Ukitaka kujua Watanzania wengi hawapendi kazi, zunguka maofisini muda wa lunch

Dagger-v

JF-Expert Member
Mar 6, 2020
1,869
2,000
Habarini wakuu,

Kwa Tanzania hapa, asilimia kubwa ya watu wafanya kazi Ile basi tuu, wachache tuu wana uzalendo na kazi lakini wengi hawana moyo kabisa wa kufanya kazi.

Ukipita maofisini utagundua wafanyakazi wengi iwe private sector au serikalini wanazingatia muda wa lunch kuliko muda wowote wanapokuwa makazini.

Vitengo kama Customer Care & Service hawa utawakuta wanachati muda wa kazi na ikifika lunch hata kama haendi kula ni mwepesi kukujibu niko lunch.

Vitengo kama TRA, Uhamiaji benki, mitandao ya simu n.k wanapenda kusingizia kuwa system iko slow huku wakiendelea kuchat.

Lakini muda wa lunch hukuti mtu ofisini.

Anyway hawa ndo aina ya wafanyakazi tulionao katika kulijenga taifa.
 

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,874
2,000
Na ndo ktk group waliokua mitandaoni Wana mchukia na kumtukana sana JPM.

KWA Sasa wanatafuta hela kupitia Semina,per diem na kazi maalumu,huku wakichelewa makazini KWA visingizio lukuki na likizo za hovyo hasa dada zetu.

Nchi ishakua kama kambale kila mtu ana ndevu
 

Jameel2013

JF-Expert Member
Aug 21, 2014
694
1,000
Na ndo ktk group waliokua mitandaoni Wana mchukia na kumtukana sana JPM.

KWA Sasa wanatafuta hela kupitia Semina,per diem na kazi maalumu,huku wakichelewa makazini KWA visingizio lukuki na likizo za hovyo hasa dada zetu.

Nchi ishakua kama kambale kila mtu ana ndevu
Huwezi lazimisha mtu kufanya kazi kwa matakwa yako binafsi au Kuwa bull ukategemea efficiency kwenye kazi isipokuwa unategeneza kundi la wanafiki na kujipendekeza katik sehemu husika.

Kazi zote zinataratibu na sheria zake katika kila NCHI husika ndio maana viongozi wote kazi yao kubwa ni kuwa-inspire na kuimpliment strategy kwa wale anaowaongoza ili kupata matokeo bora ya kazi zao.

Unaposema zamani watu walikuwa wanafanya kazi sio kweli walikuwa wanafanya kazi kikuda na ndio hatari zaidi ukiona wanamefika stage hiyo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom