miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,805
- 49,104
sitasalimika mkuu basi ngoja nisamehe ila kusahahu sijuiHahA umeitika vizuri kweli!! Jiulize wewe hujawahi kumfanyia mtu mabaya au hufanyi mabaya? Je nao wakiamua kujibu mapigo utasalimika?
sitasalimika mkuu basi ngoja nisamehe ila kusahahu sijuiHahA umeitika vizuri kweli!! Jiulize wewe hujawahi kumfanyia mtu mabaya au hufanyi mabaya? Je nao wakiamua kujibu mapigo utasalimika?
Naona mshana jr umekuja kuwapa watu ticket ya kulipiza visasi.Mmmh! Wacha niandae kisasi nimeshindwa kusamehe!!

miss chagga ulipigwa mimba ukiwa shule nini???mkuu kuna mambo ukiangalia impact iliyokuletea maishani na unaishi ndani ya hiyo hali aisee unashindwa kusahau kabisa .. a
Jitahidi mshiki oko Ruwa akutaramesitasalimika mkuu basi ngoja nisamehe ila kusahahu sijui
haika mbeJitahidi mshiki oko Ruwa akutarame
ha hahaha mkuu wewe .. navyo penda watoto sidhani kama ingekuwa tatizo kwangu aisee.... mambo tu yalitokea tokeamiss chagga ulipigwa mimba ukiwa shule nini???
All in all samehe ili milango ya baraka/opportunity ifunguke.
Pole mkuu.
Mkuu ukifika uendako, wakati wa kurudi pitia hapa ukae kitako utoe japo neno

Thanks kwa andiko lako.Nimesoma kwa makini andiko hili na nimetoka na jumuisho hili,Kwa kawaida kulipa kisasi ni rahisi kuliko kusamehe, hivyo mwanadamu wa kawaida atapenda kulipa kisasi kuliko kusamehe, lakini je kwa wale wanaonamini katika MUNGU -JEHOVA ndivyo inavyotakiwa kuwa? ulipe kisasi?
Kwa mtu anayetamani kuiona mbingu siku moja andiko hili linahitaji fikra ya ziada kwani tiyari Mungu amesema usiripe kisasi, na kisasi ni mali yake wala siyo ya mwanadamu. Waebrania 21.14 Mungu anawagiza mtu aishi na watu wote kwa amani, tunajua amani inakuja kwa msamaha na wala si kwa kisasi, ni rahisi mtu kujifunza ndani ya msamaha lakini kisasi kinaleta kisasi kingine uzao hadi uzao, kabila hadi kabila na taifa hadi taifa.
Mapigano tuliyo nayo leo na hayaishi ni kwa sababu watu wamejaribu kulipa kisasi, wameshindwa na mwisho wake wanarudi tena kwenye msamaha. Toka nimekuwa na akili, hakuna mgogoro ulioanza kwa kisasi ukaisha, ila nimeona migogoro imeanza kwa kisasi na ikaisha kwa msamaha, na hii ndiyo kanuni aliyoiumba Mungu kwamba wema utaushinda uovu. Hivyo kabla hujawaza kullipa kisasi kumbuka ipo siku mtakaa kwenye meza kupatana ili mmalize.
Kwa mkristo yeyote, kipimo chako cha msamaha kwa wengine ndiyo, msamaha wako kwa Mungu hivo usitegeme kusamehewa kama hukusamehe Marko 11:25,26. Na watu wajue, Mungu alitusamehe ili yeye awe na amani nasi, hivyo tunasamehe for our own sake, for our own well being, Msamaha kwa wengine ni upuzii lakini kwa mkristo ni afya ya moyo na uzima wa mifupa yetu, usije jaribu kumsamehe mtu ukafikiri ataona umefanya jambo la maana sana na anaweza kukudhihaki kuwa umemuogopa, lakini wewe jua unatengeneza nafsi yako na MUNGU wako.
Nashauri Mkrisro kusamehe ni lazima na sio ombi kama unatamani kuingia mbingu mpya siku moja. Ukikuta unashindwa kusamehe, jua kipawa cha roho mtakatifu kipo mbali nawe, kikija karibu utasamehe moyoni hata kabla mdomo hajasema kitu. Kumbuka kazi ya roho mtakatifu ni kutupatanisha sisi kwa sisi, pia wewe na mwili wako, lakini pia wewe na MUNGU wako, wala haesabu maovu.
