Usilalamike huna ndugu, huna kitu...

Jun 10, 2023
54
76
USILALAMIKE HUNA NDUGU,HUNA KITU

Habari wana jamvi,

Natumai wote ni wazima wa afya.

Leo nimeona nitoke kule kwenye uzi wa ujenzi nije huku kutazama tazama yanayojiri nikaona naweza kuandika japo kwa kifupi mawazo yangu kuhusu baadhi ya mambo likiwemo hili la udugu na urafiki.

Kutakuwa na makosa mengi ya kiuandishi kwasababu mimi sio muandishi mzuri basi mnivumilie lakini hoja na mawazo yangu yote yataeleweka vizuri kabisa teenzetu.

Kunafunzo kubwa nataka kuwapa watu wangu wa nguvu,usihuzunike na kulalamika sana ukiwa katika kipindi kigumu hasa cha kifedha,huna kazi,kila ukiomba kazi unakosa,kila ukikosa unachekwa kila when you ask some help from ndugu zako ambao unaamini wanaweza kukusaidia wanakutupa,washkaji ambao unahisi wanaweza kukusaidia wanakutupa,demu wako kila akikupiga mzinga huna nae anakutupa,unamtumia jumbe nyingi hajibu,simu zako hashiki.

Kwa wale mliokuwa na wake basi angalieni ile respect unayopewa ukiwa na pesa na pale usipokuwa na pesa,kama ulioa kwa kufata matako basi sina cha kukushauri
Anyway ni hivii nyakati ngumu maranyingi hutuonesha mambo kadhaa,

1- Mapungufu yetu au madhaifu yetu
Maranyingi tukiwa na nyakati nzuri huwa hatuoni mapungufu yetu,tunahisigi kuwa tuko vizuri ndiomaana tunanyakati nzuri,kumbe …tunafanya makosa mengi sana ambayo hatuyaoni kwasababu ya usindi weru mpaka pale tutakapopoteza ndio tunaona kuwa kunasehemu tunakoseaga,hivyo ukiona umekosa usilalamike ni moja ya njia Mungu wako anatumia kukuonesha makosa yako na madhaifu yako ili upambane ujirekebishe na ukirudi utakuwa bora zaidi ya mwanzo na kama kupata utapata mara mbili ya ukivyokuwa unapata mwanzo,hivyo ukikosa angalia wapi unakosea badala ya kulalamika kwa kukosa.

2-Nguzo zetu
Tukikosa pia huwa tunaoneahwa nguzo zetu muhimu za kuegemea. Utamuona ni nani anaekupamoyo na kukufariji,ni nani atakaekusaidia kiasi kidogo cha pesa alichonacho?maana kiukweli wengi wetu vipato vyetu huwa havitutoshi hata robo sisi wenyewe kwahiyo tunavyotoa kukupa wewe na mashida yako usidhani kuwa tunatoa kwasababu tunacho kikubwa ila tunatoa kwasababu tunaguswa na majanga yako.

Pia tunatoa kwasababu msaada ni uwekezaji kwamba siku na sisi tutakwama hivyo tutahitaji msaada kwahiyo tunaweka mitego ya kunasa kitoweo siku na sisi tusipokuwa na kitoweo. Kwahiyo tukikupa na wewe usiwe mgumu kutoa siku tukiomba tena haswa yule anaekupa then yeye mara nyingi hajawahi kukuomba hakikisha siku akikuomba usimwambie huna,hakikisha unampa hata kama huna,nenda kakope hata kwa riba kubwa tena haswa yule ambae unamuombaga na Kipato chake unajua ni kidogo,hakikisha unakopa popote umpatie tena hata na zaidi basi utatengeneza kitu kikubwa sana moyoni mwake,atafarijika sana na ataona kuwa msaada wake hajawahi kuutupa. Kumbuka kutoa ni moyo na sio utajiri. Atakeoonesha moyo wa kukupa hakikisha na wewe unaonesha moyo wa kumpa.

3-Wanafiki
Tukikosa pia huwa tunaoneshwa wanafki na Mungu,kunawanao kabisaa wanaoo,wale wanao kabisaa watakukataa unaona kabisa mtu anauwezo wa kukusaidia lakini nae atakueleza majanga yake weee mwisho kabisa sina.

