Kwenye Lugha kuna mother tongue, kwenye mapenzi kuna First love, tunaita Main Base ya Mahusiano

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,892
KWENYE LUGHA KUNA MOTHER TONGUE, KWENYE MAPENZI KUNA FIRST LOVE, TUNAITA MAIN BASE YA MAHUSIANO.

Na, Robert Heriel
Mtibeli

Kila kitu duniani kina msingi wake. Ipo misingi imara na Ipo misingi dhaifu. Lakini msingi ni msingi tuu.

Unapoenda kuomba kazi watahitaji CV yako ili wapate kuuona Msingi wako ni upi. Msingi upo Chini kabisa, upo ndani kabisa. Yaani msingi ndio unatangulia Kabla ya mengine.
Kwenye ujenzi wa nyumba msingi ni lazima. Hata hivyo ujenzi wa nyumba za ghorofa, basement inatakiwa kuwa imara ili kubeba Floor zinazofuata.

Mapenzi ya siku hizi ninayafananisha na Ghorofa. Ni nadra Sana Kwa zama hizi kumiliki Mwanamke au Mwanaume ambaye wote ndio First love. Ni aidha uwe Floor ya tatu wengine mpaka Floor ya kumi Huko. Wengine hupata nafasi katika ghorofa za juu kwenye Jeddah Tower.

Elewa kuwa msingi hautegemei Floor, Ila Floor ndio zinategemea Msingi.

Katika Lugha, msingi Mkuu wa Lugha unaanzia kwenye Lugha ya Kwanza, ambayo huitwa Mother tongue,
Lugha ya Kwanza ndio itatoa muelekeo wa lafudhi ya mtu hata akijifunza Lugha zingine.
Mfano, Mhindi aliye - acquire Lugha ya kihindi kama Lugha ya Kwanza, Lugha Mama, siku akijifunza kingereza utaona athari ya Lugha yake Mama pindi akizungumza kingereza.

Au Msukuma au mchaga aliyezaliwa Huko Vijijini wapozungumza kichaga au kisukuma, aka- acquire Lugha ya Kiswahili, utaona athari ya kichaga/kisukuma pindi azungumzapo Kiswahili.
Hiyo ndio inaitwa Athari za msingi katika muelekeo wa Maisha ya MTU.

Katika mapenzi, Mpenzi wa mwanzo katika First love ndiye atakayetoa muelekeo wa Maisha ya Mahusiano yako.
Kuanzia mtazamo wako, hisia zako, Matendo yako katika mapenzi.

Zingatia kua, unapojenga nyumba kwenye msingi utajenga Kwa kuangalia Msingi. Yaani msingi ndio unakuwa reference na center ya maamuzi na Matendo yako.

Unapojenga uhusiano labda ni floor ya pili Kwa Mwanamke ambaye alishajenga basement (alikuwa First lover ) kaa ukitambua chochote utakachokifanya kitakuwa kinawekwa katika muelekeo wa aliyetangulia. Yaani utakuwa unalinganishwa Hii NI kumaanisha mapenzi ya Nyuma yatakuathiri Mpenzi wa Mbele. Hiyo Ipo natural.
Hata kisiasa, kiutawala, kiutamaduni, kijamii au kisayansi na Teknolojia.

Hata waisrael walipokuwa wakitoka Misri tayari walikuwa Wana basement ya kimisri ndio maana kila mara walikuwa wakikumbuka na kuona Bora warudi Misri. Sio ajabu Mungu aliwaua wote Kwa sababu Mungu angekuwa the second badala ya First, Msingi wa jamii hiyo.

Kisiasa, mataifa mengi unayoyaona Yana msingi wake. Ni lazima uujue huo msingi na mjenzi wa msingi huyo ni Nani. Kwa mfano Kwa hapa Tanzania Msingi Mkuu wa nchi umejengwa na Hayati Nyerere akiwa na wenzake, hivyo wengi wanaokuja Baada yake ni ngumu Kutoka kwenye msingi wake. Sio ajabu mpaka sasa wapo wananchi watakuambia angekuwepo Nyerere mambo yangekuwa mazuri, sio kwamba Nyerere hakuwa na madhaifu, nop, yalikuwepo Ila ishu ni Msingi wa nchi umejengwa na nani na Kwa namna ipi.

