Ukitaka kujua Watanzania wengi hawapendi kazi, zunguka maofisini muda wa lunch

WaTZ wengi na asilimia kubwa hawapendi kukosolewa, hawapendi kuambiwa ukweli...hawapendi kuelekezwa..hawapendi kufundishwa.. Pia hawapendi kuonyeshwa aibu na makosa yao!

Binaadamu yyte LAZIMA ahalalishe muda wa uwajibikaji (Laa sivyo kupokea kipato bila kazi halali ni Uharamia)
Turekebishe hizi tabia/ hulka!
 
Huwezi lazimisha mtu kufanya kazi kwa matakwa yako binafsi au Kuwa bull ukategemea efficiency kwenye kazi isipokuwa unategeneza kundi la wanafiki na kujipendekeza katik sehemu husika .

Kazi zote zinataratibu na sheria zake katika kila NCHI husika ndio maana viongozi wote kazi yao kubwa ni kuwa-inspire na kuimpliment strategy kwa wale anaowaongoza ili kupata matokeo bora ya kazi zao. Unapo sema zamani watu walikuwa wanafanya kazi sio kweli walikuwa wanafanya kazi kikuda na ndio hatari zaidi ukiona wanamefika stage hiyo.
Wewe ni mmoja wapo wa hao wavivu kupindukia, ndo mmejazana humo ofisini mnachati tu.
 
Ni kweli kabisa! nenda mashuleni hususani vyuoni, unakuta mwanafunzi jukumu lake la kusoma halitilii manaani kabisa, yaani hakuna kuchimba wala kutafuta ukweli wa changamoto zinazoikabili jamii, ndo hao wengi wao wako maofisini, ufanisi mdogo kazi kudai mishahara minene Basi.
 
We jamaa umesema muda wa lunch! ni kazi gani utafanya ukiwa na njaa!? hii sikuafiki kabisa.

Labda unamaana nyingine!
Mleta mada hajamaanisha kua watu wasiende lunch, amemaanisha muda wa lunch watu wanakua wanaufuatilia zaidi na kua nao serious kuliko muda wao wa kufanya kazi.

Hajasema kua watu wasiende lunch, ila kama na muda wa kazi wangekua nao wanauchukulia serious kama wanavyouchukulia serious muda wa lunch isingekua tatizo.

Binafsi naona hii issue ya uvivu na kutokuwajibika ni issue ya kimalezi toka utotoni, kubadili hii tabia inabidi wazazi waanze kuwafundisha watoto wao toka utotoni,ila kumbadili mtu mzima tabia sio issue ndogo.
 
Wanampimia mwajiri kiwango cha kazi kuendana na mshahara anaolipa, ndo maana huwezi kutoa jero ukapewa dumu zima la mafuta bali utapimiwa kibaba..
Mimi naona,mtu kama hujaridhika na malipo ya sehemu unayofanyia kazi, ni bora ukacheki issue zingine kuliko kupoteza muda wako au kuharibu kazi za watu coz mpaka unaanza hiyo kazi lazima utakua umesign contract au umekubaliana na muajiri wako,

Kufanya kazi kivivu hakuwezi kubadili chochote kisa unalipwa kidogo bali kinaweza kukusababishia hata hicho kidogo ukakikosa,

Mtu mvivu hata umlipe mshahara anaoutaka,atabadilika kwa muda tu ila ile hali yake ya uvivu na kutokuwajibika itarudi pale pale,uwajibikaji na kujituma ni tabia.

Piga kazi,timiza majukumu yako ipasavyo, Mungu atakuona tu na malipo yako utayapata tu,kama sio hapo ofisini kwako basi Mungu atakupa kazi bora zaidi hata sehemu nyingine, juhudi na kujituma hua haziendi bure,piga kazi huku ukimtegemea Mungu, hawezi kukutupa,jasho la mtu haliendi bure, jijengee tabia ya kujituma na uwajibikaji ni jambo zuri hata kama utaamua kufanya kazi zako binafsi.
 
Back
Top Bottom