DHANA YA UKOMBOZI WA MWANAMKE BADO NI TATA.
- ASASI NYINGI ZIMEANZISHWA KUWEKA MIKAKATI YA KUMKOMBOA
MWANAMKE.
- WANAWAKE WENGI WAMEINGIA MADARAKANI KWA KUWAAHIDI UKOMBOZI
WANAWAKE WENZIE.
- WANASIASA MAJUKWAANI WANASISITIZA UKOMBOZI WA MWANAMKE.
MIMI NAOMBA MNIELEWESHE,
- HIVI WANAWAKE WAKO UTUMWANI?
KAMA NI KWELI MWANAMKE YUKO UTUMWANI, ILI KUJIKOMBOA MWANAMKE ANAHITAJI KUMJUA ADUI YAKE.
BASI NIJULISHENI;
- NANI ADUI WA MWANAMKE ALIYEMTIA UTUMWANI?
Exaud J. Makyao
0784347001
Na kweli unahitaji kueleweshwa. Sijui unaishi ulimwengu gani. Binafsi, inanitia uchungu. Hivi, mfano, ulishawahi kusafiri kwa kutumia daladala na ukasikia hata kama wanaume wanagombana, lakini tusi litahusu "tabia fulani ya kike au sehemu zake za siri?" Nadhani uko familia na tusi kama: 'Ku****ko' na siyo 'm*** ya ****ko'
Imagine unasafiri na mama yako, dada yako, mke wako, mtoto wako wa kike au mwanamke yeyote, je kwako hayo hayahitaji ukombozi?
Baadhi ya dini zinamwona mwanamke kama "mtu mchafu" kwa vile wakati fulani anatokwa na damu sehemu zake za siri na siyo mwanamme anapotokwa na damu puani. Je, unasemaje kwa hilo?
Familia nyingi wanawake/watoto wa kike wanawekewa amri kali kuliko wanaume/watoto wa kiume ikiwa ni pamoja katika kula - mwanamke anamwandalia mwanamme chakula; mwanamme anakula chakula kizuri zaidi kuliko mwanamke; mwanamme anapewa kiti akalie na mwanamke anakaa chini; mwanamke anampigia magoti mwanamme; mwanamke anawekewa muda wa kurudi nyumbani na mwanamme hana muda maalum - akichelewa ana 'excuses' na mwanamke inabidi azikubali.
Lakini mwanamke akichelewa mwanamme siyo rahisi kukubali 'execuses'; mwanamme akifumaniwa anaweza kuomba msamaha na mwanamke akamkubali tena; mwanamke akifumaniwa mara nyingi anapigwa hadi kufa au anaachika.
Pia watoto wa kike wanauzwa. Kama kwenye familia fulani kuna watoto wa kike wengi mtu anaona atatajirika kwa mahari kuliko kuwa na watoto wa kiume tu. Pia baadhi ya familia kumsomesha mtoto wa kike ni hasara kuliko wa kiume.
Nafasi fulani hawapewi wanawake siyo kwa sababu ya uwezo wao ila kwa sababu ya 'prejudice' tu na wakati mwingine tunawaaminisha kuwa wao ni dhaifu na wanaume siyo.
Hata tunatafsiri maandiko matakatifu vibaya kwa kusema: dhambi iliingia duniani kupitia mwanamke au barua za Paulo (out of context) tukisema... 'enyi wanawake watiini waume zenu' lakini hatusemi kile Paulo alichosema kwa wanaume: 'enyi wanaume wapendeni wake zenu.'
Kwangu mimi: ukimpenda mtu utamtii kwa mema; na kama utamtii kwa hayo mema, ina maana unampenda. Kwa hiyo, tafsiri nzuri: ni 'enyi wanandoa pendaneni na heshimianeni'.
Kuna pia misemo kama: unalia kama mwanamke; una'behave' kama mwanamke etc. Kuna mifano mingi sana. Inawezekana kwa hayo yote wewe unaona hamna shida kabisa lakini kama kweli unampenda mke wako, mama yako, dada yako au mwanamke yeyote usingependa adharirishwe kwa sababu ya maumbile yake au kwa vile yeye ni mwanamke. Au unasemaje?