Haiti; Ndoto ya ukombozi iliyosafiri kutoka Afrika, ikawageuza watumwa kuwa watawala na watawala kuwa watumwa

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
HAITI; NDOTO YA UKOMBOZI ILIYOSAFIRI KUTOKA AFRIKA, IKAWAGEUZA WATUMWA KUWA WATAWALA NA WATAWALA KUWA WATUMWA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Sunday-16/10/2022
Himo, Kilimanjaro, Tanzania

Haiti ndio Taifa la Kwanza Duniani la watu weusi kujitangazia uhuru Mnamo mwaka 1804, ikawa ya kwanza ulimwenguni ambapo watumwa wenye asili ya Afrika walifanikiwa kupindua utawala wa Kizungu (Ufaransa) na kuwa huru, hii inamaana kuwa nchi ya kwanza yenye asili na Afrika kupata uhuru duniani ni Haiti.

Usisahau kuwa Haiti ndio Taifa la Kwanza Duniani kufuta kabisa utumwa, naomba niweke sawa hapa...

Utumwa ni mfumo unaotoa fursa kwa binadamu kummiliki binadamu mwenzake kama mali yake, Binadamu anayemilikiwa anakuwa na hadhi sawa na chombo au kifaa chochote kinachoweza kuuzwa.

Mfumo huu ulianza kabla ya uandishi kubuniwa, yani zama za kale, ukawa maarufu hasa kabla ya harakati za ukoloni duniani, kuanzia karne ya 15, ambapo watumwa walihitajika katika shughuli za kilimo na uchimbaji madini katika sehemu mbalimbali za ulimwengu.

Hivyo basi Haiti ni nchi ya kwanza duniani ambako watumwa wenye asili ya Afrika walifaulu kukomesha utumwa kabisa (totally abolished).

Iliwezaje kifanikisha mapinduzi ambayo yanayojulikana kuwa moja ya uasi mkubwa na uliofanikiwa zaidi wa watumwa katika Ulimwengu wa Magharibi.

Ilikuwa hivi...

Mnamo mwaka 1791, Waafrika waliokuwa watumwa waliwaasi mabwana zao ambao ni Ufaransa, waliasi na kuanzisha vita na kuwachakaza vibaya wazungu, ushindi huo uliifanya Haiti kuwa jamhuri ya kwanza ya watu weusi duniani.

Mapinduzi hayo yaliongozwa na mtumwa wa zamani, Toussaint L'Ouverture, ambaye alichukua jukumu kubwa katika kulishinda jeshi la Ufaransa mnamo 1801.

Lakini Toussaint L'Ouverture mwenyewe hakushuhudia uhuru alio upambania kwani aliuawa mwaka mmoja kabla ya uhuru wa Haiti, toka mwaka 1791 mapinduzi na maasi ya kupinga utumwa na kutafuta uhuru yalitamatika Haiti ilipo jitangaza rasmi uhuru wake mwaka 1804.

Aliyeogoza mapambano mpaka uhuru kupatikana baada ya kifo cha Toussaint L'Ouverture ni Jean-Jacques Dessalines.

Huyu Jean-Jacques Dessalines ndio alama ya uhuru kwa mtu mweusi duniani kote.

Huyu Jean-Jacques Dessalines alizaliwa mwaka 1758 na kufa miaka miwili baada ya uhuru wa Haiti yani mwaka 1806, huyu ndie mtawala wa kwanza wa Haiti, aliyeunda bendera ya taifa ya Haiti inayotumika mpaka sasa, ile nembo ya taifa iliundwa na Toussaint L'Ouverture, Jean-Jacques Dessalines akaiweka nembo ile katikati ya bendera yao.

Huyu alichukua uskani baada ya kifo cha kiongozi wa mapinduzi Toussaint L'Ouverture mwaka wa 1802, hivyo Luteni mkuu, Jenerali Jean-Jacques Dessalines, alijitangaza kuwa kiongozi wa mapambano na kuendeleza uasi mpaka alipo shinda na kutangaza Jamuhuri mwaka 1804.

Jean-Jacques aliposhika hatamu aliamuru kuuawa kwa wazungu wengi huko Haiti, mpaka leo wazungu humuita mwafrika mnyama kuliko wote duniani.

Huyu Jean-Jacques alikuwa na asili ya Kongo, lakini alilelewa na mama shujaa kutoka Benin (Dahomey), mama yake mlezi alikuwa ni Agbaraya Toya, huku mama yake mzazi alitokea Nigeria, ila hakuwahi kufahamika alipo ishilia na wala baba yake hajulikani ni nani.

Jean-Jacques Dessalines, alilelewa na Agbaraya Toya kutoka Dohomey ambayo ndio Benin ya sasa.

Yes ni Agbaraya Toya, mwana Mama shupavu kwenye historia ya dunia, mwanamke wa kwanza duniani kupewa cheo cha jeneral kwenye jeshi.