Kiutawala, unapochukua utawala au madaraka sehemu ambayo kulikuwa na utawala ni muhimu kama sio lazima kuondoa basement (msingi wa mtangulizi wako) ikiwapo wale Watu wa karibu wa Mtawala aliyetoka. Hiyo itakufanya utawala Kwa utulivu, na kama kutakuwa na changamoto basi zitakuwa ni zile za kawaida.

Elewa kuwa, binadamu ni kiumbe ambaye hapendi kukubali mabadiliko na hii ni Kutokana na mazoea.

Ni ngumu Kwa First lovers kugombana kiasi cha kutisha. Lakini ni Jambo linalotarajiwa Kwa Watu ambao sio First lovers kugombana ikiwezekana kumwagana Kwa urahisi.

Taikon Master ninashauri, kama vile ambavyo ukienda kuomba kazi utafanyiwa usahili WA kutosha ndivyo hivyohivyo unatakiwa unapotafuta Mwenza lazima uchunguze na kumjua mtangulizi wako ni Nani, au aliyejenga msingi Kwa Mpenzi wako huyo Mpya ni Nani?

Kwa sababu huyo ndiye ambaye amemuathiri pakubwa huyo unayemchumbia. Yeye ndiye Kwa kiais kikubwa amembebesha attitude iwe nzuri au Mbaya kuhusu mapenzi, yeye ndiye anamsingi WA mazuri au mabaya ya kihisia Kwa huyo Mwenza wako. Yeye ndiye anafalsafa ya mapenzi na Maisha Kwa huyo Mwenza wako.

Wahenga walisema awali ni awali na hakuna awali mbovu. Hao ni wahenga wanaweza kuwa right or wrong lakini Kwa muktadha wa mahusiano, kauli Yao Ipo thabiti.

Kosa kubwa wanalofanya wengi ni kujenga kwenye msingi ambao ni mbovu, lakini pia hawajui mjenzi wa huo msingi ni Nani,
Kiafya, jino likiuma ujue tatizo ni Mzizi wa jino. Namna pekee ya kudhibiti lisiume ni kung'oa jino na Mzizi, au kukata Mzizi WA jino kisha uzibe.

Sasa unakuta umeopoa Mwanamke ambaye aliyejenga msingi wa mapenzi alijenga msingi mbovu. Akamuacha, akaja mjenzi mwingine akapandisha Floor ya Kwanza, akaona kuna nyufa akakimbia, au Mwanamke akaona huyo Mwanaume sio mjenzi mzuri wakamwagana, akaja mwingine anajenga floor ya tatu, vivyohivyo mpaka mjenzi wa floor ya kumi ndio wewe ukajitokeza, unaona kabisa Ghorofa linanyufa au limepinda na muda wowote litaanguka lakini wewe unaamua kupandisha floor yako.
Badala ya aidha ulivunje jengo lote mpaka msingi uanze upya, au uachane na huo mradi. Wewe unang'ang'ania kisa tuu ni injinia. Sawa!

Mahusiano ya sasa ni hatari Mno ikiwa hakuna wajenzi Wazuri wa mahusiano. Mainjinia wa majengo wakikosekana ni kuhatarisha usalama.

Acha nipumzike sasa.

Ijumaa Kareem
Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Robert hii kitu ni kweli kabisa na ndio maana wataalamu wa mambo wanakwambia before huja m- date mtu fatilia angalau wanaume wake watatu wa mwisho , utapata kitu cha kukusaidia na kugundua una deal na mtu wa namna gani !
 
Unafanya mambo kuwa magumu sana,Ukishamjua aliyejenga msingi unafanyaje?Unamtafuta umjue ili umhoji au?na usipomjua inakuaje?

Mimi kazi yangu ni kurahisisha mambo Mkuu.

Neno langu sio sheria.

Iwe hata kwenye Dawa, Siasa, au Jambo lolote ni lazima uangalie foundation ya kitu Kabla hujaleta ujenzi au ujuzi wako.

Kupuuzia ndio kuleta ugumu

Wasalamu.
 