Ndugu sasaa yule umezalwa tumbo nae moja,huyu mmekutana kwa shangazi huyu mmekutana kwa mjomba lakini unaamini ni ndugu zako na wanauwezo wa kukupush lakini hawafanyi hivyo. Jirani unaeishi nae vizuri kabisa ambae unaamini anaweza kukusaidia kabisa hata elfu 2 ya unga na dagaa ule na wanao japo mara moja tuu kwa siku atakwambia hana wakati yeye anakula kuku kwa mrija. Usihuzunike hutokufa kwa njaa.

Mungu aliekuumba ndio atajua utakula nini lakini kikubwa itakuwa ushamuona ni nani na nani rafiki na ndugu na nani mnafki,na wewe tumia akili sasa usiwe kama fala ukimuomba mtu unaeamini hawezi kukosa unachomuomba na akakwambia hana basi tulia siku nyengine muombe tena akisema hana tena basi usijaribu kumuomba tena kamweee usijaribu,usije ukatukanwa ukaumia zaidi au akakujibu vibaya ukafadhaika zaidi

Kama unae mmoja ambae anabeba shida zako kama zake kulanae sahani moja huyohuyo kamwe hatokuchoka na akikuchoka basi nae ni mnafki pia, lakini maranyingi Mungu huwa anatupa watu wa namna hii,hata uwe chizi fala mwehu lazima kunakuwaga kuna mtu atakaekuwa upande wako,basi simama nae huyohuyo achana na sisi,tutakuumiza moyo wako wakati unahitaji faraja kwetu.

Na yule unaemtegemea siku akikwambia sina jaribu kumuelewa sio kakusaidia mara 10 kakwambia hana siku moja unaanza kinyongo oohh jamaa kanikataa utakuwa fala mwehu wewee, muda mwengine tunawakataa ili na nyinyi mjitahidi kuangalia njia nyengine au mumkumbuke zaidi na zaidi Mungu.

4- Kukosa pia ni njia ya kukumbuka kuwa kuna Mungu
Wakati mwengine tunakosa sio kama tunakosea au tuna madhaifu au tunataka kuoneshwa wanafki na marafki bora,ndugu na uliezaliwa nae ukoo mmoja,ila wakati mwengine tunakosa ili Mungu aoneshe ukuu wake,tukumbuke pia kuwa kuna Mungu maana kilasiku ukiwa unapata tuu,kila unachofanya inakuwa imo aaahh sasa si utajiona wewe ndio wewe tenaa na hata kutudharau tunaokosa,

5-Kukosa kwasababu ya visasi
Pengine unakosa kwasababu ya kuweka visasi na viapo vibaya kwa watu wengine,sikia sio kila anaekukosea basi ni wakumuwekea kisasi,kunamwengine amekosea kwa bahati mbaya bila kudhamiria hata kama hajaomba msamaha lakini ukiangalia unaweza kuona bahati mbaya ambayo hata wewe ungeweza kukosea basi usiweke kisasi na chuki na mtu huyo,tena mwengine na neno samahani katamka lakini bado unaweka kisasi.

Mwengine anaweza kuwa amekukosea kwa bahati mbaya bila yeye kujua kama kakosea kwahiyo akashindwa hata kusema samahani au kurekebisha kosa lake,wewe tayari ushaweka kisasi. Visasi vyetu vijana tunavijua ngoja nipate nitamuonesha au ngoja nipate nitawaonesha

My friend wengine ni watu wema sana kuliko sisi tunawawekea visasi hivyo unakuta Mungu hajapanga yule limkute unalopanga basi anaona njia ya kumuepusha yule ni kukunyima wewe hicho unacho.