Najua unajiuliza hapa kivip mwanamke awe jeneral tena Afrika?, Ni kwamba huyu Agbaraya Toya ni mwanamke mwenye historia kubwa sana Afrika, alipewa heshima kubwa sana kwasababu ni mwana Mama aliyefanikiwa kupambana kwenye vita zaidi ya 59 na kuleta ushindi kote.

Sababu hiyo alipanda vyeo mpaka kufika cheo cha juu kabisa ndani ya Jeshi la ngome ya Dahomey, yes ni dola ya Dohomey, yani Benin ya leo.

Mfalme Dada Tegbessou alimpandisha cheo Agbaraya Toya kuwa Jenerali ( yani "gaou") katika Jeshi maalumu la wanawake.

Ngoja nieleze hapa kidogo...

Dohomey ndio Benin ya sasa, ndio dola pekee Afrika kipindi hicho lilokuwa tishio Afrika magharibi, ilikuwa na jeshi kubwa na lenye mbinu za kivita za kipekee, ilitengeneza jeshi la tabaka tatu, moja, ni jeshi la vijana lenye mafunzo ya hali ya juu, jeshi hili lilikuwa na askali 20000.

Pili ni jeshi la askali wa kike, hawa waliitwa "Agojie" hawa walikuwa askali muhimu sana wa mfalme, walipewa mafunzo ya siri na ya hali ya juu, walitumiwa kwenye vita ngumu na yenye vikwazo vingi, inakadiliwa kuwa na askali zaidi ya 6000, movie ya "The woman King" inasanifu uimara na uwezo wa jeshi la wanawake huko Dohomey.

Tatu, jeshi mchanganyiko, hili lilikuwa jeshi lenye askali wote yani askali wa wakike na kiume.

Mfalme wa Dahomey, Dada Tegbessou alimteua Agbaraya Toya kuwa jeneral wa jeshi lote la Dohomey na mkuu wa kikosi cha askali wa kike ambalo mfalme alikuwa na imani sana juu ya Jeshi hilo.

Sasa basi...

Mnamo mwaka 1753, kijiji cha abekuta, kilivamiwa na wafanyabiashara ya utumwa, baada ya mapigano makali jenerali Toya alifanikiwa kuwachakaza vibaya sana baadhi ya wanaume kwenye vita hiyo.

Bahati mbaya jeshi la Dohomey lilizidiwa nguvu baada ya usaliti wa dola ya jirani ya Edo, ikapelekea Agbaraya Toya kukamatwa na kufungwa, kisha kusafirishwa kama mtumwa.

Lakini kila jambo lina faida na hasara kuna methali ya Kiirani usema " Linaweza waijia jambo baya lakini likawa ndio uokovu wako baadae".

Hivyo kusafirisha kwa Agbaraya Toya utumwani ndio ikawa nusura ya huko aendako, tutaliona hili baadae kidogo, hivyo Toya alisafirishwa kutoka Dahomey hadi Sant Domingue ambapo ndio Haiti ya sasa.

Baada ya kufika Haiti, Toya alinadiwa kwenye mnada maalumu wa kuuza watumwa, hatimaye Toya alinunuliwa kama mtumwa, baada tu ya Toya kununuliwa, Toya alitoroka na kukimbila msituni, huko alitumia usiku na mchana kufundisha Jeshi lake ili waweze kujikomboa, ilishindikana kwa kuwa hakupata aina ya watu anaowataka.

Hatimaye Toya wakati yupo msituni alikutana na mwanamke alikuwa anataka kujifungua, Mwanamke yule alijifungua salama lakini alimuomba Toya amchukue mtoto yule ili amlee, kwasababu yeye alikuwa mtumwa na asingeweza kuishi na mtoto huyo.

Toya alichukua jukumu la kumlea mtoto yule wa kiume, lakini aliamua kurudi kule mashambani kwenye chakula kingi ili akamlee mtoto na kumfunza mtoto yule mbinu mbalimbali za kivita ipasavyo.

Toya alimfumfunza mtoto yule lugha ya Yoruba, sayansi ya vita, sanaa ya muziki na kuchora, Toya alimuita yule mtoto jina la "Koupe tet-boule kay” lenye kutokana na lugha pacha (Haitian Kreyòl) ambalo maana yake ni "kata kichwa na vunja na choma nyumba zao" (means “cut off their heads, burn down their houses") lakini alipo batizwa akaitwa Jean–Jacques Dessalines.

Baadae kidogo Jean–Jacques Dessalines alitenganishwa na mama yake mlezi baada ya Agbaraya Toya kupelekwa mbali.

Mtoto wa nyoka ni nyoka, Jean–Jacques Dessalines alipokuwa mkubwa akaanzisha vuguvugu la uasi, akaungana na Toussaint L'Ouverture wakakusanya waafrika watumwa na kuunda kikosi cha uasi.

Wakahamia mstuni na kutoa mafunzo ya mapigamo, mwaka 1790 wakaanzisha uasi, wakachoma mashamba, unguza nyumba za wazungu na kuwaua wazungu kadhaa, Ufaransa kuona hivyo ikatangaza vita na watumwa, ikatuma askali na vita ikatokea rasmi mwaka 1791.

Mwaka 1803 Toussaint L'Ouverture alifariki na Jean–Jacques Dessalines kuwa kamanda mkuu wa jeshi, mwaka mmoja baadae yani 1804 Haiti ikajitangazia Uhuru na Jean–Jacques Dessalines kuwa raisi kwa kwanza wa Haiti.

Jean–Jacques Dessalines aliishindwa vibaya sana Ufaransa kwenye vita, mama yake Toya alifariki June 12, 1805, mwaka mmoja baada ya uhuru wa Haiti, alifanikiwa kuona ndoto yake ya kuwakomboa watumwa ikitimia kupitia mwanae.

Mwanamama Agbaraya Toya aliwekeza fikra ya ukombozi kwa mwanae Jean–Jacques Dessalines, ambae nae alikamilisha ndoto ya mama yake ya kuwageuza watumwa kuwa watawala na watawala kuwa watumwa, ndoto ya ukombozi ilisafiri kutoka Dohomey-Benin mpaka Haiti.

Haiti ni damu ya Afrika ambayo imeandika historia kwa kalamu ya damu na dhahabu yenye heshima katika historia ya taifa huru la watu weusi.

Na kutimiza ndoto ya ukombozi iliyosafiri kutoka afrika na kuwageuza watumwa kuwa watawala na watawala kuwa watumwa.

Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu kwa gharama ya Tsh 3000/=.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu

Kwa Tanzania
+255679555526 (WhatsApp).
+255765026057.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com

Copyright 2022, All Rights Reserved.

Maktaba Kuu.View attachment 2388850View attachment 2388848View attachment 2388847View attachment 2388846View attachment 2388849View attachment 2388851
FB_IMG_1665901091484.jpg
 
Andiko lako lina mapungufu. Mfano mimi ambaye ndo mara ya kwanza kusikia Haiti nitajua ni kitu gani hiki? Kama ni nchi inapatikana sehemu au bara gani hapa duniani?
Hayo ni Mapungufu yako, sio kazi yangu hiyo, hilo ndio uwaponza Watanzania wengi hupenda vitu vilivyo iva....

Unaposoma jambo usimalize hapo, nenda vyamzo vingine kujilizisha kile ulichosoma kuwa ni kweli? Sio unasoma kwangu kisha unabena elimu hii unaenda nayo huko vijiweni, ukifika huko unaanza kiluitema kama ulivyo meza, kama ni matango pori utayatema hivyo hivyo.

Katika kujifunza hakikisha unajifunza kanuni moja iitwa "certification" ukisoma kitu nenda kajiridhushe ulichosoma kama unataka kujifunza kuhusu hicho ama kimekuvutia, hii itakusaidi kuhifadhi kitu sahihi na kujua zaidi ya pale awali.
 
Andiko bora ahsante mwandishi.
Haiti nchi ya Africa iliyo mbali na Africa
 
Andiko lako lina mapungufu. Mfano mimi ambaye ndo mara ya kwanza kusikia Haiti nitajua ni kitu gani hiki? Kama ni nchi inapatikana sehemu au bara gani hapa duniani?
Haiti ipo Caribbean ni nchi maskini sana na wanapenda uloz sanai(vodoo)
 
Andiko lako lina mapungufu. Mfano mimi ambaye ndo mara ya kwanza kusikia Haiti nitajua ni kitu gani hiki? Kama ni nchi inapatikana sehemu au bara gani hapa duniani?
Dunia ya sasa imebadilika na kuwa rahisi zaidi bhana.
Mleta mada ni chanzo cha elimu, hivyo ukiona kuna jambo haulielewi katika topic mfano hiyo nchi ya Haiti, usimlaumu mtoa mada, si unabofya tu google jibu unalipata?
 
Andiko lako lina mapungufu. Mfano mimi ambaye ndo mara ya kwanza kusikia Haiti nitajua ni kitu gani hiki? Kama ni nchi inapatikana sehemu au bara gani hapa duniani?
Upo hapo kuangalia makosa madogo madogo! Ulipaswa kwanza kumpongeza mwandishi!
 
Andiko lako lina mapungufu. Mfano mimi ambaye ndo mara ya kwanza kusikia Haiti nitajua ni kitu gani hiki? Kama ni nchi inapatikana sehemu au bara gani hapa duniani?
Are you serious!? Kama ni kweli basi elimu Yako Ina mapungufu
 
Cry for Haiti!! Taifa limeparaganyika panya rodi wa Haiti wameizidi nguvu serikali Yao mpaka UN inataka kupeleka polisi kutoka Kenya!?? Waafrika nani katuroga!?
 
Back
Top Bottom