Uko sahihi, dada angu alianza mahusiano na kijana falani wa kishua, anaejifanya shar khan, walipoachana, dada akajua ule ndo uhalisia, kila anaempata anataka drama na matumizi ya kijinga. Alihangaika sana
 
Malezi(maisha ya utotoni kwa ujumla) pia yanachangia kwasababu yanatengeneza tabia flani ngumu kuzibadilisha. Zinaweza kua tabia mbaya
 
Mkuu ningependa kujua ratiba yako ya msosi kuanzia asubuhi hadi jioni, huwa unakula vyakula gani mara kwa mara, na huwa unakula kiasi gani

Asubuhi 6:00am, Naomba. Kisha nakunywa Nusu Lita ya maji ya vuguvugu.
6:30am naenda kupigwa na upepo wa Asubuhi au kutembea.
7:30 naandaa chai na mhogo, hapa nitakunywa aidha maziwa chapati, maji mhogo, au kiporo.
8:30 nakunywa chai.
9:00. Naingia kazini.
11:30 break ya Kazi, napiga Nusu Lita ya maji. Natoka kutembea kupigwa na upepo.

12:00- 15:00 nazurura mtandaoni
14:00 nakula zangu ugali au wali, maharage au dagaa au mchicha na katunda kakuzugia.

15:-16:30 naingia kazini tena.
17:00 natoka zangu kupigwa na upepo. Napiga Lita ya maji nyingine.
18:30: Nipo ndani nacheki movie
19:00. Nakunywa maji
19:00-19:30 Maombi ya jioni.
19:30-20:00. Nakula chakula cha jioni
20:00-22:00, Movie, mpira, games, familia, mtandaoni.
22:30- 05:59 kulala.
 
KWENYE LUGHA KUNA MOTHER TONGUE, KWENYE MAPENZI KUNA FIRST LOVE, TUNAITA MAIN BASE YA MAHUSIANO.

Na, Robert Heriel
Mtibeli

Kila kitu duniani kina msingi wake. Ipo misingi imara na Ipo misingi dhaifu. Lakini msingi ni msingi tuu.

Unapoenda kuomba kazi watahitaji CV yako ili wapate kuuona Msingi wako ni upi. Msingi upo Chini kabisa, upo ndani kabisa. Yaani msingi ndio unatangulia Kabla ya mengine.
Kwenye ujenzi wa nyumba msingi ni lazima. Hata hivyo ujenzi wa nyumba za ghorofa, basement inatakiwa kuwa imara ili kubeba Floor zinazofuata.

Mapenzi ya siku hizi ninayafananisha na Ghorofa. Ni nadra Sana Kwa zama hizi kumiliki Mwanamke au Mwanaume ambaye wote ndio First love. Ni aidha uwe Floor ya tatu wengine mpaka Floor ya kumi Huko. Wengine hupata nafasi katika ghorofa za juu kwenye Jeddah Tower.

Elewa kuwa msingi hautegemei Floor, Ila Floor ndio zinategemea Msingi.

Katika Lugha, msingi Mkuu wa Lugha unaanzia kwenye Lugha ya Kwanza, ambayo huitwa Mother tongue,
Lugha ya Kwanza ndio itatoa muelekeo wa lafudhi ya mtu hata akijifunza Lugha zingine.
Mfano, Mhindi aliye - acquire Lugha ya kihindi kama Lugha ya Kwanza, Lugha Mama, siku akijifunza kingereza utaona athari ya Lugha yake Mama pindi akizungumza kingereza.

Au Msukuma au mchaga aliyezaliwa Huko Vijijini wapozungumza kichaga au kisukuma, aka- acquire Lugha ya Kiswahili, utaona athari ya kichaga/kisukuma pindi azungumzapo Kiswahili.
Hiyo ndio inaitwa Athari za msingi katika muelekeo wa Maisha ya MTU.

Katika mapenzi, Mpenzi wa mwanzo katika First love ndiye atakayetoa muelekeo wa Maisha ya Mahusiano yako.
Kuanzia mtazamo wako, hisia zako, Matendo yako katika mapenzi.

Zingatia kua, unapojenga nyumba kwenye msingi utajenga Kwa kuangalia Msingi. Yaani msingi ndio unakuwa reference na center ya maamuzi na Matendo yako.

Unapojenga uhusiano labda ni floor ya pili Kwa Mwanamke ambaye alishajenga basement (alikuwa First lover ) kaa ukitambua chochote utakachokifanya kitakuwa kinawekwa katika muelekeo wa aliyetangulia. Yaani utakuwa unalinganishwa Hii NI kumaanisha mapenzi ya Nyuma yatakuathiri Mpenzi wa Mbele. Hiyo Ipo natural.
Hata kisiasa, kiutawala, kiutamaduni, kijamii au kisayansi na Teknolojia.

