Abiria kulipa ushuru kwa kadi getini Stendi ya Magufuli hata kama ana tiketi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Manispaa ya Ubungo, imeanzisha utaratibu mpya wa kuingia na kadi katika stendi ya kimataifa ya mabasi ya Magufuli ili kudhibiti upotevu wa mapato kwa abiria wanaoingia katika kituo hicho kilichopo Mbezi Luis.

Hatua ya matumizi ya N- Card iliyoanza leo Jumatatu Februari 20, 2023 imelenga pia kupunguza changamoto ya foleni hasa wakati asubuhi ambapo kuna kuwa abiria na wasindikizaji wengi katika eneo hilo.

Kaimu Ofisa Habari wa Manispaa ya Ubungo, Joina Nzali amewaambia wanahabari katika mchakato huo wameshirikiana na Kituo cha Taifa cha Kutunza Kumbukumbu Kimtandao kilichoweka mfumo wa kieletroniki wa kukata na kudhibiti tiketi kwa kutumia milango ya kisasa.

" Mfumo huu utarahisisha huduma kwa wananchi kwa kukidhi mahitaji ya Serikali ya kukusanya mapato kidijitali, kupunguza foleni na kuondoa matumizi ya fedha taslimu kwa watendaji wetu.

"Kwa upande wa abiria asiyekuwa na kadi, akifika stendi atapatiwa kadi ya kutumia mara moja ambayo akipita itabaki kwenye mlango kwa kumezwa," amesema Nzali.

Hata hivyo, Nzali amesema kwa matumizi ya kadi, kila abiria atalazimika kulipia ushuru getini kwa kutumia N- Card hata kama ameshakata tiketi ya basi husika. Amesema awali abiria akiwa na tiketi anapita bila kulipa ushuru, lakini hivi sasa atalipia.

Chanzo: Mwananchi
 
Kumbe lengo ni kuwabana abiria, kila zigo zito anatupiwa mwananchi wa chini huku wenyewe wanatembelea V8
 
Aisee kazi ipo hadi abiria nilipe wakati wa kuingia ilhali niko na tiketi kwa ajili ya kusafiri! Haina shida tukamueni tu si mmeamua bhana.
 
Airport mbona hakuna hivi vitu. Standard za usafirishaji zipo wazi na sasa sio kama zamani mtu alipe kodi tu ili aende kumuaga ndugu na jamaa wakiwa wanasafiri.

Mfano wa airports ni mzuri kwani unafanya kazi dunia nzima. Kodi ni muhimu sana lakini pia ukusanaji wake ni muhimu pia.

Again kwanini airports hakuna au watu wanao safiri na ndege ni matajiri sana hawahitaji kusumbuliwa na maskini ndio inastahili.
 
Hizo kodi zinakusanywa , then sio zote zinafika. Sehemu husika unaweza shangaa in reality or ki uhalisia kuwa millioni 200 kwa mwezi zimekusanywa , ila 120 millioni ndo zinafika sehemu husika....
 
Manispaa ya Ubungo, imeanzisha utaratibu mpya wa kuingia na kadi katika stendi ya kimataifa ya mabasi ya Magufuli ili kudhibiti upotevu wa mapato kwa abiria wanaoingia katika kituo hicho kilichopo Mbezi Luis.

Hatua ya matumizi ya N- Card iliyoanza leo Jumatatu Februari 20, 2023 imelenga pia kupunguza changamoto ya foleni hasa wakati asubuhi ambapo kuna kuwa abiria na wasindikizaji wengi katika eneo hilo.

Kaimu Ofisa Habari wa Manispaa ya Ubungo, Joina Nzali amewaambia wanahabari katika mchakato huo wameshirikiana na Kituo cha Taifa cha Kutunza Kumbukumbu Kimtandao kilichoweka mfumo wa kieletroniki wa kukata na kudhibiti tiketi kwa kutumia milango ya kisasa.

" Mfumo huu utarahisisha huduma kwa wananchi kwa kukidhi mahitaji ya Serikali ya kukusanya mapato kidijitali, kupunguza foleni na kuondoa matumizi ya fedha taslimu kwa watendaji wetu.

"Kwa upande wa abiria asiyekuwa na kadi, akifika stendi atapatiwa kadi ya kutumia mara moja ambayo akipita itabaki kwenye mlango kwa kumezwa," amesema Nzali.

Hata hivyo, Nzali amesema kwa matumizi ya kadi, kila abiria atalazimika kulipia ushuru getini kwa kutumia N- Card hata kama ameshakata tiketi ya basi husika. Amesema awali abiria akiwa na tiketi anapita bila kulipa ushuru, lakini hivi sasa atalipia.

Chanzo: Mwananchi
Kuna haja kweli ya kupandia basi hapo? Na wanaotelemka inakuwa aje?
 
Back
Top Bottom