Watibeli tunaruhusiwa Kulala Ukweni. Hatuna huo Mwiko

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
39,741
Reaction score
92,197
WATIBELI TUNARUHUSIWA KULALA UKWENI. HATUNA HUO MWIKO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Zipo jamii au makundi ya watu ambayo kwao ni mwiko kulala Ukweni. Kwao ni jambo aibu. Mila hiyo imerithishwa toka kizazi hata kizazi

Yaani mwanaume akiposa mke. Basi mwanaume huyo hatakiwi kulala Ukweni.
Na wazazi wa binti hawatakiwi kwenda kulala kwa kijana aliyemposa binti yao.

Sisi Kwetu, Naam Watibeli hatuna desturi kama hiyo.

Mwanaume wa kitibeli, akiwemo mimi Mtibeli OG, sisi tunaweza kulala ukweni, kwa binti ambaye tumeoa. Tukalala fofofo kabisa bila tatizo kama tupo nyumbani

Pia sisi wazazi Wakitibeli tunauwezo wa kulala kwa Wakamwana(wakwilima) bila tatizo lolote. Tukalala kama tupo nyumbani.

Tunapooa mwanamke hatumnunui. Kule tulipoolea hatupafanyi kuwa daraja la pili. Sisi kama Watibeli hatuna sababu hata moja ya kutuzuia kulala ukweni.

Unapooa binti yetu, unaruhusa kuja kulala kwetu. Sisi ni kama Wazazi wako. Wewe ni kijana wetu.

Sisi wazazi wa binti yetu tunaruhusa ya kuja kulala huko mnapoishi ila kwa kuzingatia masharti yenu. Labda kama ni maskini, mnajitafuta na hamna sehemu ya kulaza wageni.

Sisi ni Watibeli. Na yeyote atakayeoa binti zetu lazima iwe imethibitishwa kwamba anavigezo na sifa za kuwa mtibeli. Na watibeli hatuko limited na mambo yaliyo nje ya Haki, ukweli, upendo na Akili.

Kama Mtoto hana makazi ya kutosha kukidhi wageni wake. Ni kweli Sio mkwe tuu bali hata mzazi wake hapaswi kuja kumtembelea.
Unachumba kimoja, au viwili unaishi na mkeo/mumeo hakuna haja ya Mkwe wako na wazazi wako kuja kulala hapo.

Au Wakwe zako wana nyumba ndogo na wanamakazi yasiyo weza kuwatosheleza wote. Ni kweli haitakiwi uende ukweni, au kwa wazazi wako na mkeo/mumeo.
Na kama mtaenda mtalala nyumba ya jirani au makazi ya jirani.

Sio dhambi, sio jinai. Sio aibu kulala Ukweni.

Kama mkeo analala kwenu, wewe ni nani usilale kwao? Kama sio ujinga unaokusumbua kichwani, kama sio ubinafsi unaokusumbua moyoni, kiburi.

Kuna wale wanaume wajinga wenye upeo mdogo, au wafungwa na watumwa wa mitazamo potofu. Wanasema, mimi ni mwanaume siwezi lala ukweni.
Sasa ukilala ukweni uanaume wako unapungua wapi? Ni mitazamo ya watu walioshimoni, gizani.

Karne hii sio rahisi kukuta mtu mwenye mtazamo kama huo. Isipokuwa wale wabinafsi, elimu ndogo, akili finyu, watumwa.

Watibeli tulisema, mwanamke na mwanaume ni sawa lakini hawalingani kiwajibu na kimajukumu.

Mwanamke ni kiongozi katika umbile la kike.
Mwanaume ni kiongozi katika Umbile la kiume.

Kiongozi wa familia ni Mwanaume lakini kuongoza katika haki, ukweli, Akili na upendo.
Mkewe ni msaidizi wa mwanaume. Naye ni kiongozi. Hakuna aliyebora zaidi ya mwingine.

Wote ni bora katika nafasi zao.
Mmoja ni mke, mwingine ni Mume wote ni wamoja katika shilingi ileile.
Mmoja ni Baba(chanzo), mwingine ni Mama(Mlezi) wote ni wazazi. Hakuna aliyezaidi ya mwingine.

