Ukitaka kujipima kama una upendo wa kweli na uvumilivu basi fuga mbuzi wa kienyeji

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
10,488
34,792
Kuwafuga hawa wanyama inahitaji uvumilivu wa Hali ya juu na upendo uliotukuka vinginevyo utakuwa unavunja mguu wa mbuzi kila sku.

Wana visirani na viburi sijawahi ona.

Picha linaanza akikata kamba aisee atakupigisha tizi moja sio ya nchi hii na ukimkamata ukaanza kumvuta na kamba yake anaamua kuzingua tuu yaani, anagoma kabisa na anaamua kukaa huku amenyanyua kichwa juu na amekuangalia Kwa kibri kana Kwanba huna la kumfanya.

Humo kwenye Banda usiku wanaweza amua kuanza kuzichapa Tu yaan , ni mnyukano na makelele usiku mzima. usishangae kuwakuta wote wamejifunga kamba kama wanataka kujinyonga.

Na kama kuna shamba Fulani wamezoea kuharibu aisee ukiwafungulia tuu asubuhi ni mwendo wa Usain bolt, mchungaji lazima utepete.

Kama Una miadi ya kuonana na demu usiingie kwenye Banda la mbuzi Kwanza maana ni full kunuka kibeberu.

Wachunga mbuzi wengi huwa dishi limeyumba kidogo maana ni mwendo wa kupigishwa jogging non stop, kama unaamini una huruma Sana na upendo basi fuga hawa wanyama, vinginevyo unatutania.




images - 2023-05-06T182934.665.jpeg





 
Beberu akiona kundi la mbuzi kilometa 3 hafikirii hata sekunde anaanza mbio ili aonje hata jike moja ambalo hajawahi kulipanda. Mbuzi wengine wanaanza kumfukuzia ila wakikutana na shamba la mtu wanaanza kufyeka mazao kwanza na safari inaendelea.
 
Daadek umenikumbusha shangazi yangu alikuwa na mbuzi enzi hizo Oya hawa jamaa wanakera mpaka basi tangu utoto mpaka ukubwani.

Akakukera unamfukuza ukirudi kukaa kanakuja kukuchungulia kuna siku nilikereka nilimpa jiwe moja mpaka akayumba tangu day hiyo kale kandama kakiniona mbio no utani.
 
Wafugaji mje huku mtupe visa vya visirani vya mbuzi wa kienyeji
Hawa mbuzi wanakera wakianza kulia mfano hakuna kumbuka hapo umewapa chakula na tumbo zipo kama pipa lakin hizo kelele mfano hakuna.

Basi enzi hizo tukiwa wadogo tukiona kelele zimezidi tunakoroga pilipili kichaa tuna wanywesha halafu mbio maana ni msala.

Wanabaki kusugua midomo kwenye ukuta na kelele kuzidi au mmoja anakamata kichwa mwingine anachapa makalio
Ila utoto Mungu atusamehe.
 
Hawa mbuzi wanakera wakianza kulia mfano hakuna kumbuka hapo umewapa chakula na tumbo zipo kama pipa lakin hizo kelele mfano hakuna
Basi enzi hizo tukiwa wadogo tukiona kelele zimezidi tunakoroga pilipili kichaa tuna wanywesha alafu mbio maana ni msala
wanabaki kusugua midomo kwenye ukuta na kelele kuzidi
Au mmoja anakamata kichwa mwingine anachapa makalio
Ila utoto mungu atusamehe
Na ujasiri mlikuwa nao 😂
Mie hata kuua mjusi nilikuwa siwezi
Sahivi nikipiga mdudu akafa nampa na pole
 
Back
Top Bottom