Wafu hawana simulizi: Jinsi hadithi za waliofanikiwa zinavyoweza kukupotosha na kukupoteza

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,781
3,074
Rafiki yangu mpendwa,

Hadithi za watu waliofanikiwa huwa zinatupa hamasa kubwa sana kwamba hata sisi pia tunaweza kufanikiwa. Huwa zinatupa ile hali kwamba kwani wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini.

Hivyo waandishi na wahamasishaji wamekuwa wakizitumia hadithi hizi kwenye habari na mafundisho yao mbalimbali kama sehemu ya kuwapa wengine hamasa ya kufanikiwa pia.

Ni nia njema sana, na inayolenga mambo mema kwa wale wanaopokea taarifa hizi, lakini pia inaweza kuwa njia inayopotosha na kuwapoteza wale wanaopokea taarifa hizo za hadithi za mafanikio ya baadhi ya watu.

Watu wanapofanikiwa, huwa zinatengenezwa hadithi nzuri sana za nini kimesababisha mafanikio yao. Na sifa nyingi hutolewa kwao, kuhusu uchapakazi wao, uchukuaji wao wa hatua za hatari na uwezo wao mkubwa wa kuziona na kuzichukua fursa mbalimbali.

Lakini kipo kitu kimoja kinachochangia mafanikio ya walio wengi ambacho kimekuwa hakijumuishwi kwenye hadithi za mafanikio tunazopewa. Kitu hicho ni BAHATI. Ndiyo, kuna watu wengi sana wamefanikiwa kwa bahati tu. Watu hao wanakuwa walikutana na bahati fulani kwenye safari yao ya mafanikio, ambayo iliwapa upendeleo fulani ambao wengine hawakuupata na ndiyo maana wamefanikiwa.

Lakini wakati wa kuandaa hadithi za mafanikio, bahati huwa haipati nafasi kabisa kwenye hadithi hizo, hivyo wale wanaopokea hadithi hizo, wanaweza kukazana kile ambacho waliofanikiwa wamefanya lakini wasipate matokeo kama yao, kwa sababu hawakuambiwa kwamba kuna bahati watu hao walikutana nazo. Na hapo ndipo hadithi hizi zinakuwa zimewahadaa na kuwapoteza badala ya kuwa msaada kwao.

Mwanahisabati, mwekezaji, mwanafalsafa na mwandishi Nassim Nicholas Taleb ni mmoja wa watu ambao wameandika sana kuhusu mchango wa bahati kwenye mafanikio ya walio wengi. Kupitia kazi yake ya uwekezaji, hasa wa kununua na kuuza hisa (trading) ameweza kujifunza kwa uhalisia kwamba wale ambao wanaonekana wana mafanikio kwenye biashara hiyo siyo kwa sababu ya ubora wao, bali ni kwa bahati tu.

Kwenye kitabu chake alichokiita Fooled by Randomness: The Hidden Role of Chance in Life and in the Markets, Taleb anasema mafanikio yamekuwa yanawadanganya watu wengi sana. Mafanikio ya wengi yanakuwa yametokana na bahati fulani ambayo hata wao wenyewe hawawezi kuielezea, lakini wanaamini ni juhudi walizoweka na hata watu wa nje nao wanaamini hilo.

fooled by randomness cover.jpg

Kwenye kitabu hiki, Taleb ametumia mfano wa wawekezaji ambao wamefanikiwa kwa miaka mitano mfululizo, hawa wanaweza kuonekana wanaijua siri ya uwekezaji na hivyo hadithi zao zikatumika sana. Lakini kumbe kilichowawezesha kuwa na mafanikio hayo ni bahati tu.

Anasema chukua mfano wa wawekezaji elfu kumi ambao wanafanya uwekezaji ambao unaamuliwa kwa kurusha shilingi. Nusu wana nafasi ya kupata faida ya milioni kumi kwa mwaka na nusu wanapata hasara ya milioni kumi. Hivyo mwaka wa kwanza unapoisha, wawekezaji elfu 5 wamepata faida ya milioni kumi, na elfu 5 wamepata hasara ya milioni kumi.

