Mhh hivi wote wanaoacha ni kwa ubaya.., Je haiwezekani mtu mnapendana ila kukaa kwenu pamoja mnagombana na kutiana huzuni na majonzi.., sababu ya utofauti fulani baina yenu, au labda kwa udhaifu wake anaondoka ila sio kwa kukutakia mabaya..
ngoja nikupe mfano wa kweli kuna mtu alimuacha mke wake akaenda kwa kimada, tena huyu alimuacha kwa vurugu na kumtelekeza yeye na watoto.., mwisho wa siku alikoenda mambo yakamuharibikia akapata ajali akawa kilema na akapooza mke mdogo kamuacha akarudi kwa mke wake wa kwanza, huyu mke wake wa kwanza akampokea na kumtunza mpaka kifo cha huyo baba...
Sasa swali linakuja Je ungekuwa wewe ni bora jamaa angefanikiwa au ungefurahia vile alivyopooza na angekuja kwako ungemfukuza na usingempokea ?