
 
Mkuu:
Ni dhahiri Japan wanazo hizo Terrible Teens lakini wao wanategemea zaidi ukomo wa masafa yao.
Inawezekana ni kwa ajili ya matumizi ya ndani (Domestic Operations) au Jeshini, kama Mexican Airforce wao ukomo wa masafa sio tatizo
Japan ni ndogo kwa size vsiwa vile ukivweka pamoja mkoa wa morogoro ni mkubwa unaweza zunguka pote kwa siku moja. Hawawez nunua dege kama hilo for domestic operation.
 
Terrible teens,mara ilidoda 5 yrs..achilia mbali chenji tuliyopigwa,...usalama wake vepee..jina la terrible linastua hehe
 
Kweli kabisa. Tulisema tunanunua ndege tangu 2016. Ndege iliyoko tayari inasubiri miaka miwili kufika. Hapo ndio shida. Hapo bado inaonekana kama iko "on order". Wakati wa Q400 Bombardier walisema inachukua masaa matatu -Dar-Moshi. haikuwa hivyo.

Kwenye mikataba hakuna anaye disclose details. Kampuni ya Canada imeigomea Marekani kudisclose details. Itajulikana tumenunua bei gani tu haijifichi-si mkaguzi mkuu si yupo

Ila hizi kelele si jambo baya. Airline safety and security ni kitu sensitive sana. Kwenye hii industry hakuna nafasi ya kufanya makosa.

Niulize tu. Kwa hiyo na Japan wanayo hizo terrible teens; kulingana na mleta mada.
Hizo ndege baada ya kukosa soko zilipunguzwa bei zaidi nusu ya bei zake(strike price), sasa ni je imekuwaje tumenunua katika bei yake ya awali.

Is either kama taifa tumepigwa AU wajanja wachache wamepiga pesa
 
Japan ni ndogo kwa size vsiwa vile ukivweka pamoja mkoa wa morogoro ni mkubwa unaweza zunguka pote kwa siku moja. Hawawez nunua dege kama hilo for domestic operation.
Nani amekudanganya wewe muongo? Japan ni nchi ndefu sana(think chile) kutoka point moja hadi nyengine ni zaidi ya km 3000. Na ina ukubwa karibu asilimia arobaini ya tanzania.,thats not the size of Morogoro.

Huu uongo kadanganye watu kijiweni kwenu huko shitimbi.,sio JF
 
Hizo ndege baada ya kukosa soko zilipunguzwa bei zaidi nusu ya bei zake(strike price), sasa ni je imekuwaje tumenunua katika bei yake ya awali.

Is either kama taifa tumepigwa AU wajanja wachache wamepiga pesa
Kwa sababu ya kiherehere cha yule baba kutokutaka kufuata procurement procedures. Alishani anaenda kununua suruali kkoo.
 
Hizo ndege baada ya kukosa soko zilipunguzwa bei zaidi nusu ya bei zake(strike price), sasa ni je imekuwaje tumenunua katika bei yake ya awali.

Is either kama taifa tumepigwa AU wajanja wachache wamepiga pesa
Baada ya hzo terrible teens Boeing waliendelea kutengeneza ndege zngne? Je walizpa jina gani? Ni hii 787-8? Kama zna jina hilo znauzwa bei gani? Niltegemea mtoa post ange ainisha vyote hvo. Ila nadhan yupo kwenye pdf ya jana
 
Ethiopian wame-order ndege mbili hapo kny orodha ya 1-20, tunaamini kuwa ni moja ya shirika la ndege makini ktk bara la afrika hivyo sidhani kama tumebugi. Tupunguze tu wivu wa vyama tu-focus kny maendeleo ya vyama
Wame-order ndiyo, but at which price? Strike price au discounted price
 
Nani amekudanganya wewe muongo? Japan ni nchi ndefu sana(think chile) kutoka point moja hadi nyengine ni zaidi ya km 3000. Na ina ukubwa karibu asilimia arobaini ya tanzania.,thats not the size of Morogoro.

Huu uongo kadanganye watu kijiweni kwenu huko shitimbi.,sio JF
Toa na maji
 
Asante. Kama Ni hivyo. Mbona azijifika Tanzania? Na ukiuliza unaambiwa hiko kwenye line. Na kuna baathi ya Watanzania wako kule wakijifunza jinsi ya kufanya matengenezo madogomadogo. ATCL Watufamishe kuhusu hilo. Maana walikuweko kwenye uwazi Na kushauri serekali.
 
Ninavyojua ndege hazitengenezwi kama magari kisha kutafutiwa mteja, utaratibu unatoa order kisha wanakutengenezea, hiyo uliyotengeneza kwa excel mtu yoyote anaweza kutengeneza.
Kama Rwandair waliinunua kwanini baada ya miezi miwili hawajaichukua ikarudishwa sokoni (kwa majibu ya draft ya excel yako) kwanini sisi tumeambiwa mpaka 2018 ndiyo itafika hapa?
Punguzeni chuki hazisaidii chochote acheni rais apige kazi kama mnachuki nae hamieni hata Burundi au Congo, akija siku yoyote akichukua madaraka mnaemtaka mtarudi, mtakufa kwa chuki zenu.
Hizo ndege zilishauzwa kwa makampuni, wakiwa bado hawajizipokea ikagundulika zina kasoro. Zikabaki zimedoda hadi baadae walipopunguza bei(massively discount) ndio zikaanza kutoka.

Swali ni je, ni ipi bei tuliyonunulia, ni hiyo 224.6USD au ni katika ile waliita massive discount?
 
Shalom watanzania wenzangu!

Disemba 12, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa baadhi yetu tuliomchagua JPM na Tutamchagu tena 2020 Mungu akitujaalia na wengine mlinuna baada ya taarifa kutoka serikali imeweka oda Boeing, ili kununua ndege ya kisasa kabisa 787-8.

Na yakwamba serikali itatoa $224.6Millioni ili kupata ndege hiyo.

Kumekuwa na taarifa mbali mbali, kwamba manunuzi haya yana chembe chembe za ufisadi. Na kwakuwa sipendi kuamini vitu bila kufanya utafiti nami nimeona nizame kwenye websites mbali mbali kutafuta ukweli.

Kwa ufupi kama wengine wasemavyo ni kweli hata Mimi nimeshaamini "SERIKALI IMEPIGWA"
lakini hadi kufikia hii Conclusion kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyajua.

1. SERIAL NUMBER(SN) NA LINE NUMBER.
-Kila ndege huwa na serial number yake kama yalivyo magari. Ndege tulioagiza serial number yake ni 35508
-Line number ni ndege ya ngapi kutengenezwa. Kwa mfano kama zimetengenezwa ndege 10. Ndege ya kwanza itakuwa LN1, ya pili LN2 nakuendelea.

2. TERRIBLE TEENS NI NINI?
Terrible teens ni zile ndege za mwanzo kutengenezwa za Boeing 787-8. Hizi ndege zilikuwa 20. Kwahiyo hiyo ni Line number 1-20 (Kuwa makini hapa). Na hizi ndege zilifanyiwa majaribio mengi na matengenezo mengi mapya ili kupata ndege bora zaidi.

Kwa kifupi tunaweza sema zilikuwa sample ya kutengenezea ndege zingine. Kutokana na kufanyiwa modification za mara kwa mara hizi ndege zilipitiliza uzito uliotakiwa. Kutokana na kuongezeka uzito ndege hizi hata uwezo wake wa Masafa ukawa Umepungua kwa Maili 1000 au KM 1609.344

Kutokana na hili makampuni yaliotaka order za mwanzo kama All Nippon, Maroc etc. yaligoma kuchukua hizi ndege bali yalichukua ndege zilizotengenezwa baada ya zile 20 za mwanzo yaani Line number 21 na kuendelea.

Terrible teens zingine ziliwekwa kwenye majumba ya kumbukumbu na baadhi ya kampuni walizichukua. Zikabaki 12 uwanjani miaka mitano bila mnunuzi toka 2009 zilipoanza tengenezwa.

Kutokana na aibu iliyokuwa inaipata Boeing ya kukaa na mindege isiyo uzika. Ikaamua yafuatayo

(a) Kutafuta Wateja ambao hawatajali issues ya kikomo cha masafa ya ndege

(b) Kuziuza hizi ndege kwa bei rahisi ( karibu nusu bei kutoka $224M hadi $99M)

CONCLUSION
Kutoka katika websites ya Boeing na na web zingine za usafiri wa anga zimeweka wazi Ndege tulio iwekea order ni Boeing 787-8, serial number 35508, Line number 19.

