Ukitaka kujua Watanzania wengi hawapendi kazi, zunguka maofisini muda wa lunch

Kayaula Musa

JF-Expert Member
Jan 2, 2020
530
1,000
Huwezi lazimisha mtu kufanya kazi kwa matakwa yako binafsi au Kuwa bull ukategemea efficiency kwenye kazi isipokuwa unategeneza kundi la wanafiki na kujipendekeza katik sehemu husika.

Kazi zote zinataratibu na sheria zake katika kila NCHI husika ndio maana viongozi wote kazi yao kubwa ni kuwa-inspire na kuimpliment strategy kwa wale anaowaongoza ili kupata matokeo bora ya kazi zao.

Unaposema zamani watu walikuwa wanafanya kazi sio kweli walikuwa wanafanya kazi kikuda na ndio hatari zaidi ukiona wanamefika stage hiyo.
Hili tatizo lipo huyu alieleta mada hii ninahakiki amefanya kautafiti kidogo anajua alichoandika ww kama unaleta ushabiki sawa hata huku mtaani kwenye vibarua vidogovidogo tunayaona watu wanataka hela sio kaz
 

Kayaula Musa

JF-Expert Member
Jan 2, 2020
530
1,000
Mimi naona,mtu kama hujaridhika na malipo ya sehemu unayofanyia kazi, ni bora ukacheki issue zingine kuliko kupoteza muda wako au kuharibu kazi za watu coz mpaka unaanza hiyo kazi lazima utakua umesign contract au umekubaliana na muajiri wako,

Kufanya kazi kivivu hakuwezi kubadili chochote kisa unalipwa kidogo bali kinaweza kukusababishia hata hicho kidogo ukakikosa,

Mtu mvivu hata umlipe mshahara anaoutaka,atabadilika kwa muda tu ila ile hali yake ya uvivu na kutokuwajibika itarudi pale pale,uwajibikaji na kujituma ni tabia.

Piga kazi,timiza majukumu yako ipasavyo, Mungu atakuona tu na malipo yako utayapata tu,kama sio hapo ofisini kwako basi Mungu atakupa kazi bora zaidi hata sehemu nyingine, juhudi na kujituma hua haziendi bure,piga kazi huku ukimtegemea Mungu, hawezi kukutupa,jasho la mtu haliendi bure, jijengee tabia ya kujituma na uwajibikaji ni jambo zuri hata kama utaamua kufanya kazi zako binafsi.
Wakianza kutoa malalamiko yaukosefu waajira utadhani watapiga kaz kwelikwel
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
1,869
2,000
Hili tatizo lipo huyu alieleta mada hii ninahakiki amefanya kautafiti kidogo anajua alichoandika ww kama unaleta ushabiki sawa hata huku mtaani kwenye vibarua vidogovidogo tunayaona watu wanataka hela sio kaz
Ndo Hali ilivo watu wanatanguliza pesa mbele wakati huduma mbovu....
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
1,869
2,000
Na wewe umesahau kipindi upo shule, ulikua unahaha ukiona muda wa kula unakaribia
ni kweli mkuu. .but kipindi hicho kumbuka tulikua tunaishi kwa Muongozo... Yan hata Kama hatupend kusoma lakini tunabanwa kutokana na Sheria za shule ...Ila huku makazini especially serikalini watu wanalindana Sana ... Mtu anaweza akatega hata week na bado mshahara uko pale pale ...tofaut kidogo na hz Taasisi au Kampuni binafsi
 

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
1,869
2,000
mkuu umeongea jambo la msingi sana, mfumo wetu wa malezi una kasoro, zipo tabia ambazo ni matokeo ya makuzi tuliyopitia tungali wadogo, Leo tunaziona familia za Wahindi hazitetereki kiuchumi kwasababu Wazazi wao huwashirikisha watoto katika kutafuta mali toka wangali wadogo, tunaona miji ya wenzetu ikiwa misafi hata majengo ya miaka mingi yanadumu ni kwasababu ya malezi na ustaarabu waliokuwa nao toka wakiwa wadogo.

kwa kweli yapo mambo ili tufanikiwe kama taifa lazima wazazi wawalee watoto katika misingi itakayowafanya kesho wawe watu bora. Sijisifii lakini najivunia Mama yangu alikataa kuajiriwa akachagua kuwa mjasiriamali ili awe na muda wa kutosha kutulea, aliwahi kuwa na Dada wa kazi lakini nakumbuka hatukudumu naye hata miezi 6 baada ya binti kushindwa kutekeleza majukumu yake. kumbukumbu zangu mara ya Mwisho familia yetu kuwa na Dada wa kazi ni mimi nilikuwa na miaka 3, tokea kipindi hicho kazi zote Mama na Baba walizifanya na kazi ndogo ndogo kama kusuuza vyombo kufuta vyombo, kufua nguo za ndani tulifundishwa tukiwa wadogo sana. Katika uzima sasa hivi ndo naelewa faida ya yale malezi.

leo wapo mabinti wakubwa tu hawawezi hata kupika chai sababu wana mfanyakazi nyumbani, tuna kizazi cha Wavivu, Wazembe ambao wanataka maisha mazuri na bora bila kufanya kazi. Hapa hata kutokomeza tabia mbaya ni changamoto. Kwa kweli tuanzie katika familia
Agreed ...Malezi yanamchango mkubwa Sana sana
 

chef detat

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
16,008
2,000
Mimi nikimkuta mtoa huduma mwanamke kwanza akili tayari inaanza kuchoka.. maana lazima utakutana na excuse au huduma ya kivivu, kama sio benki basi tegemea kuambiwa njoo kesho.

Yaani mtu yupo kwenye kutoa huduma akikuona mteja umekuja anaanza kukasirika maana alikuwa anachati
Kama mtu yupo ikulu na anaharibu imagine hizi ofisi za kawaida niaje, wale jamaa wa Ikulu kila siku wanakosea kuhusu teuzi na wakati wana mishahara mizuri nasikia na chai wanapiga nzito. Yani wanashindwa kuangalia tu kwa makini kazi kabla ya kuiweka public

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Xkalinga

JF-Expert Member
Sep 10, 2010
374
250
Bandiko halieleweki linazungumzia nini? Kumlaumu mfanyakazi kwenda lunch au kupumzika muda wa lunch ni kukosa nidhamu...Ungekuwa na hoja kama ungesema labda wakienda lunch wanachelewa kurudi hivyo kupunguza tija. Muda wa lunch umewekwa mahususi kwa kwenda kula au ambae haendi basi ni sehemu ya kupumzika.Huo muda sio wa kufanya kazi labda mtu apende tu kulifukia magepu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom