SMU
JF-Expert Member
- Feb 14, 2008
- 9,613
- 7,902
DHANA YA UKOMBOZI WA MWANAMKE BADO NI TATA.
- ASASI NYINGI ZIMEANZISHWA KUWEKA MIKAKATI YA KUMKOMBOA
MWANAMKE.
- WANAWAKE WENGI WAMEINGIA MADARAKANI KWA KUWAAHIDI UKOMBOZI
WANAWAKE WENZIE.
- WANASIASA MAJUKWAANI WANASISITIZA UKOMBOZI WA MWANAMKE.
MIMI NAOMBA MNIELEWESHE,
- HIVI WANAWAKE WAKO UTUMWANI?
KAMA NI KWELI MWANAMKE YUKO UTUMWANI, ILI KUJIKOMBOA MWANAMKE ANAHITAJI KUMJUA ADUI YAKE.
BASI NIJULISHENI;
- NANI ADUI WA MWANAMKE ALIYEMTIA UTUMWANI?
Exaud J. Makyao
0784347001
Nadhani majibu yapo katika historia ya uumbaji (kama unaamini katika historia hiyo).
Mwanaume aliumbwa kabla ya mwanamke hivyo toka mwanzo anadhani ana haki zaidi ya mwanamke: Nadhani hili pia unaweza kuliona kwa binaadamu mpaka leo. Wale wenye umri mkubwa wana tend kujiona bora zaidi kulio wenye umri mdogo.
Mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanaume na si kinyume chake ('...nitakuletea msaidizi wa kufanana nawe'): Hili linapelekea wakati mwingine mwanaume kumuona mwanamke kama chombo tu ana si mwenza katika maisha!
Baada ya uasi pale edeni laana aliyopewa mwanake ni tofauti na mwanaume. Mwanamke aliambiwa atazaa kwa uchungu, tamaa yake itakuwa kwa mumewe nae atamtawala!
Wakati mwanaume ameamriwa kumpenda(nadhani mungu alijua mwanaume atapata shida kupenda kwa dhati) mkewe, Mwanamke yeye amuheshimu mumewe. Ukitizama utaona matatizo mengi katika ndoa yanasababishwa na wanandoa kushindwa kuyaishi maamrisho haya. Hata hayo matatizo uliyoyataja hapo juu yanatokana na tatizo katika eneo hili. Unawezaje kumtendea mabaya mtu unaempenda kwa dhati?
Nafahamu kuna watu wengi hawaamini katika historia hii, lakini ukitizama kwa makini kwa kiasi kikubwa yanaelezea kiini cha imbalance katika mahusiano baina ya wanaume na wanawake.