Ukijifunza kwa waliofanikiwa, hawawezi kukupa njia za mafanikio

Nyafwili

JF-Expert Member
Nov 27, 2023
2,779
6,901
Habari wana JamiiForums, poleni na majukumu ya hapa na pale šŸ¤

Imekuwa kawaida sasa kwa watu waliofanikiwa kiuchumi kubaki na siri zao namna walivyo ukimbia ukata, kila Tajiri utakaye muuliza kuhusu mafanikio yake lazima atakuambia:

ā€¢ Nilianza kuuza karanga za kupima.

ā€¢ Nilianza kushona viatu maeneo ya Ubongo (shoe shine).

ā€¢ Nilianza kuuza sumu ya panya, sumu ya mende, sumu ya viroboto, sumu ya kunguni na utitiri.

Baada ya hapo nilidunduliza mpaka unavyo niona sasa nimesimama katika uchumi wa kati.

Majiri nikweli ufanye biashara ya kushona viatu (shoe shine) au kuuza sumu ya panya alafu uwe Tajiri mkubwa?
 
Umewauliza wangapi? Ama una ukaribu na wangapi?

Binafsi naamini kama una nia ya kufanikiwa, njia utaipata tu

Tatizo, ni kuamini ukisali utafanikiwa, au ukiloga utafanikiwa, hii inatengeza a mental ceiling uwezo wa kufikiri unapungua
Kama ni mkristo kasome biblia vizuri wengi wanaisoma biblia kama kitabu cha hadithi biblia inaeleza kila kitu kwa mafundisho kutoka kwa manabii na mifano biblia inatupa miongozo yote katika kupata mafanikio/utajiri mifano mingi ipo katika biblia

Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa
Paulo alifanya maombi kwa wakolosai ili wajazwe maarifa

Wakolosai 1:9
 
Kama ni mkristo kasome biblia vizuri wengi wanaisoma biblia kama kitabu cha hadithi biblia inaeleza kila kitu kwa mafundisho kutoka kwa manabii na mifano biblia inatupa miongozo yote katika kupata mafanikio/utajiri mifano mingi ipo katika biblia

Kumcha Mungu ni chanzo cha maarifa
Paulo alifanya maombi kwa wakolosai ili wajazwe maarifa

Wakolosai 1:9
Kumcha Mungu kunapunguza uwezo wa kufikiri kwasababu; huchanganui mambo, kila kitu unakihusianisha na 'ulimwengu wa roho'

Mungu mwenyewe hayupo.
 
Siri kubwa niliyoiona ni kujibana. Hao jamaa inawezekana maana wanasave ili kiwe kingi wainvest.

Nidhamu ya kusave ndio wengi hakuna.

Kuna jamaa namfahamu akiwa tajiri sishtuki. Aliwahi kuwa tajiri akafirisika.

Amekuja DSM, lowest profile. Kajifunza kupaka rangi nyumba etc. Hana mke hana mchepuko hapa mjini. Yeye kazi yake ni kutuma pesa bank tu hata kama ni ten, anapiga kazi na kula na kutuma pesa bank. Alianza kulala kwenye pagala akiwa kama mlinzi, Naamini kwa trend yake miaka 4 atakuwa na pesa nyingi sana.

Na anaufahamu mkubwa sana, ingawa huwezi kumsikia anaongea chochote kuhusu pesa. Yeye muda wote hana pesa na ni kweli hata ukimkagua hana.
 
Habari wana JamiiForums, poleni na majukumu ya hapa na pale šŸ¤.

Imekuwa kawaida sasa kwa watu waliofanikiwa kiuchumi kubaki na siri zao namna walivyo ukimbia ukata, kila Tajiri utakaye muuliza kuhusu mafanikio yake lazima atakuambia:-

ā€¢ Nilianza kuuza karanga za kupima.

ā€¢ Nilianza kushona viatu maeneo ya Ubongo(shoe shine).

ā€¢ Nilianza kuuza sumu ya panya, sumu ya mende, sumu ya viroboto, sumu ya kunguni na utitiri,

Baada ya hapo nilidunduliza mpaka unavyo niona sasa nimesimama katika uchumi wa kati..

Majiri nikweli ufanye biashara ya kushona viatu( shoe shine) au kuuza sumu ya panya alafu uwe Tajiri mkubwa??
Matajiri mnaitwa huku Kuna Uzi wenuuuā˜ŗļøā˜ŗļøšŸ˜ŠšŸ˜Š
 
Back
Top Bottom