KERO Ukilipia kuingia Magufuli stendi wanarudisha chenji nusu kwa kigezo cha "hatuna chenji"

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mawele

Member
Jul 25, 2023
30
116
Ni mchezo mchafu wa wanaotoza hela kwa wanaotaka kuingia Magufuli stendi, ni mara kadhaa kila nikifika pale ukiwa na sh. 500 au 1000 nk watakwambia hawana shilini 100 au 200.

Mara nyingi wanafaya mchezo huo wakati kukiwa na msongamano wa foleni wanakwambia uchukue chenji nusu au wakurudishie hela ukatafute chenji urudi kupanga foleni upya, na watu kwa kuona usumbufu wa kupanga foleni na kwenda kutafuta chenji wanakubali kuacha hizo 200 au 100.

Wanachofanya ukienda kwa mtu wa kwanza anakwambia hamia dirisha la pili ndio kuna chenji ukienda la pili anadai nenda la 3 wa mwisho anakwambia wa kwanza ndio anachenji au ukatafute mweyewe na wakati huo watu wana haraka.

Kwa nini kila siku wao hawana chenji? Kwa nini wasiende kutafuta chenji benki kwa ajili ya huduma yao wanayoitoa huku wakijua inahitajika chenji kila siku?

Nachoamini ni mradi wa wizi wameanzisha maana hizo hela wanabaki nazo wao.

Mamlaka wafuatilieni wanaibia abiria makusudi na watu wanaoingia kupata huduma mbalimbali humo stendi.
 
Ni mchezo mchafu wa wanaotoza hela kwa wanaotaka kuingia Magufuli stendi, ni mara kadhaa kila nikifika pale huduma mbalimbali humo stendi.
Hii kawaida sana sehemu nyingi wanapotumia vishina
 
Janja janja kila mahali nchi hii. Ile ruhusa ya kula kwa urefu wa kamba itabidi ifutwe sasa, tunapigwa mpaka mia... mia...!!

Zikiunganishwa hapo jioni wanagawana elfu 30 zao maisha yanawaendea, kwa wiki, mwezi, mwaka... lazima wajenge.
 
Ni mchezo mchafu wa wanaotoza hela kwa wanaotaka kuingia Magufuli stendi, ni mara kadhaa kila nikifika pale ukiwa na sh. 500 au 1000 nk watakwambia hawana shilini 100 au 200.

ta huduma mbalimbali humo stendi.

Yaweza kuwa ni uzembe wa waendesha kituo ambao unapelekea kutafsiriwa kama wizi...
Kuna baadhi ya vituo vikubwa tu (hub) mfano Msamvu pale Morogoro huwezi kukuta uzembe wa kijinga kama huo
 
Janja janja kila mahali nchi hii. Ile ruhusa ya kula kwa urefu wa kamba itabidi ifutwe sasa, tunapigwa mpaka mia... mia...!!

Zikiunganishwa hapo jioni wanagawana elfu 30 zao maisha yanawaendea, kwa wiki, mwezi, mwaka... lazima wajenge.
Wasipokula wanatoa huduma hafifu, Bora wale wakuhudumie chapu kwa furaha, ukiona ofisi ya umma wanajivuta vuta kutoa huduma jua njaa imezidi hapo.
 
Ni mchezo mchafu wa wanaotoza hela kwa wanaotaka kuingia Magufuli stendi, ni mara kadhaa kila nikifika pale ukiwa na sh. 500 au 1000 nk watakwambia hawana shilini 100 au 200.

a kupata huduma mbalimbali humo stendi.
Ukisikia jiji la wezi maana yake ni hiyo, kama hukuibiwa mizungukoni basi lazima uibiwe hapo unapoaga jiji taka usitake, utatokaje Dar bila kuibiwa!!
 
Kuibiwa chenji.... Means unatoa Hela unarudishia chenji nusu. Sasa kama hujui unaondoka ukiamini kwamba ndio bei. Na hili wanalifanya Kwa kucheza na akili ya mtu anakuangalia uhakaraka wako uliokonao then ukishampa Hela anachoanza kukupa ni N card ili either usahau chenji au akupe chenji kiawamu.. mfano umelipa 1000 badala akurudishie 700 anaanza kukupa 500 ndo akuangalie kama unaondoka au vp... Na wengi wanaondoka wanaacha chenji zao
 
Back
Top Bottom