Ilikuwa ni siku ya lugha adhimu, lugha ya Kiswahili

FIKRA NASAHA

Member
May 22, 2023
7
5
Hii ni Aburani na ahadi Iliyowekwa Siku za Nyuma na Umoja wa Mataifa, Kuwa Kutakuwa na Siku Maalumu ya Kusheherekea Lugha ya Kiswahili Duniani Kila Mwaka.

Hii ni Abra nzuri kwa sisi wazungumzao lugha hii Adhwimu ya Kiswahili kujadili Mustakabali mzima wa lugha yetu.

Basi na Sisi Waswahili Tuwe na tabia ya Kuabtadisha jambo hili kila siku na si tu kupiga Porojo na Ndarire bila Ndaro na kusogora kwa yasiyo na maana.

Siku Hii Ilivutia Rika Mbalimbali, Wazee Wabobevu, Maghulamu, Mabanati, Vijulanga na Vichugandevu, kulikuwa na Mtanange wa Ulumbanaji wa lugha na Kutongoa Mashairi.

Yakajadiliwa mengi kuhusiana na lugha yetu ya Kiswahili, japokuwa huku mitaani lugha inakwenda Benibeni na Arijojo, wazungumzaji wengi tukizungumza Shelabela, kiasi ukajiuliza; wapo wapi Mbuji na Wambukuzi wa Kiswahili...!

Basi napenda tuwe Unyounyo, Sako kwa Bako kwenye kukienzi Kiswahili, binafsi ninapowaona magwiji wa lugha basi usimamisha masikio yangu kama Sungura aliyeona mbwa wa Msasi, ninakuwa Angeange kusikiliza, sina ngoma sina maulidi, nitasikiliza kinachojiri hapo kwa Mpororo bila Majaka kwenye hayo majadiliano, tena mjadala ukiwa hauna Makorowezo ya kupoteza, basi najihisi nazama kwenye bahari ya maziwa na asali, najichotea bila kipimo.

Siku hii ya tarehe Saba Mwezi wa Saba ya Mwaka huu, Kulikuwa na Magwiji Walioturovya Rovurovu na Kututebweresha Tebwele kwa maneno yao Debwedebwe ikawa ni Dafina kwetu wasikilizaji, nasi tukawa kama bisikuti ndani ya Kiowevu kwa hoja zao Wabobevu Tondowevu Tondozi.

Basi tusiwe kama mfinyanzi kulia Kigaeni, maana Mzungu wa kula Hafundishwi mwana. Lugha ya Kiswahili ni sawa na Dunga pana na imara kuna mengi sana ya kujifunza.

Wale Masombombi walikaa mbali nasi, Viranja walikaza Sombo na Kusombogoleka, tukiwa tayari kabisa kuulinda Mtanange.

Maana Huwezi Icheza Ngoma na Mzigo Kichwani.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom