Ukimya ni usaliti

Ukimya ni usaliti

Hayo Maduka na miundombinu inaweza kurudishwa na kutengenezwa!! Fikiria maisha ya maelfu ya watu waliouliwa kinyama na polisi uhai wao mtaurudisha?
Wezi wengi tu waliuawa na raia wenye hasira Kali,hao wahalifu kuuawa hakuna shida,nilijichanga kidogo dogo miaka nikaanzisha biashara,mmeichoma moto,nilikopa nadaiwa,nani atalipa,nani atalisha familia yangu,nani atanipa mtaji?
 
Hao wote ni wakuweka pamoja kwenye kapu la wanafiki.Hawastahili kupewa heshima wala kusikikilizwa na Mtanzania yoyote mwenye akili timamu.
 
Hofu imewajaa hakika hizi ni nyakati mbaya sana kwenye taifa letu.
Hofu kwa wauaji ni mbaya sana na inaua kuliko hizo risasi. Angalia hii scenario. Hii ni tukio baya sana tena la kudhamiria na linahitaji hatua zisizo za kawaida. Je, wakitoka maaskofu wote wa Tanzania nzima, wakiongozwa kardinali, wakafanya mkutano, na kulaani yote yaliyotokea, hawa wahuni watathubutu kuwaua wote? Hivyo hivyo kwa viongozi na majaji wote wastaafu na asasi zote.
 
Kilichotokea kinahitaji uthibitisho gani?
Uharibifu wa mali za watu na miundombinu ulifanywa na vijana wavuta bangi hauonekani??
Alaaniwe roma na mange kijambio kwa kuhamasisha hiki kilichotokea
Mali gani wewe chizi? hizo mali ni za watanganyika na wana haki ya kuzifanya chochote wakitakacho.

Unampangia mtu vile aifanye mali yake? Hata akiichoma moto ni sawa tu.
 
Labda ni mimi tu. Labda mimi ndo tatizo. Labda nina uwezo mdogo wa kuelewa mambo.

Labda ni hivi au labda ni vile.

Labda nategemea mambo flani flani toka kwa watu ambao sipaswi kutegemea chochote au lolote toka kwao.

Kuna ukimya wa ajabu sana kutoka kwa baadhi ya watu na taasisi ambazo mtu ungedhani ziko mstari wa mbele katika kutetea haki za kibinadamu.

Kwa uwazi tu, sitegemei chochote toka kwa muuaji na kiongozi haramu.

Ataanzia wapi kukemea kilichotokea na kutoa pole kwa wahanga?

Lakini wengine nao je?

Wako wapi wale viongozi wa dini ambao huwa wanakemea utekaji?

Wako wapi wale viongozi wa zamani ambao wamestaafu kukemea kilichotokea?

Watu wamejikausha tu kama vile hakuna chochote kilichotokea!

Kuna mambo mtu mwenye akili timamu hupaswi kuyakalia kimya.

Zaidi ya wiki sasa na watu hawasemi chochote.

Ukimya mbele ya ukiukwaji wa makusudi wa haki za kibinadamu ni usaliti.

Waendelee kupumzika kwa amani wazalendo wote waliopoteza maisha yao na wale walioumizwa.

Kwa nyie wasaliti, kama mnadhani kila kitu ni upepo tu na lililotokea nalo litapita tu kama upepo, subirini muone.
..usipoteze muda kuhoji kwa nini fulani hasemi, tafuta jibu la yale usiyopenda kutokea na yametokea, mfano viongozi wa dini, si mara moja wala mbili wametoa tahadhari ya hatari kutokea haya yaliyotokea, hawakusikilizwa..bado unarudi kutaka waseme chochote, kitasaidia nini km maangalizo walitoa na hayakufatwa! wewe tafuta majibu, acha kulalama..!
 
Hofu kwa wauaji ni mbaya sana na inaua kuliko hizo risasi. Angalia hii scenario. Hii ni tukio baya sana tena la kudhamiria na linahitaji hatua zisizo za kawaida. Je, wakitoka maaskofu wote wa Tanzania nzima, wakiongozwa kardinali, wakafanya mkutano, na kulaani yote yaliyotokea, hawa wahuni watathubutu kuwaua wote? Hivyo hivyo kwa viongozi na majaji wote wastaafu na asasi zote.
Yaani tuna watu wa ajabu sana nchi hii.
 
Leo nimeona Antony Mtaka akilia na waombolezaji. Seems hizi amri zilikuwa beyond wakuu wa mikoa. Hata majambazi tunaaswa wananchi tusijichukulie sheria mkononi, why why why kuua watoto wetu! Why mpaka sasa hakuna anayewajibika? Walikufa wafungwa magereza kizembe mzee Mwinyi aliwajibika! Why huu ukimya????
Inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom