Ukosefu wa ladha ya lugha ya Kiswahili kwenye mapenzi

nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,273
3,750
Hivi ni kwa nini lugha inaonekana kukosa mvuto hasa kwenye suala la mapenzi? Utamwakaji wa maneno kama vile: nakupenda sana hauna mvuto kama vile '' i love you so much'' pia maneno kama vile '' i miss u baby'', ''honey'', ''darling'', ''baby'' na mengine unaweza kuongezea kiswahili chake kimekuwa utata.
 
Ushenda mwambao weye nitonye ?

Kiswahili kina maneno bora na matamu ya mapenzi..na unasema bila kung'ata ulimi...

mathalani neno "mpenzi" ukilisema vyema, waweza stua hata vilivyo lala.

Ndo mana latumika kwa mtu wa jinsia moja kuelezea hisia zake kwa mtu wa jinsia nyingine, tofauti na neno "dear" ambalo hata boss wako wa kiume akikuandikia e-mail anakuita hivyo, nawe utakuwa unamchekea chekea tu....
 
Last edited by a moderator:
La Azizi, Mahabuba, wa ubani, mwandani wangu, asali wa moyo wangu, kidundisha moyo wangu, mboni yangu, nk..
zote husimama kumaanisha mpenzi..
Nitarudi kukuletea za kilugha..........

Ni kweli lakini haya maneno yako kwa wachache tu tulio wengi tunajua darling, honey, i miss you n.k. Ule utamkwaji sio wote wanaojua
 
Ni kweli lakini haya maneno yako kwa wachache tu tulio wengi tunajua darling, honey, i miss you n.k. Ule utamkwaji sio wote wanaojua

Kwa hiyo tatizo si ukosefu wa ladha ya lugha, bali ni watu kutojua lugha.
 
Back
Top Bottom