Ukosefu wa ladha ya lugha ya Kiswahili kwenye mapenzi

'nina hamu na wewe'

Nina hamu na wewe ni more like I want you than I miss you. Big difference based on a subtilty. Kuielewa vizuri "I miss you" inabidi uelewe it's flattering nature. "Nina hamu na wewe" inaondoa focus kwenye subject na inaweka kwenye predicate.

Nakuhitaji is more like it, but not quite, because it overreaches into "I need you" territory.

Kiswahili hatuna I miss you kwa tathmin yangu ya sasa.

Ngoja niangaze kwa wahenga na marasuli wa Kiswahili wamelizingatia hili kivipi.
 
SIKIZA MANENO MATAMU :

2.Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai;
3 Manukato yako yanukia vizuri; Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa; Kwa hiyo wanawali hukupenda.
4 Nivute nyuma yako, na tukimbie; Mfalme ameniingiza vyumbani mwake. Tutafurahi na kukushangilia; Tutazinena pambaja zako kuliko divai; Ndiyo, ina haki wakupende.
5 Mimi ni mweusi-mweusi, lakini ninao uzuri, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani.
6 Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi-mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
7 Nijulishe, ee mpendwa wa nafsi yangu, Ni wapi utakapolisha kundi lako, Ni wapi utakapolilaza adhuhuri. Kwa nini niwe kama aliyefungiwa kidoto, Karibu na makundi ya wenzako?
8 Usipojua, wewe uliye mzuri katika wanawake, Shika njia uzifuate nyayo za kondoo, Na kuwalisha wana-mbuzi wako Karibu na hema za wachungaji.
9 Mpenzi wangu, nimekulinganisha Na farasi katika magari ya Farao.
10 Mashavu yako ni mazuri kwa mashada, Shingo yako kwa mikufu ya vito.
11 Tutakufanyizia mashada ya dhahabu, Yenye vifungo vya fedha.
12 Muda mfalme alipoketi juu ya matakia, Nardo yangu ilitoa harufu yake.
13 Mpendwa wangu ni kama mfuko wa manemane Ukilazwa usiku maziwani mwangu.
14 Mpendwa wangu ni kama kishada cha hina, Katika mizabibu huko Engedi.
15 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu, U mzuri, macho yako ni kama ya hua.
16 Tazama, u mzuri, mpendwa wangu, Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;
17 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, Na viguzo vyetu ni miberoshi

SOURCE: pata ziada ya maneno matamu Swahili Holy Bible - Old Testament / SongsOfSolomon-2
 
Watu wanatiririka kwa vina vya kiswahili, hapa demu akichomoa itakuwa hajui kiswahili kabisa!
 
Nina hamu na wewe ni more like I want you than I miss you. Big difference based on a subtilty. Kuielewa vizuri "I miss you" inabidi uelewe it's flattering nature. "Nina hamu na wewe" inaondoa focus kwenye subject na inaweka kwenye predicate.

Nakuhitaji is more like it, but not quite, because it overreaches into "I need you" territory.

Kiswahili hatuna I miss you kwa tathmin yangu ya sasa.

Ngoja niangaze kwa wahenga na marasuli wa Kiswahili wamelizingatia hili kivipi.

Umeichambua vema lakini umetia najisi uchambuzi wako woooote baada ya kutumia lugha ya kimalkia!
 
Hivi ni kwa nini lugha inaonekana kukosa mvuto hasa kwenye suala la mapenzi? Utamwakaji wa maneno kama vile: nakupenda sana hauna mvuto kama vile '' i love you so much'' pia maneno kama vile '' i miss u baby'', ''honey'', ''darling'', ''baby'' na mengine unaweza kuongezea kiswahili chake kimekuwa utata.
bwana Shibuda(smb) mwajamvi humu?angetufaa saana hapa,kiswahili ni murua saana
 
Umeichambua vema lakini umetia najisi uchambuzi wako woooote baada ya kutumia lugha ya kimalkia!

Lugha ya kimalkia ndo ikoje? Malkia huyo mtu au malkia wa nyuki?

Na kama mtu, kwa nini lugha ya mtu iwe najisi? Au wewe mbaguzi wa lugha/ rangi?

Wenzetu wanatuonea gele kwa kuwa ndumilakuwili kwa sababu undumilakuwili huu wa lugha unapanua maoni, wewe unaona najisi kwa ufinyu wa mawazo uliopandikizwa na ubaguzi ambao hauna tofauti na wa NAZI au makaburu.

Najisi unaijua?

Kama unataka purity tengeneza intaneti yako ya makuti tujue unataka chako tu.

Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
 
Enzi za mada kuitwa mada..sio siku hizi porojo urojo mwingi hata mtu hutoki kwa kujifunza mengi.
 
nakupenda sana, lina uzito sana
mtu anaekwambia serious nakupenda sana ujue anakupenda kweli(hasa face to face)
tofauti na anaekwambia i love u, i love u ni neno jepesi kulisema hata mume wa mtu naweza mwambia i love you, kama ni uzito
basi nakupenda ni70%
na i love you ni30%

yapo maneno matamu ya kiswahili mengi sana
na ndio yanatumika
kingereza ni ajili ya kudeka.
 
Maneno ya kiswahili ni mazito kuyatamka na ukiyatamka lazima umaanishe unachokisema kutoka moyoni tofauti na haya maneno yenu mnayoyaita ya malkia wa nyuki ni kama wimbo tu ukimaliza unasepa zako
 
La Azizi, Mahabuba, wa ubani, mwandani wangu, asali wa moyo wangu, kidundisha moyo wangu, mboni yangu, nk..
zote husimama kumaanisha mpenzi..
Nitarudi kukuletea za kilugha..........
Kisukuma damu changu...
 
La Azizi, Mahabuba, wa ubani, mwandani wangu, asali wa moyo wangu, kidundisha moyo wangu, mboni yangu, nk..
zote husimama kumaanisha mpenzi..
Nitarudi kukuletea za kilugha..........
Tatizo zimekaa kinafki sana. (Sijui mkuu upo, sijui ushakufa anyway, kitambo sana
 
Hamjakutana tu na wenye mahaba yenu af wote mjue kudeka af woite mjue lugha af wote mjue mahaba!

Weeeeh!
 
Back
Top Bottom