Sisi Watibeli, mtoto anaweza kuchukua majina ya Baba au ya Mama yake. Hakuna ile ya kuwa lazima mtoto achukue jina la Baba tuu. Hatuna kitu kama hicho. Kwa sababu sisi wote ni Watibeli.

Tunapooa hatutoi mahari. Wala binti zetu hawatolewi mahari. Hilo nilishalisemea na litabaki hivyohivyo. Hatutoi mahari kwa sababu mahari ni biashara ya kununua watu, ingawaje ukweli huo hawataki kuwasema kwa sababu ukweli kwao waliukataa na hawaupendi.

Sisi tunanunua Watumwa, tunanunua binadamu lakini kamwe hatuwezi kununua Mtu. Mtu hanunuliwi. Na hivyo kwa vile Watibeli ni Watu. Kamwe hawawezi kuuzwa au kununulika. Iwe kwa jina la Mahari au kwa majina mengine. Hiyo ni kinyume cha haki na miiko ya Kitibeli.

Binti za Tibeli ni watu huru. Wanauamuzi wa kuolewa na yeyote kwa hiyari na hawatatolewa mahari.

Huwezi lala nyumba ya Mtumwa au watumwa wako. Ndio maana zamani ilikuwa mwiko kulala ukweni. Sehemu uliyonunua mwanamke ukamfanya mkeo.

Sababu zingine ni pamoja na umaskini. Kuamka nyumba moja na mkweo na vijumba vyenyewe havipo vizuri vinaweza kuleta aibu za rejareja kama kuona utupu wa mkweo jambo ambalo lingehusishwa na laana(kwa tafsiri ya fedheha au ubaya).

Miongoni mwa watu waliolala Ukweni zamani katika Biblia ni pamoja na Nabii Musa.
Huyu alikaa Ukweni kwa zaidi ya miaka 10. Akiwa anaishi kwa Mkwewe kuhani Yethro, akiwa na mkewe Sipora.
Kwa wasiomjua Musa, alikulia jumba la kifalme la Misri kwa miaka zaidi ya 20, akatoroka na kukimbilia Kushi, huko akawa mfalme wa Kushi kwa miaka isiyopungua 20,
Kisha akaenda Midian akakaa kwa Yethro kwa miaka isiyopungua 10. Kisha akarudi Misri na kuwa mtawala wa Waisrael kwa zaidi ya Miaka 30.
Hiyo ni sehemu ya CV ya Nabii Musa.
Sasa unakuta mtu hata elimu hana, pesa hana, cheo hana, kutembea hajatembea anakuambia silali ukweni. Unabaki unamuangalia tuu. Sema unamuelewa kwamba ndio upeo wake ulipoishia.

Mtu mwingine ni Mfalme Daudi, huyu ameshakaa sana ukweni, kwa Mfalme Sauli. Licha ya kuwa na mahusiano ya Milka ya siri Kisha baadaye akawa mkewe kwa kuozeshwa na Mfalme sauli.
Tunazungumzia mfalme Daudi, mfalme kalala ukweni, sasa mtu kajamba nani anaongea vitu havielewi.

Nabii Yakobo, moja ya watu wenye majina Makubwa,yaani Israel. Huyu ndiye Israel OG, mwenye jina lake.
Sifa nzuri na mbaya za waisrael unazozijua, hao Waisrael na hilo jina unalolisikia. Huyu ndiye Baba yao.
Yakobo(Israel) ameishi Ukweni kwa zaidi ya miaka 14. Sio akilala tuu bali hata kumtumikia Mkwe wake. Alikuwa ameajiriwa na Mkwe wake, Labani ambaye pia ni Mjombaake.
Sasa wewe ambaye hata huna jambo la maana unakuta unakazania vitu ukiulizwa sababu nini, unambwela mbwela. Hujui hata ujibuje. Zaidi ya kusema mimi ni mwanaume mimi blah blah blah.

Sasa utakuwa mwanaume zaidi ya Musa? Daudi? Au Yakobo? Ambao CV zao zinatisha na hutoweza kuwapata hata kwa ukaribu.