Mwaka wa pili, wale elfu tano waliopata hasara hawaonekani tena, wale elfu 5 waliopata faida wanaendelea na uwekezaji. Nafasi ni ile ile, nusu wanafanikiwa, nusu wanashindwa. Hivyo mwisho wa mwaka wa pili, wawekezaji 2500 wanakuwa wametengeneza faida kwa miaka miwili mfululizo.

Mwaka wa tatu, wawekezaji 1250 wanakuwa wametengeneza faida, mwaka wa nne 625 na mwaka wa tano wawekezaji 312 wanakuwa wametengeneza faida kwa miaka mitano mfululizo. Kumbuka hii yote ni kwa bahati tu, hakuna ujanja wowote.

Sasa akichukiliwa mmoja katika hao 312 waliopata faida kwa miaka mitano mfululizo, atapewa kila aina ya sifa. Hadithi yake ya mafanikio itakuwa ya kuvutia na ya kuhamasisha. Tutaambiwa huwa analala na kuamka saa ngapi, huwa anafanya nini anapoamka, anasoma vitabu gani pamoja na nguo gani anazovaa siku anapofanya maamuzi ya uwekezaji.

Sasa huyu aliyechaguliwa kama hadithi ya mafanikio kwenye mwaka wa tano, anaenda kwenye mwaka wa sita wa uwekezaji, na kwa sababu ni bahati tu, safari hii anakuwa kwenye ile nusu ya walioshindwa. Hadithi yake ya mafanikio inabadilika. Wale walioleta hadithi juu ya mafanikio yake na siri za mafanikio, watakuja na sababu kwa nini ameshindwa. Wataonesha vitu vipya alivyojaribu kufanya kwenye mwaka wa sita ambavyo hakuwa anafanya miaka ya nyuma, watamlaumu kwa kulewa mafanikio na kuacha kujituma kama awali na mengine mengi.

Lakini hakuna popote katika hadithi hizo za mafanikio ambapo kutaeleza mchango wa bahati kwa watu kama hao katika kufanikiwa kwao au mchango wa bahati mbaya katika kushindwa kwao.

Hii ina maana gani? Je hakuna siri za mafanikio?

Haya ni maswali unayoweza kujiuliza kutokana na makala hii ya leo, na kuona labda siri zote za mafanikio ambazo hata mimi nimekuwa nakushirikisha nimekuwa nakudanganya na kukuhadaa. Lakini siyo hivyo.

Kama ambavyo nimekuwa nakushirikisha kwenye mafunzo mengi, kwanza kabisa hakuna siri za mafanikio, siri ni kitu kilichofichwa, lakini kwenye mafanikio, hakuna kilichofichwa.

Kwenye mafanikio kuna misingi, ambayo ukiishi unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa kuliko wale ambao hawaishi misingi hiyo. Lakini pia kuishi misingi hiyo hakukupi uhakika wa asilimia 100 wa mafanikio, kwa sababu bado bahati ina nafasi yake.

Unaweza kukutana na bahati nzuri kwenye maisha yako na ukafanikiwa au ukakutana na bahati mbaya kwenye maisha yako na ukashindwa licha ya kuiishi vizuri misingi ya mafanikio.

Mambo matano ya kuzingatia ili kuivuta bahati nzuri kuja upande wako.

Rafiki, baada ya kuona nafasi kubwa ya bahati kwenye mafanikio yetu, swali la wengi linaweza kuwa je kuna namba ya kuvuta bahati nzuri kuja upande wetu ili tuweze kufanikiwa? Jibu ni ndiyo, ipo namna ya kuvutia bahati nzuri kuja upande wako. Na hapa kuna mambo matano ambayo ukiyafanya, utavutia bahati nzuri kuja upande wako na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa.

MOJA; KUWA NA MAANDALIZI BORA.

Kwenye mafanikio huwa wanasema bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi. Kwenye mfano tuliotumia hapo juu wa wawekezaji, pamoja na kuwepo kwa bahati, lakini lazima anayepata bahati awe tayari kwenye uwekezaji. Hivyo bahati haitakufuata kitandani ukiwa umelala. Hata kwenye michezo ya bahati nasibu, mshindi hatangazwi tu kwa sababu ana bahati, lazima achukue hatua ya kucheza bahati nasibu hiyo.

