Ukimuomba pesa rafiki yako anakusaidia kwa haraka, lakini kila akikuomba kwako huna kitu.

BAKIIF Islamic

JF-Expert Member
Jul 11, 2021
594
1,827
Na mwingine anasaidia sana rafiki zake na jamaa zake wanapopata anguko la uchumi, lakini likija upande wake hawamsaidii, akikwama anakwama kwelikweli.

Katika uislamu tumefundishwa kwamba mkopeshaji ''mwenye kukopesha'' anathawabu nyingi kulikoni mwenye kutoa sadaka. Yaani wewe kama 'Umemkopesha mtu' elewa una malipo makubwa mbele ya MUNGU kulikoni yule mwenye kutoa sadaka, hii ni kwasababu:

Mkopaji ili akope ni lazima atoe aibu zake, ni lazima akueleze aibu zake alizo nazo, ni lazima akueleze shida yake aliyo nayo hadi kuja kwako umpe mkopo, na wewe ukaguswa na yale mambo, sasa ukatoa pesa kumsaidia kutatua zile aibu zake, basi elewe wewe una malipo makubwa mbele ya MUNGU kuliko yule mwenye kutoa sadaka, kwasababu sadaka unaweza kumpa mtu yeyote hata mwenye nacho.

Kanuni ni kwamba,


Siku rafiki yako akikulilia shida na wewe ukawa huwa uwezo huo, basi jitahidi sana lile jambo lake mlibebe wote kwa pamoja, mwambie kiasi hicho kwakweli sina kwasasa lakini nakuahidi kukitafuta pahala hata kwa kukopa ili nikupatie, na baada ya hapo anza kuhangaika kumtafutia msaada kwa sehemu zingine unazo zifahamu na ukiupata basi mpatie. 'Hakika atakushukuru na huyo hatokuacha siku ukikwama na urafiki wenu utadumu.

Inaumiza sana, rafiki ambaye alikua anakusaidia sana wakati wa shida zako, halafu siku anakwama anakuomba msaada na wewe ilihali huna kitu wakati huo.

Sasa ili kujitoa katika hayo maumivu baina yenu, livalie njugu swala lake na umtafutie ufumbuzi katika hilo, ukiacha kufanya hivyo basi elewa rafiki yako atakuchukulia kama mbwa, thamani yako kwake itapungua.

Siku ukimwambia rafiki yako huna na wakapotea, usiwarudie tena hao watu, fukuza ni kama mbwa mpotevu ataning'inia ilimradi unamlisha lakini ukiacha kumlisha atahama kwa nyumba inayofuata ambayo itafanya kama ulivyokua unafanya.

''Mara nyingi watu wa namna hii hawana tofauti na mkopaji wa bidhaa duka namba 1, lakini akipata Cash anakwenda kununua duka namba 2. Anasahu kwamba duka namba 1 ndio huwa anamjali akiwa na dhiki. Ila akipata Cash anakwenda duka namba 2 kwasababu anamkwepa wa duka namba 1 kwakua anamdai.

1690457803954.png
 
Yan kama mimi sinanaga bahati kabisa mtu nimkopeshe hela alafu akaludisha au nikawa na shida nikapata msaada kwa watu hao sasa ninacho fanya mtu akija na shida yake labda elfu 50 kama ninayo elfu20 nampa for free simkopeshi namwambia hiyo sitaki unilipe ww tafuta kwingine uongezee hapo huo ndo unakuwa msaada wangu tofauti na hapo sifanyi ujinga kama sina na mwambia kwa sasa sina inakuwa imeisha hivyo
 
Wema humaanisha kumfanyia mtu mambo mazuri na kumfanya mwingine aweze kufurahi. Je! Tunaweza kuwafanyia wema ndugu zetu, marafiki zetu na watu wengine bila kutaraji malipo kwao?
Mkuu unapomsaidia mtu awaye yeyote, namaanisha awe ndugu au rafiki just do it for free na usitegemee chochote,, kwasababu sio kila mtu ataona umuhimu wa msaada wako hapo ndipo utakapozalisha maumivu
 
Yan kama mimi sinanaga bahati kabisa mtu nimkopeshe hela alafu akaludisha au nikawa na shida nikapata msaada kwa watu hao sasa ninacho fanya mtu akija na shida yake labda elfu 50 kama ninayo elfu20 nampa for free simkopeshi namwambia hiyo sitaki unilipe ww tafuta kwingine uongezee hapo huo ndo unakuwa msaada wangu tofauti na hapo sifanyi ujinga kama sina na mwambia kwa sasa sina inakuwa imeisha hivyo
Pole sana, basi MUNGU na akubariki mikono yako ikamate Bilioni 10 katika miaka hii mitano ijayo.
 
Back
Top Bottom