Ukosefu wa ladha ya lugha ya Kiswahili kwenye mapenzi

Huu mtanange unavyoendelea itabidi tumtafute Madam Rita atupe ujuzi wa kuchagua mshindi
Companero naona unampiga Yericko Nyerere kwa bakora yake mwenye! Nakuamkia "Chei Chei".

Ila Nguruvi3 mtu mzima dawa, naona unataka kutoa somo la manufaa ya nyama ya ulimi kwa wanagenzi
 
Last edited by a moderator:
Gaijini kumbe ni binti, hilo sikujua
Sasa natoa boriti, Kaunga namrudia
Kongosho ni kizingiti,shikamoo kunitupia
Hiki ni kizungumkuti,Homa sasa yanirudia

kuna binti na binti, ewe nguruvi elewa
silete za vijisenti, eti kisa umechelewa
gaijin si kabinti, enyi waposa mlolewa
kwenu ni anti, wangu gaijin mwolewa
 
Gaijini kumbe ni binti, hilo sikujua
Sasa natoa boriti, Kaunga namrudia
Kongosho ni kizingiti,shikamoo kunitupia
Hiki ni kizungumkuti,Homa sasa yanirudia

Sungura mjanja tulambiwa, ndizi mbivu kakacha
Kama nyuki walojambiwa, asali tamu wakaacha
Nguruvi huyo kakimbiwa, kisa kavujia pakacha
Boriti imekuwa mbwa, yasingiziwa ya machicha
Eti sasa twaimbiwa, sizitaki mbichi zimechacha
 
Kongosho huyu ruhani hata maalim hatoshi labda shura ya wanazuoni!

Au kama alivyosema Nguruvi3 huyu itakuwa mzuka, na hali ikiendelea hivi hivi sio ubani tu na kanga ya pande tatu itakayohitajika, nadhani itabidi tuongelee masuala ya vikuba sasa!

Ndio na sema ndio, kama vile Mungu wa tatu (Nguruvi3) alivyonena, kaweka muamala hadharani,

kapalilia penzi letu tamu, Gaijin stuka toka mtimani, fikiri mara sabini, isizidi saba,

Nimekuwa muhanga wa subira, tena nisiyechoka kumeza mate,

Mapigo ya moyo yaenda kasi, mithiri ya mtalawanda wa nyika,

Gaijin sikia kilio cha beberu, tena lilofuzu vikinza,

Subira yangu ni muhimu, kwako na kwa malimwengu pia,

Mungu anatuona, kwa macho ya rohoni si ya nyama na mwili!
 
Last edited by a moderator:
Kiswahili bado hakina maneno mazur ya kuvvia kimahaba,lugha hi bado inakua na kuongeza misamiati mipyaamwakaji wa maneno kama vile: nakupenda sana hauna mvuto kama vile '' i love you so much'' pia maneno kama vile '' i miss u baby'', ''honey'', ''darling'', ''baby'' na mengine unaweza kuongezea kiswahili chake kimekuwa utata.[/QUOT
 
Ndio na sema ndio, kama vile Mungu wa tatu (Nguruvi3) alivyonena, kaweka muamala hadharani,

kapalilia penzi letu tamu, Gaijin stuka toka mtimani, fikiri mara sabini, isizidi saba,

Nimekuwa muhanga wa subira, tena nisiyechoka kumeza mate,

Mapigo ya moyo yaenda kasi, mithiri ya mtalawanda wa nyika,

Gaijin sikia kilio cha beberu, tena lilofuzu vikinza,

Subira yangu ni muhimu, kwako na kwa malimwengu pia,

Mungu anatuona kwa macho ya rohoni si ya nyama na mwili!

asiyekubali kushindwa, mhenga alinena
hakika ni mshindwa, si mshindani tena
gaijin umemshindwa, ni wangu mbena
mnzagila napendwa, naye binti mnena
 
asiyekubali kushindwa, mhenga alinena
hakika ni mshindwa, si mshindani tena
gaijin umemshindwa, ni wangu mbena
mnzagila napendwa, naye binti mnena

Haahaaahaa daah mkuu, ngoja hili zali aliamue Gaijin mwenyewe, maana sisi hata tungeimba vina vyote kama Gaijin hajaamua mshindi ni kazi bure tu!

Mnzagila nimekukubali haahaaa Mbena wewe nuksi!

Mnyalu bwana Nguruvi3 naona kazima kabisa!
 
Jamani hamjui kuwa "haya ni sehemu ya imani"?

Hamjui pia kuwa mila na tamaduni hazipendezewi na mtoto wa kike mwenye kujihashua hadharani?

Hamjasikia nyie kuwa mila zinataka mtoto wa kike "kuona haya" hata kutamka hadharani kuwa amemkubali mwanamme anaetaka kumuoa, kiasi cha kuruhusu "silence" kuwa ni sawa na kukubali?

Kwa hiyo kimila, tamaduni, na kiimani, kinachoendelea hapa ni batili

:A S-frusty:
 
Kwa kinywa cha dhahabu naomba ni shangilie!

Huu ni ushindi wetu Gaijin,dhidi ya wakware na wabaka haki,

Kimya chako nakiheshimu, najua nawe wajua pia,

Chenga hii ni aghali, hakika nimewalamba wafitini wangu wote,

Asante Gaijin na sema toka mtimani kweli asante Gaijin,
 
kimya kimya jamani, mhenga si alitujuza
sio dalili ya amani, mshindo wake hujuza
mie wangu gaijini, sasa mpaka awe ajuza
silete za majini, kutwangia kama mshuza
 
Fani yengiwa utani, watenzi waso ughani
Uvundo uso ubani, wagenzi waso mizani
Ufundi uso na kani, wapenzi waso na shani
Iktisadi si idadi, shairi alimuradi ?

Iktisadi si idadi, shairi alimuradi ?
Tungo kazi ya stadi, usambe kwenda midadi
Afaleki kwenye jadi, pwani wapi Bariadi?
Si bora wa Takoradi, upwa ana kwa ahadi

Si bora wa Takoradi, upwa ana kwa ahadi
Wewe hata kwa bajaji, hujaipata taraji
Kuzama katika haji, bila alifu kipaji ?
Fani kutiwa dukizo, kwa malenga ni chukizo

Fani kutiwa dukizo, kwa malenga ni chukizo
Tenzi za uambukizo, washairi ni kimbizo
Fani kama maigizo, yalokosa uchagizo
Kuiharibu kalamu, kwa malenga ni haramu

Kuiharibu kalamu, kwa malenga ni haramu
Kamwe mpaka dawamu, milango ya Jehanamu
Kuondoa ufahamu, kwa chukizo za awamu
Watoto jifunze vina, shikizeni na mizani

Watoto jifunze vina, shikizeni na mizani
Virefu kama visima, vya enzi Mjeremani
Mjue chota hekima, ka vito vya Mererani
Kwa si haba taadhima, hapa mpaka Merekani

Kwa si haba taadhima, hapa mpaka Merekani
Mashairi kwa kupima, sio ukware wa ghani
Kimbi shairi kubina, kwa ngoma za baniani ?
Angalizeni kusoma, kabla kujitia homa

Angalizeni kusoma, kabla kujitia homa
Mje kutoka Musoma, kufika Ilala Boma
Vipi msipate noma, kutokujua ya Roma?
Vina na mizani kina, ni lulu ya mshairi

Vina na mizani kina, ni lulu ya mshairi
Najua kuna Wachina, watokuja kughairi
Lakini jadi kuchina, haiwezi Mswahili
Kama saa inagota, shairi lapiga mota

Kama saa inagota, shairi lapiga mota
Kama ni misheni kota, au Kinyasini sota
Ugwiji wataka tota, so mambo kuotaota
Mshairi hajifichi, mwanagenzi shusha hadhi

Mshairi hajifichi, mwanagenzi shusha hadhi
Haswa wa kichwa tikiti, ajivikaye ukadhi
Vipi ujenzi wa miti, bila pori kunradhi
Mwaka Kogwa wakogwile, wayajua maadili?

Mwaka Kogwa wakogwile, wayajua maadili?
Kwenye jua kulekule, watuletea kandili?
Kwenye viota vya bure, unaleta ubahili
Stadi zizingatiwe, sanaa iendelee

Stadi zizingatiwe, sanaa iendelee
Kaditama niachiwe, niwaachie sherehe
Wadogo weshaambiwe, kwa tarehe kubalehe
Fani yengiwa utani, watenzi waso ughani
 
Hilo hapo juu ni darsa tosha la ushairi wa asili wa Kiswahili kwa kutumia vina na mizani.

Na changamoto kwa wote wanaosema Kiswahili hakina ladha.
 
Hilo hapo juu ni darsa tosha la ushairi wa asili wa Kiswahili kwa kutumia vina na mizani.

Na changamoto kwa wote wanaosema Kiswahili hakina ladha.

