Maisha ya Mwanadamu: Ukitaka kupima kiwango cha juu cha uvumilivu wa mtu yeyote, basi mpokonye kile anachokipenda sana

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Je, ni kweli kwamba, ukitaka kupima kiwango cha juu cha uvumilivu wa mtu yeyote, basi mpokonye kile anachokipenda zaidi?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Ndugu zangu wa Tanzania;

SITOSAHAU SIKU AMBAYO NILIKUTA PANYA AMETAFUNA SURUALI YANGU YA THAMANI.
================
Mwezi November ya Mwaka wa 2016, niliwahi kupokea zawadi nzuri sana ya suruali aina ya kadet kutokwa kwa kaka wa mama yangu (mjomba) aliyekuwa ameenda nchini South Afrika kwa mkutano wa kama week moja tu wa masuala yao ya huko kazini. Kama kuna vitu ambavyo nilikuwa ninavithamini sana katika maisha yangu kwa wakati ule basi ni hiyo suruali yangu nyeusi na maridadi

Sasa bwana kuna siku moja nilipata mualiko kwa njia ya simu kwenda kuhudhuria usaili wa kazi katika kiwanda kimoja hivi cha wahindi kilichopo Dar eneo la viwanda kule Nyerere Road. Simu nilipigiwa siku ya Ijumaa kwamba ikifika Jumatatu asubuhi basi niwe nimefika na kuonana na Mr **** ndiye HR Manager kwa wakati ule. Basi sawa mimi nikakubali na kisha kuanza kufanya maandalizi ya kwenda katika shughuli ile

Nilifua nguo mashati yangu vizuri na kupiga pasi, sasa ilivyofika muda wa kwenda kabatini kuchukua suruali yangu ile ya mtoko ebwana eeeh....!!! Mbona nilibaki mdomo wazi. Panya hata walipotokea. Nitakuta ngoma imeliwa maeneo ya magotini miguu yote miwili na sehemu ya nyuma katika makalio. Hakika roho yangu ilisononeka sana kwa ukatili wa panya wale.

Ilinibidi nivae suruali yangu nyingine ambao sikuwa ninaipenda sana kama ile Kadet aliyonitunuku mjomba ndio hapo nikasema hakika; Ukitaka kupima kiwango cha juu cha uvumilivu wa mtu yeyote, basi mpokonye kile kitu ambacho anakipenda sana.

Mwana JF mwenzangu, ni kitu gani uliwahi kupoteza kikapima kiwango chako cha juu cha uvumilivu?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Panya aliwahi kula gauni la mama yangu wakati bado nipo mdogo na tunakaa kule Kurasini shimo la udongo.

Mama alikasirika sana mpaka huruma ikanijaa.
Pole sana kwa mama yetu.

Je, kwa upande wako, ni kitu gani uliwahi kupoteza katika maisha kikapima kiwango chako cha juu cha uvumilivu?
 
Nakumbuka kipindi cha likizo, shangazi yangu alikuja na mtoto wake hom kututembelea, huyo mtoto wake alikuja na umri was Kama 6-8 hivi.

Sasa basi siku yao ya kuondoka ilipofika mie sikuwepo, tulikua tumeweka kambi shambani na mshua.

Nimerudi nyumbani nikaenda kuoga, naingia geto nivae tishet langu lenye picha ya Nelly mwenye plasta usoni(Nelly wa dillema) silioni, nikatafuta Kila Kona silioni, natoka nje kumuuliza bi mkubwa, akanijibu easy tu, eti mdogo wako amelilia nikaona nimpe.

Yaani hakuna siku niliumia moyo Kama siku ile, nilinyong'onyea mpaka akanionea huruma.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Sio kila muda tunapaswa kusoma na kujadili makala zinazohusiana na masuala ya cold war, jeshi na ujasusi wa KGB, CIA na Mossad. Ngoja leo tujadili kidogo changamoto za maisha katika jamii tunamoishi.

Ndugu zangu wa Tanzania;

SITOSAHAU SIKU AMBAYO NILIKUTA PANYA AMETAFUNA SURUALI YANGU YA THAMANI.
================
Mwezi November ya Mwaka wa 2016, niliwahi kupokea zawadi nzuri sana ya suruali aina ya kadet kutokwa kwa kaka wa mama yangu (mjomba) aliyekuwa ameenda nchini South Afrika kwa mkutano wa kama week moja tu wa masuala yao ya huko kazini. Kama kuna vitu ambavyo nilikuwa ninavithamini sana katika maisha yangu kwa wakati ule basi ni hiyo suruali yangu nyeusi na maridadi

Sasa bwana kuna siku moja nilipata mualiko kwa njia ya simu kwenda kuhudhuria usaili wa kazi katika kiwanda kimoja hivi cha wahindi kilichopo Dar eneo la viwanda kule Nyerere Road. Simu nilipigiwa siku ya Ijumaa kwamba ikifika Jumatatu asubuhi basi niwe nimefika na kuonana na Mr **** ndiye HR Manager kwa wakati ule. Basi sawa mimi nikakubali na kisha kuanza kufanya maandalizi ya kwenda katika shughuli ile

Nilifua nguo mashati yangu vizuri na kupiga pasi, sasa ilivyofika muda wa kwenda kabatini kuchukua suruali yangu ile ya mtoko ebwana eeeh....!!! Mbona nilibaki mdomo wazi. Panya hata walipotokea. Nitakuta ngoma imeliwa maeneo ya magotini miguu yote miwili na sehemu ya nyuma katika makalio. Hakika roho yangu ilisononeka sana kwa ukatili wa panya wale.

Ilinibidi nivae suruali yangu nyingine ambao sikuwa ninaipenda sana kama ile Kadet aliyonitunuku mjomba ndio hapo nikasema hakika; Ukitaka kupima kiwango cha juu cha uvumilivu wa mtu yeyote, basi mpokonye kile kitu ambacho anakipenda sana.

Mwana JF mwenzangu, ni kitu gani uliwahi kupoteza kikapima kiwango chako cha juu cha uvumilivu?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

BIASHARA: Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher
Uzi wa moto sana huu kijana wangu Infantry Soldier ngoja wajumbe waje kutoa shuhuda zao.
 
Usiseme sana kwa sauti ,wasije kusikia Watu wa Sumbawanga na Mbeya .
Kwao hilo tukio la panya kula nguo unayoipenda na panya ni Ushirikina.

Hamjanielewa ni kwamba Huyo panya aliona wivu (Panya = Mtu mchawi)
 
Hatuwez ku reflect kweny siasa mkuu?maana tulitaman sana tumuone TAL live kwa tv, ila ndo ivo haoneshw kwa hyo uvumilivu umetushinda tumeamua kufanya mbadala wa kweny cm, na hapa nmemnunulia bi mkubwa kakimeo ili apate taarifa za kina Lisu maana n mdau wake mkubwa
 
Back
Top Bottom