Ukishindwa kusamehe lipa kisasi

Ukishindwa kusamehe lipa kisasi

Mkuu Mshana Jr.Inasemekana kila kitu kinacho tutokea ni function ya karma.
Kwamba, ukipata ajali ni karma,ukipata maradhi fulani ni karma,mtu akikuumiza, hiyo ni sababu ya karma.
Sasa ukilipiza kisasi, huoni kama unaendelea ku accumulate karma?.
 
Ni kweli katika waaminio karma kwahiyo uchaguzi unabaki kuwa kwa mtendwa
 
Na vp mshana jr kwa wale wanaombea wenzao kwa Mungu mabaya pale mnapokuwa mmetofautiana
Mtu anafunga kabisa na Kumuomba Mungu ampe pigo mbaya wake. Maombi ya aina hii si yanaangukia kwenye kulipiza kisasi?
 
Mungu huwa habariki maovu ni sawa na wale wanaomuomba Mungu awasaidie washinde vita.. Mungu hubaki kuwa Mungu na ana jinsi yake ya kutoa adhabu
 
Nimeamua kuishi hivyo na maumivu sina jinsi jambo limetokea zaidi ya miaka 16 lkn maumivu yake utafikiri ni jana.Siwezi kwenda kinyume na imani yangu na nimejitahidi kusamehe nimeshindwa kabisa.
mama kubwa kuna kitu unaweza kufanya hapa na ikawa hatua moja kuelekea kusamehe.

Jambo lenyewe ni kuhadithia.
Ila kama unaogopa kuhadithia hapa unaweza tafuta mtu ukamhadithia na ukipatwa na uchungu lia ni tiba nzuri kuelekea msamaha.
 
Nimekupata mkuu, tatizo langu lipo hapo kwenye kusema unasahau. Hauwezi kusahau tukio hata siku moja, msamaha wa kweli ni ule ambao hata ukikumbuka tukio lililotokea halikupi shida au maumivu kama miss chagga

Mambo mengi yanayotusumbua yapo kichwani tu au kwenye mawazo hayana uhalisia, wakati mwingine unaweza tu ukabadili unavyoyachukulia mambo na kila kitu kikabadilika.
Upo sahihi?Kichwa cha binadamu kilivyoumbwa umbwa hutunza kumbukumbu nyingi sana...Tutasahau vitu vidogo vidogo ila navyo pia ukikaa ukatulia au ukaona kinachofanana nacho basi utakumbuka,huwezi sahau kamwe jambo baya ululilofanyiwa hata kama utaielewa na kuishi ndani ya dini kiasi gani.Hiyo ni human nature,navyojua kwa akili yangu ni unasamehe na usikumbuke kutenda ubaya juu ya kile ulichofanyiwa..maana yake ni kwamba yule aliyekutendea ubaya utaendelea naye na maisha ya kawaida pasipo kumtendea tofauti na msamaha uliopo.Kuachana na mawazo hasi juu ya ubaya uliotendewa,kama ni kosa wewe msamaha wako uoneshe njia sahihi na ndipo nguvu ya msamaha huja.Mtu anayesamehe mambo bila manung'uniko ndio huwa njia bora kwa mkosaji.
 
Mungu huwa habariki maovu ni sawa na wale wanaomuomba Mungu awasaidie washinde vita.. Mungu hubaki kuwa Mungu na ana jinsi yake ya kutoa adhabu
Kama habariki maovu mbona anatuambia kisasi ni juu yake?
 
Back
Top Bottom