Hivyo wewe angalia ni eneo lipi unalotaka kufanikiwa, kisha hakikisha una maandalizi bora kabisa. Kama ni kwenye kazi basi hakikisha unaijua vizuri kazi yako na kuweza kuifanya kwa ubora wa hali ya juu sana. Kama ni biashara hakikisha unaijua vizuri biashara yako kwa kila eneo na unajuana na watu wengi wanahusika na biashara yako.

Kadiri unavyojua kwa kina kile unachofanya na unavyojuana na watu muhimu wanaohusika na kitu hicho, unajiweka kwenye nafasi ya kukutana na bahati. Mfano kama unafanya kazi yako vizuri, na anatafutwa mtu wa kuwakilisha eneo lako la kazi kwenye tukio fulani, wewe utachanguliwa, ni bahati, lakini kwa sababu tayari ulikuwa na maandalizi mazuri.

MBILI; PIMA HATARI ZAKO VIZURI.

Mmoja wa wawekezaji wenye mafanikio makubwa duniani na mwenye historia ya kupata faida kwa kiwango kikubwa kwenye uwekezaji ni Bilionea Warren Buffett. Yeye huwa anasema ana sheria kuu mbili kwenye uwekezaji. Sheria ya kwanza ni KAMWE USIPOTEZE FEDHA. Na sheria ya pili ni USISAHAU SHERIA NAMBA MOJA. Kwa sheria hizo mbili, Buffett ameweza kuwa na mafanikio kwenye uwekezaji kwa zaidi ya miaka 50.

Pima hatari zako vizuri kabla hujaingia. Kumbuka mfano tulioanza nao hapo juu, ukishapata hasara kubwa, umeondoka kabisa kwenye mchezo. Hivyo lengo lako kubwa linapaswa kuwa kutokupata hasara kubwa kwenye jambo lolote lile.

Achana na zile hadithi za mafanikio kwamba waliofanikiwa ni ‘RISK TAKERS’ kwamba wanachukua hatua kubwa na kupata mafanikio makubwa. Unachopaswa kukumbuka ni kwamba wafu huwa hawana simulizi. Wanaweza kuchukua hatari watu kumi, tisa wakafa na mmoja akapona. Mmoja aliyepona atakuwa na simulizi nyingi za namna gani alichukua hatari hiyo kwa umakini (hatataja bahati) lakini wale kumi hawatakuwepo kukuonya usijaribu.

Pima hatari kabla hujaingia, usijiingize kwenye hatari kubwa kuliko uwezo wako wa kustahimili au kumudu kurudi kwenye njia pale unapoanguka.

TATU; KUWA KING’ANG’ANIZI.

Hakuna mtu yeyote anayefanikiwa kwa mara ya kwanza anapojaribu kitu. Kila mtu anakutana na ugumu na vikwazo mbalimbali mwanzoni. Hii huwa ni kama njia ya dunia kuwapunguza wale ambao hawajajitoa kweli ili kufanikiwa.

Hivyo unapokutana na ugumu na vikwazo mwanzoni usikate tamaa, badala yake ng’ang’ana. Endelea kujifunza na kuwa bora zaidi. Angalia ni maeneo gani unakutana na bahati mbaya na jifunze kuzikwepa. Pia angalia ni namna gani unaweza kujitengenezea bahati nzuri.

Na uhimu zaidi, hakikisha hufi, maana wafu hawana simulizi, hakikisha unapima vizuri hatari kabla ya kuingia. Ni bora kwenda taratibu lakini ufike, kuliko kwenda haraka na ufe kabla ya kufika.

NNE; ZUNGUKWA NA WALE WANAOFANYA.

Hadithi za mafanikio zina hamasa nzuri, lakini huwa ni hadithi za nyuma, huwa tunaoneshwa watu hao walitoka sifuri na sasa wapo kileleni. Hivyo hatuoni kila hatua waliyopiga na namna walivyopambana na magumu waliyokutana nayo kwenye safari hiyo.

Njia bora kabisa ya kupata hamasa ya kukusukuma kwenye safari yako ya mafanikio ni kuzungukwa na wale ambao wanafanya sasa. Wale ambao ndiyo wanaanzia sifuri kama wewe na kwa pamoja mnakwenda kileleni. Hapa chagua watu ambao unaona kabisa wamejitoa ili kufanikiwa, watu ambao wapo tayari kupambana na kung’ang’ana mpaka wafanikiwe, kisha ambatana na watu hao, shikana nao.

Hawa ndiyo watakaokuonesha wazi namna ya kuvuka changamoto mbalimbali, kwa sababu hata wao wanazivuka. Hawa ndiyo watakufundisha maana ya ung’ang’anizi, maana nao wanang’ang’ana. Na unapochagua watu hao vizuri, mafanikio ya mmoja wenu yanakuwa mafanikio yenu wote.

TANO; ANGALIA IDADI YA WALIOANZA NA SIYO WALIOMALIZA.

Taleb anatuambia kila unaposikia hadithi ya mafanikio ya mtu yeyote yule, usimwangalie yeye peke yake, badala yake angalia ni watu wangapi ambao walianza naye na kwa sasa wako wapi.

Tukiangalia mfano tuliotumia kwenye makala hii, walianza wawekezaji elfu 10, baada ya miaka mitano walikuwa wamebaki 312 pekee, hii ni sawa na asilimia 3 ya wale walioanza ndiyo wamefanikiwa. Asilimia 97 wamepotea kabisa na hawajulikani walipo.

Huwezi kutengeneza hadithi yoyote ya mafanikio yenye usahihi kama watu 97 kati ya 100 wanashindwa na watatu pekee ndiyo wanafanikiwa. Hapo ni bahati tu inakuwa imefanya kazi.

Hivyo kabla ya kujiambia kwamba wewe umeshindwa kufanikiwa kwa sababu huijui misingi au siri za mafanikio, angalia namba ya walioanza na waliomaliza, kama walioanza ni wengi na walimaliza ni wachache, bahati inahusika na hivyo rudi kwenye kujijengea bahati yako kama tulivyojifunza hapo juu.

Rafiki, hivyo ndivyo hadithi za mafanikio zinavyowapotosha na kuwapoteza watu wengi. Kwa kuwaangalia wachache waliofanikiwa na kuwasahau wengi walioshindwa, tunakosa nafasi ya kujua mchango wa bahati kwenye mafanikio ya walio wengi.

Fanyia kazi haya uliyojifunza, hasa mambo matano ya kufanya ili kuvuta bahati upande wako na mara zote usisahau kutambua mchango wa bahati kwenye mafanikio yako na ya wengine pia.

Kwenye uchambuzi wa kina wa kitabu FOOLED BY RANDOMNESS: The Hidden Role of Chance in Life and in the Markets kilichoandikwa na Nassim Nicholas Taleb tutakwenda kujifunza nafasi ya bahati kwenye maeneo mbalimbali ya maisha ambayo wengi huwa hawaioni. Mwandishi anatuonesha jinsi hata wasomi, hasa wanahisabati, wanatakwimu na wanasayansi wanavyofanya makosa makubwa kwa kuchukulia bahati kama sheria.
 
Kupata uchambuzi wa kina wa kitabu hicho pamoja na vitabu vingine vingi, jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kuvungua hapa; SOMA VITABU TANZANIA

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania
Thanks kwa nakala nzuri yenye mafunzo bora ndani yake......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Nimeanza na mtaji wa elfu 10" - Shamimu Zeze.
Ecclesiastes 9:11 King James Version

11 I returned, and saw under the sun, that the race is not to the swift, nor the battle to the strong, neither yet bread to the wise, nor yet riches to men of understanding, nor yet favour to men of skill; but time and chance happeneth to them all.
 
Bahati haiji bila kutake risk. Tena ile risk ambayo inaweza kuku gharimu hata maisha.
Na kila risk lazima uilipie

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli, na kama nilivyoeleza kwenye pointi namba mbili, PIMA HATARI ZAKO VIZURI. Maana wengi kati ya wanaochukua hizo hatari wanapotea, na wachache sana wanaofanikiwa ndiyo tunasikia habari zao.
Usikubali kuwa mmoja wa wale wanaopotea, hakikisha unabaki kwenye mchezo.
 