Kunawakati kilakitu utafanya kwa usahihi na kwa umakini na weledi mkubwa lakini utakosa, basi usifadhaike piga goti sali huenda Mungu anaonesha ukuu wake kwako, kuwa yeye ndio mtoaji haijalishi unafanya vipi na kwa ubora na ukubwa gani waswahili wanamsemo wanasema “KUPATA KUNA MUNGU” kwahiyo usione unapata ukahisi wanaokosa ni wajinga au wanakosea au namna gani nyengne yoyote ila KUPATA KUNA MUNGU unachotafuta ili umkomeshe mwenzio, mwisho wa siku unafanya kila kitu sahihi kwenye utafutaji wako,unasali unatoa na sadaka lakini wapiii ngoma ngumu, mwisho wasiku unaenda mpaka kwa waganga lakini ngoma ngumu badoo.

Futa roho ya chuki na visasi huyo ndio mchawi wako, unachukia watu wenye makarama yao utakufa masikini,
Lakini pia usisahau kisasi ni haki kuna namna lazima mkosefu alipe,hakikisha unaweka kisasi cha haki.

Sasa basiii, Ukiona kunamtu umehitaji msaada wake na unahakika kabisa anaweza kukusaidia, kwasababu wewe sio mwehu uombe msaada kwa mtu ambae unajua kuwa hawezi kukusaidia msaada huo, yani unipigie simu mimi uniambie unashida na milioni 10 jioni ya leo wakati uwezo wangu wa buku na wewe nae utakuwa na nongwa sasaa.

Yani mtu anauwezo wa milioni unamuomba buku mbili afu anasema hana,unakesi ndogo polisi na unahisi kabisa kwa cheo na uwezo wake kakesi hako anakatatua hata kwa simu moja tuu au ujumbe mfupi then anakwambia bwana mimi siwezi kwenye hilo labda utafute mtu mwengine,
Na watu wengine wa aina hiyo

Maanazao zinaweza kuwa
1-Wewe sio wa muhimu kwao

2-wewe sio mtego wao(kwamba wanaamini wao watakuwa wanakusaidia wewe tuu na sio wewe kuwasaidia kwasababu labda shida zao zinaweza kuwa kubwa kuliko uwezo wako wa kicheo au kifedha hivyo hata wakikusaidia wewe huwezi kuwalipa chochote kesho) sana sana wao ndio watakuwa watoaji msaada kwako tuu kila siku.

zinaweza kuwa sababu nyingi sana lakini maranyingi hizo ndio kubwa haswaa,sasa na ww ujishikilie sio mtu hataki mazoea na wewe ya kimsaada na wewe unamuombaomba tuu, tafuta mgomba wako upige huohuo kilasikuu mpaka uchakae achana na asie na time na wewe, using’ang’anie kisa ni ndugu yako kabisa toka ntoke au ni rafiki yako damdam kabisaa,huo ni udugu wa kuzaliwa tuu na ni urafki wa kuzurira pamoja na kunywa bia tuu lakini sio kuwa ndio mnaweza kufaana kwenye shida, hata boss wako kazini sio kisa anakupa mshahara ndio ukadhani anakupenda,anakupa mshahara kwasababu ni haki yako sio kwasababu anapenda kukulipa,anakulipa kwasababu ya huo mkataba lakini anatamani ufanye kazi bure milele ndiomaana zamani sana kulikuwa na mambo ya watumwa hiyo yote ni kuonesha ni jinsi gani hata boss wako sio kuwa anaweza kukufaa kwenye shida eti kisa mwisho wa mwezi anakupaga milioni moja kama mshahara,basi ukiwa na shida ya elfu 20 basi atakusaidia,sahau hilo kwani msaada sio haki wala sheria ni moyo tuu

WEWE SASA UNAEOMBWA KILASIKU HUNA AU HUWEZI
Sio shida kusema huna kila tunavyoazima kwako. Au kusema kuwa huwezi labda jambo ni zito sana kwako,sisi tunaoomba tunaamini unaweza kutusaidia sasa unaposema huna au huwezi huwa tunajua huna na huwezi kweli,tunapoomba mara kadhaa na mara zote au maranyingi sana unasema huna au huwezi basi hapo ndipo tunapoona kuwa wewe sio mwenzetu tena,wewe sio ndugu yetu tena lakini usisahau kuwa likienda huwa linarudi, leo ukiwa huna na huwezi basi usishangae na mimi nikisema sina na siwezi, ndioo hata nikiwa na uwezo wa Mo Dewj au Aliko dangote ukiomba elfu 10 tuu nikisema sina usikunje, nikiwa na cheo cha Mama Samia ukikamatwa na puli la bangi au kuzurura hovyo usiku nikisema siwezi kukusaidia unielewe na kukubali,usianze kunung’unika…au unadhani ndugu zake Dangote wote wana mihela?