Nataka kusema nini?
Lengo langu sio ujilinganishe na hao watu. Lengo langu sio ujilinganishe na Sisi Watibeli au watu wenye mifumo kama yetu.
Lengo langu ni kuwa usiwe mtu wa kukurupuka, kujifanyia fanyia mambo, kuwa na mtazamo fulani bila kufikiria kwa kina. Na huwezi kutetea hoja zako utakapoulizwa kwa nini?

Usiishie kusema ni utamaduni wetu. Usiishie kusema ni imani yetu inasema hivi. Usiishie kusema ni chama chetu kinasema hivi. Jiulize why, kwa nini uamini hivyo, kwa nini ndio msingi wa akili ulipo.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Nabii Musa alikimbia hukumu ya kuua Misri, na Yakobo alikuwa anamkimbia kaka yake Esau asimuue. Walilala ukweni kwa sababu walikuwa refugees na hawakuwa na pa kwenda.

Hukatazwi kulala ukweni ukiwa huna pakwenda!
 
Mtibeli hujakutana na Wenyeji?
Wakujuze zaidi usiyoyajua?

Mimi ni Mwenyeji,
Mwenyeji wa dunia,
Dunia ina mila,
Mila zina mipaka,
Mipaka ina sababu,
Sababu huhitaji mantiki.

Wewe Mtibeli,
Mtibeli unasema,
Unasema ni sawa,
Sawa kulala ukweni,
Ukweni hakuna mwiko,
Mwiko kwenu haupo.

Lakini kusikuwapo,
Kutokuwapo kwa mwiko,
Mwiko wa jamii yako,
Jamii yako si dunia,
Dunia si kabila lako,
Lako si kipimo cha wote.

Unasema Musa,
Musa aliishi kwa Yethro,
Yethro alikuwa mkwe,
Mkwe wa Sipora,
Sipora alikuwa mkewe,
Mkewe hakuthibitishi yote.

Unasema Yakobo,
Yakobo aliishi kwa Labani,
Labani alikuwa mjomba,
Mjomba na mkwe pia,
Pia alikuwa mwajiri,
Mwajiri si desturi tu.

Unasema Daudi,
Daudi alikaa kwa Sauli,
Sauli alikuwa mkwe,
Mkwe wa Mikali,
Mikali alikuwa mkewe,
Mkewe si hoja yote.

Tukio ni tukio,
Tukio si kanuni,
Kanuni huhitaji msingi,
Msingi huhitaji sababu,
Sababu huhitaji mantiki,
Mantiki huhitaji ushahidi.

Kama kwenu ni kawaida,
Kawaida iwe kwenu,
Kwenu hakuna mwiko,
Mwiko usiwe lazima,
Lazima kwa kila mtu,
Mtu ana utamaduni wake.

Usiposema silali,
Silali si ujinga,
Ujinga si kutofautiana,
Kutofautiana si upumbavu,
Upumbavu ni kukataa hoja,
Hoja bila kuichunguza.

Sisi WENYEJI tunasema,
Tunasema kwa mantiki,
Mantiki bila kejeli,
Kejeli si ushahidi,
Ushahidi ndio hoja,
Hoja ndiyo tunayohitaji.

Mtu ana mipaka,
Mipaka ina heshima,
Heshima ina utamaduni,
Utamaduni una tofauti,
Tofauti si ujinga,
Ujinga ni kukataa kufikiri.
 
Upo sahihi kwa kiasi fulani.

Musa alivyofanya mauaji. Alikimbia na kutoroka. Akiwa njiani alikutana na majeshi ya Kushi yakienda kuvamia miji ya Sudan. Akajiunga nayo. Baadaye akaja kuwa mfalme baada ya kutoa msaada wa kutosha na mfalme kufariki. Akaambiwa awe mfalme yeye kwa sharti la kumrithi mke wa mfalme na kuzaa naye. Sharti ambalo lilikuwa gumu kwani Musa alikataa. Na ndio sababu akafukuzwa tena kutoka Kushi,
Akakikimbilia Midiani. Huko ndio akakutana na binti Sipora akichunga mifugo ya baba yake.

Kisha Yethro alipomkaribisha Musa, Musa alijitambulisha hapo, ikajulikana amekimbia Misri na Kushi.
Yethro kwa kuogopa akamuweka Jela Musa chini ya shimo huko.
Huko akawa anapelekewa chakula kwa siri na Sipora.