Waza Mungu ange kuhesabia makosa yako ungekuwepo?, na kama watu wake MUNGU wakilipa kisasi je washetani watafanyaje? na tofauti kati ya hizi falme mbili itaonekanaje?
Kaniwekea sumu imeathiri kizazi siwezi kuzaa tena na sina mtoto naanzaje kumsamehe?
Mkuu huyo mtu alikufanyani?Mimi nimeapa kulipiza kisasi.... na kwa hili Mungu anisamehe maana hakuna namna nyinginine
Jina la Mungu lihimidiweThanks kwa andiko lako.
Mh!!!....kweli kuna mitihani!!!....pole mkuu....lazima kuna solution, jipe Moyo.Kaniwekea sumu imeathiri kizazi siwezi kuzaa tena na sina mtoto naanzaje kumsamehe?
Ndio maana sitaki kufanya kazi isiyokua yangu .Kazi ya kulipa kisasi ni ya MUNGU na mie sio.Kweli Kisasi ni Mali ya MUNGU
ndiyoo! Sa kama mtu anafanya kusudi ili kukupa maumivu,ukimsamehe atajiona ye wa fahari loh!Naona mshana jr umekuja kuwapa watu ticket ya kulipiza visasi.
content UKISHINDWA KUSAMEHE LIPIZA KISASI!
Mimi simo![]()
![]()
![]()
![]()
Kwa knowledge yangu ndogo ya psychology we unatatizo na MTU umejaribu kusamehe umeshindwa au hutaki!! Na the only option you see is revenge!! Na unataka support ya hilo!! I'm out!! Bible inasema kisasi hakimalizi ugomvi au tatizo ila huleta machafuko zaidi hata mauti zaidi!! Kama unaona kisasi kitakusaidia Fanya ila jiandaae na lolote litalotokea as a consequences!! Maana msamaha huwa ni full stop!! Wewe unatafuta "DOs" au Go On"hii ya leo ni tofauti kidogo na mada zetu zile , hii inahusika na kulipa kisasi![]()
Katika maisha bila kujali unaamini nini hakuna jambo jema kama kusamehe!msamaha hukusaidia mengi mpaka kifo na maisha yanayofuata baada ya kifo iwe reincarnation au rebirth nk !msamaha hukufanya uwe mwema mwenye furaha ya kweli usiye na makunyanzi rohoni na usoni
Mwenye msamaha ana nuru usoni , msamaha ni tiba, msamaha ni mafanikio msamaha ni amani na ni upendo
Lakini je kama huamini katika msamaha? Kama unayemsamehe hasameheki? Na je kama ni mbabe mjuaji na dhulumati mkubwa?je kama anakuletea dharau kwa hali yoyote ile hata uwe msamehevu kiasi gani? Usiishi na maumivu! lipa au lipiza..!
Msamaha wako usikushushe msamaha wako usikufanye kiumbe dhaifu na mnyonge, utu wako ni muhimu heshima na dhima yako ni vitu vya kulinda na kuzingatia mno...ukishindwa kabisa kusamehe ukizidiwa na viwango vya uvumilivu wa kibinadamu usiumize roho yako andaa kisasi
Kama ilivyo kwa msamaha ile nafuu unayoipata kwenye kusamehe basi ndivyo ilivyo hata kwenye kisasi! Kisasi humpa mtu faraja na amani ya moyo huridhika kuona amefanya jambo baya kwa mtu mbaya
Tunaishi na wajuaji wengi kwenye jamii tunaishi na watu wanaojiona wao ni bora kuliko wengine wao ni zaidi kuliko wewe...wao ndio wanaijua pesa kuliko wewe. . . . usimpe nafasi mtu wa namna hii atambe...ni lazima umfundishe ajue kuwa maisha yana pande nyingi...kisha mfundishe kwa maumivu makubwa maumivu atakayodumu nayo mpaka kifo
LAKINI maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua...Fanya kile kitakachokupa nafuu ya rohoni na afya ya akilini kwakuwa uamuzi ni wako na mwisho utabaki wewe kama wewe ....visasi misamaha na malipizi vitabaki kuwa uamuzi binafsi kutokana na imani yako hofu yako na huruma yako
Nimeamua kuishi hivyo na maumivu sina jinsi jambo limetokea zaidi ya miaka 16 lkn maumivu yake utafikiri ni jana.Siwezi kwenda kinyume na imani yangu na nimejitahidi kusamehe nimeshindwa kabisa.