Sasa kwa maelezo niliyotoa Line number 19 IPO ndani ya Line number 1-20. Kwa kifupi ndege tuliogiza ndio zile ndege za mwanzo 20 zilizopachikwa jina la Terrible Teens.

Swali lingine la kujiuliza kwanini tumeuziwa ndege iliyo doda ,iliyoshushwa bei hadi kufikia $99M kwa bei ya ndege mpya yaani $224.6M?

Bila kupepesa macho hapa tumepigwa $124M na ushee ambazo tungeweza nunua Boeing 737-800 Next Generation mpyaaaa ya 2016.

Kama nilivyokwisha sema Nina imani na Rais Magufuli ni mtu makini anayeipenda Tanzania. Na imani hili litatolewa maelekezo na kufanyiwa kazi.

Nimewawekea link na picha mbali mbali kusappoti uzi.

66cbe3973d2476f0afd0ef4b23f5d581.jpg

5ffe88270490cadedd65af84f1f2a940.jpg
32a59f2db3a1932ae85e9b8bfd8d26fd.jpg

Boeing 787 Register - Welcome

www.airliners.net/forum/viewtopic.php?t=1335649

www.airportspotting.com/boeing-finding-homes-terrible-teen-787s/

www.boeing.com/commercial/customers/air-tanzania/air-tanzania-787-order.page

Mkuu labda Mimi sijaelewa vizuri.
Hivi umesema kuwa serikali imeagiza ndege na katika order waliotoa wameagiza
Line number 19.
Ulisema namba 1-20 ndo hizo ambazo hazina ubora. Na ambazo baada ya kupunguzwa bei zikauzwa, zikabaki 12.
Na umesema kuwa hiyo iloagizwa iko ndani ya hizo 1-20.

Maswali.
1; Hizo ndege 12 zilizobaki bado zipo hadi leo.?? Katika hiyo packing yao.
2; kama ziliuzwa zote zimekwisha, je boeing bado wamerudia tena kutengeneza ndege hizo hizo zenye hasara??
Au wameamua kutengeneza kwa mifumo mipya ambayo ndege tunayoagiza ndo ipo ndani yake????

3; kama bado zipo na ndege tulioagiza ni kama hizo kwanini hatukupewa moja kwa moja na badala yake tunatengenezewa mpya ambayo mpaka sasa haijakamilika???

4; Kulikuwa na ulazima gani wa kutengeneza ndege mpya ya aina hiyo hiyo huku unazo nyingine zimepaki hazijauzika??

Naomba nijuze mkuu
 
Mkuu labda Mimi sijaelewa vizuri.
Hivi umesema kuwa serikali imeagiza ndege na katika order waliotoa wameagiza
Line number 19.
Ulisema namba 1-20 ndo hizo ambazo hazina ubora. Na ambazo baada ya kupunguzwa bei zikauzwa, zikabaki 12.
Na umesema kuwa hiyo iloagizwa iko ndani ya hizo 1-20.

Maswali.
1; Hizo ndege 12 zilizobaki bado zipo hadi leo.?? Katika hiyo packing yao.
2; kama ziliuzwa zote zimekwisha, je boeing ado wamerudia tena kutengeneza ndege hizo hizo zenye hasara??
Au wameamua kutengeneza kwa mifumo mipya ambayo ndege tunayoagiza ndo ipo ndani yake????

3; kama bado zipo na ndege tulioagiza ni kama hizo kwanini hatukupewa moja kwa moja na badala yake tunatengenezewa mpya ambayo mpaka sasa haijakamilika???

4; Kulikuwa na ulazoma gani wa kutengeneza ndege mpya ya aina hiyo hiyo huku unazo nyingine zimepaki hazijauzika??

Naomba nijuze mkuu
Hana majibu
 
Ha ha haaaaaa

Unasahau kuwa wengine akina mimi tulizaliwa tunaongea kilugha cha makabila yetu, na sasa tunajifunza kiswahili chenu.

Usijali mdau mimi mutanzania mnono haswa.

Hahahaha, pamoja sana mkuu
 
Hizo ndege baada ya kukosa soko zilipunguzwa bei zaidi nusu ya bei zake(strike price), sasa ni je imekuwaje tumenunua katika bei yake ya awali.

Is either kama taifa tumepigwa AU wajanja wachache wamepiga pesa
Mkuu hebu jaribu kuwa mdadisi kidogo
 
Back
Top Bottom