Uko vipi na mama mkwe wako?

Uko vipi na mama mkwe wako?

Niko kwenye mahusiano ambayo nimetambulishwa ukweni na ni mara ya kwanza kuwa karibu na mama mkwe.

Ila shida inakuja mama mkwe kama ananinyenyekea sana kitu ambacho sitaki kuona mama mkwe akifanya hivyo.

Napenda mama mkwe kuwa kama mshikaji, story nyingi sana yaani tuwe marafiki.

Kila ninapohisi hali hiyo ya kuninyenyekea, mimi naweke mambo sawa lakini mama mkwe anashindwa kusoma nyakati.

Vipi ulitumia mbinu gani kuwa karibu na mama mkwe wako au unaishi vipi na mama mkwe wako?.

JF
Sasa si ndio vizuri akiwa anakuheshimu hivyo?

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Ni vyema ukajua utamaduni wa kabila fulani kabla ya kutaka kuanzisha utaratibu wako,kikwetu mama mkwe hamtakiwi hata kuangaliana usoni,maongezi yanafanyika kila mmoja amekaa sehemu yake,we unataka mzoeane ili iweje?
Mmewangu akitaka kuongea na mama yangu anajipanga haswa utasema kuna interview huwa nacheka sana

Ni vizuri kujifunza.
Nimeelewa
 
Ebhana nimeoa familia yenye watoto wakike tu kwahyo mama mkwe aliniambia kabisa kuanzia leo ww ni mwanangu wa kiume nakukaribisha kwenye familia kama nimepata mtoto wa kiume kwahyo kuna mambo mengi tunashirikishana ila cha msingi kuheshimu mipaka kama ilivyo kwa mama yangu ndivyo ninavyofanya kwa mama mkwe
 
Ndio na mimi ninachotaka yaani mimi kuwa kama sehemu ya familia.

Lakini mtazamo wa wengi wanasema si vyema.

Nimewaelewa na nitaenda na hilo cos inawezekana na mama mkwe nae ana mtazamo huo.
 
Ndio na mimi ninachotaka yaani mimi kuwa kama sehemu ya familia.

Lakini mtazamo wa wengi wanasema si vyema.

Nimewaelewa na nitaenda na hilo cos inawezekana na mama mkwe nae ana mtazamo huo.
Hasa familia zisizo na mtoto wa kiume au unakuta mtoto wa kiume alishakata kamba ww ndio unakua kama mtoto wa mama mkwe na kama unamambo yalionyooka(unajielewa) inakua faraja kwake
 
Mleta mada huo ukaribu unao usema unapatikana huko, uwanja wa fisi, tandale kwa mwajuma ndala ndefu, na goba kwa Halima peku peku, na sehemu nyingi kama hizo

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Niko kwenye mahusiano ambayo nimetambulishwa ukweni na ni mara ya kwanza kuwa karibu na mama mkwe.

Ila shida inakuja mama mkwe kama ananinyenyekea sana kitu ambacho sitaki kuona mama mkwe akifanya hivyo.

Napenda mama mkwe kuwa kama mshikaji, story nyingi sana yaani tuwe marafiki.

Kila ninapohisi hali hiyo ya kuninyenyekea, mimi naweke mambo sawa lakini mama mkwe anashindwa kusoma nyakati.

Vipi ulitumia mbinu gani kuwa karibu na mama mkwe wako au unaishi vipi na mama mkwe wako?.

JF

Wewe kaa na Mama mkwe kama alivyo, achana na Phantasy za kihuni za mtaani, Heshima toka kwa Mama mkwe ni sawa.

Na hao wa Mama Mkwe hawana maana, usiwatilie maanani, bado una safari ndefu sana ngumu naye.

Kaa kwa machale, la sivyo ukijidai na bla bla utavuruga mambo yako kwa kupambana na ukweni.
 
Mama mkwe yeyeto asiyenufaika na ndoa ya bintie anayo chance ya kuibomoa ndoa ya bintie
 
Back
Top Bottom