Kiranga mwenye maarifa, mbona wahodhi umalenga?
Kompanero hata arafa, yao haki karatasi kuzilenga!
Kwani lazima sharafa, kuwa nazo kila Malenga?
Kama wataka urefa, zako mizani peleka Kalenga!
 
Fani yengiwa utani, watenzi waso ughani
Uvundo uso ubani, wagenzi waso mizani
Ufundi uso na kani, wapenzi waso na shani
Iktisadi si idadi, shairi alimuradi ?

Iktisadi si idadi, shairi alimuradi ?
Tungo kazi ya stadi, usambe kwenda midadi
Afaleki kwenye jadi, pwani wapi Bariadi?
Si bora wa Takoradi, upwa ana kwa ahadi

Si bora wa Takoradi, upwa ana kwa ahadi
Wewe hata kwa bajaji, hujaipata taraji
Kuzama katika haji, bila alifu kipaji
Fani kutiwa dukizo, kwa malenga ni chukizo

Fani kutiwa dukizo, kwa malenga ni chukizo
Tenzi za uambukizo, washairi ni kimbizo
Fani kama maigizo, yalokosa uchagizo
Kuiharibu kalamu, kwa malenga ni haramu

Kuiharibu kalamu, kwa malenga ni haramu
Kamwe mpaka dawamu, milango ya Jehanamu
Kuondoa ufahamu, kwa chukizo za awamu
Watoto jifunze vina, shikizeni na mizani

Watoto jifunze vina, shikizeni na mizani
Virefu kama visima, vya enzi Mjeremani
Mjue chota hekima, ka vito vya Mererani
Kwa si haba taadhima, hapa mpaka Merekani

Kwa si haba taadhima, hapa mpaka Merekani
Mashairi kwa kupima, sio ukware wa ghani
Kimbi shairi kubina, kwa ngoma za baniani ?
Angalizeni kusoma, kabla kujitia homa

Angalizeni kusoma, kabla kujitia homa
Mje kutoka Musoma, kufika Ilala Boma
Vipi msipate noma, kutokujua ya Roma?
Vina na mizani kina, ni lulu ya mshairi

Vina na mizani kina, ni lulu ya mshairi
Najua kuna Wachina, watokuja kughairi
Lakini jadi kuchina, haiwezi Mswahili
Kama saa inagota, shairi lapiga mota

Kama saa inagota, shairi lapiga mota
Kama ni misheni kota, au Kinyasini sota
Ugwiji wataka tota, so mambo kuotaota
Mshairi hajifichi, mwanagenzi shusha hadhi

Mshairi hajifichi, mwanagenzi shusha hadhi
Haswa wa kichwa tikiti, ajivikaye ukadhi
Vipi ujenzi wa miti, bila pori kunradhi
Mwaka Kogwa wakogwile, wayajua maadili?

Mwaka Kogwa wakogwile, wayajua maadili?
Kwenye jua kulekule, watuletea kandili?
Kwenye viota vya bure, unaleta ubahili
Stadi zizingatiwe, sanaa iendelee

Stadi zizingatiwe, sanaa iendelee
Kaditama niachiwe, niwaachie sherehe
Wadogo weshaambiwe, kwa tarehe kubalehe
Fani yengiwa utani, watenzi waso ughani

Mkuu Kiranga, natoa shikamoo, kuonyesha heshima yangu kwako!

Hakika wewe ni malenga, uliesalia nyikani,

Nasema shikamoo Kiranga, japo Gaijin namuweka kwapani,

Simuweki kwapani kwa husda, bali ushindi huru na maamuzi huru,

Nasema Kiranga Shikamooo, wewe ni nguli uliesalia!
 
Kiranga mwenye maarifa, mbona wahodhi umalenga?
Kompanero hata arafa, yao haki karatasi kuzilenga!
Kwani lazima sharafa, kuwa nazo kila Malenga?
Kama wataka urefa, zako mizani peleka Kalenga!

Hodhi hadhi kazi kadhi, kasri si ubaazi
Pozi Pazi, nazi hasi, fasihi si ubazazi
Vipi mja wa usinga, ahutubu kwa luninga?
Seuze Kalenga, Mbinga, watatubu kwa ujinga

Fani wakifakamia, ni haki kuwaambia
Ng'ombe hajawa ngamia, jangwa kuliparamia
Katika johari mia, kumi hawajapatia
Waleta kuangamia, tungo rudi atamia
 
Back
Top Bottom