Eheee ujikazee,si ukidharau alipokuwa na shida yeye, Basi tulia na wewe dawa iingie. aana ni kweli kabisa hakuna mtu ambae hasaidii ila kunisaidia mm kweli sio lazima,kuna watu ambao unawasaidia pale wanapokuwa na shida tena haraka sana,hivyo kwa kuepusha lawama na mitusi isiyo na sababu ni bora usimuombe masada yule ambae hukuwahi kumsaidia alipohiyaji msaada wako. Kama mm ndio nimesema kabla kuwa ntakwambia sina ukilalamika sasa ndio ntakupiga shaba ufe, nenda kwa ndugu zako na rafiki zako uliokuwa unawapa hao hao ndio wakupe.

Mwisho mwisho kabisa ndugu jamaa na rafiki tuwatendee watu wote sawa,unaeweza kumsaidia msaidie,unaeweza kumfariji mfariji, unaeweza kumpa furaha mpe,yoyote anaekuomba msaada unaoona kabisa unaweza kumpatia basi mpatie, kaja kwako sio kwasababu wewe ni tajiri sana au unacheo kikubwa lakini anaimani sana na moyo na utu wako. Basi usimvunje moyo wake, msaidie kwa roho safi kabisa asipokulipa yeye atakulipa mwengine au atakulipa Mungu wako.

Tunaishi maramoja tuu hiyo pumzi uliyonayo ndio ya mwisho, saidia kufa kalipwe mema na Mungu wa haki,
Hakuna kikubwa na bora kama kuombewa mema na watu wengi haswa wale wema na wenye uhitaji (hapa nasema sio useme umemsaidia mlevi kununua pombe au teja kujidunga au kumsaidia mtu kufanya ubaya kwa mwengine) saidia wema kwa wema Mungu atakulipa mema zaidi,🥹

NOTE
Ukiona mtu amefanikiwa sana na hasaidii ndugu zake au baadhi ya ndugu zake. Au hasaidii wale rafiki zake unaoona walikuwa karibu sana wakati hana kitu basi wewe acha tuu yapite kama anakosea sawa kama yuko sawa ni sawa pia, wewe hayakuhusu,watu wamebeba mengi sana moyoni,watu wanapambana sana na kurudishwa nyuma na kukataliwa na hao wewe unaoona ni ndugu zake au ni rafikizake wa karibu sana lakini Wanaishi kwa kuvumilia tuu ili mambo mengine yaende,acha kuingilia maisha binafsi ya mtu,mengine hayasameheki japokuwa kusamehe ni bora zaidi na msamaha humuweka mtu huru.

Acha maisha ya mtu mafanikio yana njia nyingi ngumu na kumbukumbu nyingi ngumu ambazo nyengine sio rahisi kufutika.

“MIKONO INAYOTOA NI BORA KULIKO MIDOMO INAYOSALI”

*USILALAMIKE
HUNA NDUGU,HUNA KITU*

By Ochoa Jr.

Haya kwa yeyote yule mwenye kazi ya ujenzi na finishing ya jengo lake aje WHATSAPP yangu ajionee maajabu maana sisi hatufany kazi tuu ila tunafanya kazi za maajabu
+255 714 122 011
Ahsante
 
Huu ni uzi bora kwa kipindi hiki na nusu ya mwaka, ni uzi bora wa kufungia mwezi na ni uzi bora wa maandalizi ya kuingia mwaka mpya wa fedha. Hongera sana mwandishi.
 
Nzuri sana! Ukweli mtupu!
 
Na sisi tunajua,ndio mana tukizipata hatutaki mazoea na mtu mana wanafiki mnakua wengi.Ukiwa tajiri lazima waseme una roho mbaya mana wanajua we umezipata kilaini
 
Back
Top Bottom