Baadaye akatolewa. Akawa mchungaji wa mifugo ya Yethro. Kisha akamuoa Sipora na kuzaa naye watoto wawili.

Musa hakuwa na mpango wa kurudi Misri tena. Kwanza alishawasahau.
Kumaanisha hakuishi tena Midian kama mkimbizi bali mkazi na mkwe.

Ni wito wa Mungu ndio uliomuondoa Huko midiani na kurudi Misri kuwakomboa ndugu zake. Tena alikuwa hataki. Yaani hakukubali kirahisi mpaka aliposhawishiwa
 
Mtibeli hujakutana na Wenyeji?
Wakujuze zaidi usiyoyajua?

Mimi ni Mwenyeji,
Mwenyeji wa dunia,
Dunia ina mila,
Mila zina mipaka,
Mipaka ina sababu,
Sababu huhitaji mantiki.

Wewe Mtibeli,
Mtibeli unasema,
Unasema ni sawa,
Sawa kulala ukweni,
Ukweni hakuna mwiko,
Mwiko kwenu haupo.

Lakini kusikuwapo,
Kutokuwapo kwa mwiko,
Mwiko wa jamii yako,
Jamii yako si dunia,
Dunia si kabila lako,
Lako si kipimo cha wote.

Unasema Musa,
Musa aliishi kwa Yethro,
Yethro alikuwa mkwe,
Mkwe wa Sipora,
Sipora alikuwa mkewe,
Mkewe hakuthibitishi yote.

Unasema Yakobo,
Yakobo aliishi kwa Labani,
Labani alikuwa mjomba,
Mjomba na mkwe pia,
Pia alikuwa mwajiri,
Mwajiri si desturi tu.

Unasema Daudi,
Daudi alikaa kwa Sauli,
Sauli alikuwa mkwe,
Mkwe wa Mikali,
Mikali alikuwa mkewe,
Mkewe si hoja yote.

Tukio ni tukio,
Tukio si kanuni,
Kanuni huhitaji msingi,
Msingi huhitaji sababu,
Sababu huhitaji mantiki,
Mantiki huhitaji ushahidi.

Kama kwenu ni kawaida,
Kawaida iwe kwenu,
Kwenu hakuna mwiko,
Mwiko usiwe lazima,
Lazima kwa kila mtu,
Mtu ana utamaduni wake.

Usiposema silali,
Silali si ujinga,
Ujinga si kutofautiana,
Kutofautiana si upumbavu,
Upumbavu ni kukataa hoja,
Hoja bila kuichunguza.

Sisi WENYEJI tunasema,
Tunasema kwa mantiki,
Mantiki bila kejeli,
Kejeli si ushahidi,
Ushahidi ndio hoja,
Hoja ndiyo tunayohitaji.

Mtu ana mipaka,
Mipaka ina heshima,
Heshima ina utamaduni,
Utamaduni una tofauti,
Tofauti si ujinga,
Ujinga ni kukataa kufikiri.

Tofauti si ujinga hilo ninakubali.
Ila ujinga ni kukataa kufikiri.

Kwenye mada yangu nimeeleza kuwa sisi Watibeli, na jamii zenye mfumo kama wetu. Kulala ukweni sio tatizo. Sio mwiko.

Kuhusu mila na desturi. Zipo mila potofu za kijinga. Na mojawapo ni hiyo hapo.

Wewe kama mkeo analala kwenu, kwa nini wewe usilale kwao?
Majibu yake lazima yaangukie hapa, mila potofu, ubinafsi, kiburi, umaskini wa fikra au makazi, dharau n.k.
Hakuna jibu lolote la akili litatoka hapo.

Kuhusu mipaka, ni kweli kila mwanadamu na jamii zinamipaka.
Lakini ipo mipaka ya potofu. Mojawapo ni hiyo.

Hoja kubwa yenye mashiko,
Labda Kulala chumba kimoja na mkweo katika mazingira fulani ni kosa. Hii ipo sahihi. Lakini kuna mazingira unaweza ukalala na Mama mkwe chumba kimoja kwa kufuata maadili na isiwe kosa.