Hata waisrael walipokuwa wakitoka Misri tayari walikuwa Wana basement ya kimisri ndio maana kila mara walikuwa wakikumbuka na kuona Bora warudi Misri. Sio ajabu Mungu aliwaua wote Kwa sababu Mungu angekuwa the second badala ya First, Msingi wa jamii hiyo.

Kisiasa, mataifa mengi unayoyaona Yana msingi wake. Ni lazima uujue huo msingi na mjenzi wa msingi huyo ni Nani. Kwa mfano Kwa hapa Tanzania Msingi Mkuu wa nchi umejengwa na Hayati Nyerere akiwa na wenzake, hivyo wengi wanaokuja Baada yake ni ngumu Kutoka kwenye msingi wake. Sio ajabu mpaka sasa wapo wananchi watakuambia angekuwepo Nyerere mambo yangekuwa mazuri, sio kwamba Nyerere hakuwa na madhaifu, nop, yalikuwepo Ila ishu ni Msingi wa nchi umejengwa na nani na Kwa namna ipi.

Kiutawala, unapochukua utawala au madaraka sehemu ambayo kulikuwa na utawala ni muhimu kama sio lazima kuondoa basement (msingi wa mtangulizi wako) ikiwapo wale Watu wa karibu wa Mtawala aliyetoka. Hiyo itakufanya utawala Kwa utulivu, na kama kutakuwa na changamoto basi zitakuwa ni zile za kawaida.

Elewa kuwa, binadamu ni kiumbe ambaye hapendi kukubali mabadiliko na hii ni Kutokana na mazoea.

Ni ngumu Kwa First lovers kugombana kiasi cha kutisha. Lakini ni Jambo linalotarajiwa Kwa Watu ambao sio First lovers kugombana ikiwezekana kumwagana Kwa urahisi.

Taikon Master ninashauri, kama vile ambavyo ukienda kuomba kazi utafanyiwa usahili WA kutosha ndivyo hivyohivyo unatakiwa unapotafuta Mwenza lazima uchunguze na kumjua mtangulizi wako ni Nani, au aliyejenga msingi Kwa Mpenzi wako huyo Mpya ni Nani?

Kwa sababu huyo ndiye ambaye amemuathiri pakubwa huyo unayemchumbia. Yeye ndiye Kwa kiais kikubwa amembebesha attitude iwe nzuri au Mbaya kuhusu mapenzi, yeye ndiye anamsingi WA mazuri au mabaya ya kihisia Kwa huyo Mwenza wako. Yeye ndiye anafalsafa ya mapenzi na Maisha Kwa huyo Mwenza wako.

Wahenga walisema awali ni awali na hakuna awali mbovu. Hao ni wahenga wanaweza kuwa right or wrong lakini Kwa muktadha wa mahusiano, kauli Yao Ipo thabiti.

Kosa kubwa wanalofanya wengi ni kujenga kwenye msingi ambao ni mbovu, lakini pia hawajui mjenzi wa huo msingi ni Nani,
Kiafya, jino likiuma ujue tatizo ni Mzizi wa jino. Namna pekee ya kudhibiti lisiume ni kung'oa jino na Mzizi, au kukata Mzizi WA jino kisha uzibe.

Sasa unakuta umeopoa Mwanamke ambaye aliyejenga msingi wa mapenzi alijenga msingi mbovu. Akamuacha, akaja mjenzi mwingine akapandisha Floor ya Kwanza, akaona kuna nyufa akakimbia, au Mwanamke akaona huyo Mwanaume sio mjenzi mzuri wakamwagana, akaja mwingine anajenga floor ya tatu, vivyohivyo mpaka mjenzi wa floor ya kumi ndio wewe ukajitokeza, unaona kabisa Ghorofa linanyufa au limepinda na muda wowote litaanguka lakini wewe unaamua kupandisha floor yako.
Badala ya aidha ulivunje jengo lote mpaka msingi uanze upya, au uachane na huo mradi. Wewe unang'ang'ania kisa tuu ni injinia. Sawa!

Mahusiano ya sasa ni hatari Mno ikiwa hakuna wajenzi Wazuri wa mahusiano. Mainjinia wa majengo wakikosekana ni kuhatarisha usalama.

Acha nipumzike sasa.

Ijumaa Kareem
Nawatakia maandalizi Mema ya Sabato.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Suluhisho ni kuoa bikra ili kuhepuka kulinganishwa, japo huu huwa ukweli mchungu.
 
Back
Top Bottom