Katika sheria za Asili zenye Akili. Uungwana una muktadha.
 
Unalala ukweni, unapewa kiwanja .. unajenga mjengo wa maana ... baada ya muda waja omba ushauri
 
Tofauti si ujinga hilo ninakubali.
Ila ujinga ni kukataa kufikiri.

Kwenye mada yangu nimeeleza kuwa sisi Watibeli, na jamii zenye mfumo kama wetu. Kulala ukweni sio tatizo. Sio mwiko.

Kuhusu mila na desturi. Zipo mila potofu za kijinga. Na mojawapo ni hiyo hapo.

Wewe kama mkeo analala kwenu, kwa nini wewe usilale kwao?
Majibu yake lazima yaangukie hapa, mila potofu, ubinafsi, kiburi, umaskini wa fikra au makazi, dharau n.k.
Hakuna jibu lolote la akili litatoka hapo.

Kuhusu mipaka, ni kweli kila mwanadamu na jamii zinamipaka.
Lakini ipo mipaka ya potofu. Mojawapo ni hiyo.

Hoja kubwa yenye mashiko,
Labda Kulala chumba kimoja na mkweo katika mazingira fulani ni kosa. Hii ipo sahihi. Lakini kuna mazingira unaweza ukalala na Mama mkwe chumba kimoja kwa kufuata maadili na isiwe kosa.

Katika sheria za Asili zenye Akili. Uungwana una muktadha.
Ama kweli Mtibeli Uko mbali na wenyeji.
Inaonekana nyota njema, huenda ukafika walipo wenyeji.

Tofauti si ujinga,
Ujinga ni kukataa,
Kukataa bila kuchunguza,
Kuchunguza kabla hukumu,
Hukumu iwe na sababu,
Sababu isimame kwa hoja.

Hoja yako Mtibeli,
Mtibeli umeiweka wazi,
Wazi kwenu hakuna mwiko,
Mwiko wa kwenda ukweni,
Ukweni kwenu ni kawaida,
Kawaida yenu yaheshimika.

Lakini hapa kuna mipaka,
Mipaka ya hoja yako,
Hoja yako inapopanuka,
Inakuwa hukumu kwa wote,
Wote wanaoitofautisha,
Tofauti yao waitwa wajinga.

Hapo ndipo napinga,
Napinga si utamaduni,
Utamaduni wenu si tatizo,
Tatizo ni hitimisho,
Hitimisho lisilo lazima,
Lazima kwa ushahidi.

Unasema mke akienda,
Akienda kulala kwao,
Kwao mume naye aende,
Aende kulala kwao,
Lakini usawa si kufanana,
Kufanana si haki.

Mume ana nafasi yake,
Nafasi ina wajibu,
Wajibu una mipaka,
Mipaka ina mazingira,
Mazingira yana taratibu,
Taratibu huleta heshima.

Ndipo mila inapopimwa,
Kupimwa si kwa jina,
Jina la mila halitoshi,
Halitoshi kusema potofu,
Potofu lazima ionekane,
Ionekane kwa athari.

Mwiko ukilinda heshima,
Heshima inalindwa vipi?
Vipi ndani ya familia,
Familia yenye faragha,
Faragha yenye mipaka,
Mipaka yenye maana?

Na kama mazingira yabadilika,
Mabadiliko huleta tofauti,
Tofauti hubadili hukumu,
Hukumu isiwe ya kudumu,
Dumu pale sababu ipo,
Ipo sababu ya msingi.

Ndiyo maana nasema,
Uungwana una muktadha,
Muktadha una mazingira,
Mazingira yana mahitaji,
Mahitaji yana mipaka,
Mipaka nayo iheshimiwe.

Kwa hiyo Mtibeli sikatai,
Sikatai mfumo wenu,
Mfumo wenu una nafasi,
Nafasi yake ni kwenu,
Kwenu si kipimo cha wote,
Wote si lazima wafanane.
 
Somehow watibeli ni watu wa hovyo.

Imani zenu juu ya wanawake na dynamic za mimba +watoto zinasikitisha. Na hili la ukweni ndio kabisa.

Anyways mengine ni mazuri kama masuala ya haki.
 
Back
Top Bottom