BAHATI UNAZUNGUMZIA AFRICA? Hebu tuambia mwanzilishi wa Alibaba Jackma kakutana na bahati gani.Je Henery Ford wakati ana vumvua Gari alikutana na bahati gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanakuwa wamepredict kesho itakuwaje, mwanzilishi wa Amazoni alipredict kesho itakuwaje na akaanza kuofanyia kazi hiuo kesho.

Wazungu hawaamini katika Bahati wanaamini katika kufight na kutumia vyema furusa walizo nazo.

BAHATI ni kusolve matatizo ya wa tu basi zaidi ya hapo haku a kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waswahili wana semi zenye mantiki kwelikweli kama vike 'Asiyebahatisha habahatiki', 'Mtembea bure si sawa na mkaa bure' n.k.
Bahati huweza kujitokeza zaidi kwa idadi kubwa ya majaribio kuliko idadi ndogo ya majaribio.
Mara nyingi timu ya mpira wa miguu inayoshambulia mara nyingi ina uwezekano zaidi wa kupata goli kuliko inayo shambulia mara chache.

Mkulima anayejaribu kulima nyanya au mahindi miaka mitano mfululizo ana fursa zaidi ya kukutana na mwaka au msimu wenye bei nzuri kuliko yule anayeingia na kutoka.

Mfanyabiashara wa wakati wote ni rahisi kupata wateja wengi kuliko mfanyabiashara wa kuvizia.

Hesabu za yamkini hapa zinahusika. Jinsi matukio ya jambo yanavyokuwa mengi ndivyo uwezekano wa matokeo chanya au hasi yanavyozidi kuwa makubwa.

Wanaosema mafanikio yanategemea bahati hawajakosea iwapo tu wanazingatia kuna majaribio ya kubahatisha kwa kiwango gani.

Mkuu hujaelewa kabisa somo lililotolewa na mtoa mada.
Kama ingekuwa ni mtihani wa NECTA ungepata division 5.
Swali la kujiuliza ni kwamba njia alizopitia huyo mwanzilishi wa Amazon hakuna watu wengine waliopitia njia Kama zake dunia nzima au ulaya na marekani?
Na je Kama wapo wengi waliopitia njia Kama zake kwa nini hawajafanikiwa kufikia level Kama huyu mwanzilishi wa Amazon?
Jibu unalo mwenyewe!
Usipoelewa na hapa Basi mwalimu wapo alipata kazi ngumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waswahili wana semi zenye mantiki kwelikweli kama vike 'Asiyebahatisha habahatiki', 'Mtembea bure si sawa na mkaa bure' n.k.
Bahati huweza kujitokeza zaidi kwa idadi kubwa ya majaribio kuliko idadi ndogo ya majaribio.
Mara nyingi timu ya mpira wa miguu inayoshambulia mara nyingi ina uwezekano zaidi wa kupata goli kuliko inayo shambulia mara chache.

Mkulima anayejaribu kulima nyanya au mahindi miaka mitano mfululizo ana fursa zaidi ya kukutana na mwaka au msimu wenye bei nzuri kuliko yule anayeingia na kutoka.

Mfanyabiashara wa wakati wote ni rahisi kupata wateja wengi kuliko mfanyabiashara wa kuvizia.

Hesabu za yamkini hapa zinahusika. Jinsi matukio ya jambo yanavyokuwa mengi ndivyo uwezekano wa matokeo chanya au hasi yanavyozidi kuwa makubwa.

Wanaosema mafanikio yanategemea bahati hawajakosea iwapo tu wanazingatia kuna majaribio ya kubahatisha kwa kiwango gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu maelezo yako sio sahihi.
Wewe hujawahi kukutana na mtu anakusimulia amefanya kila aina ya biashara miaka hata 20 halafu hatoboi.
Halafu Kuna mwingine anaanza biashara ya kwanza halafu hata mwaka mmoja hauishi anatusua.
Au mfano mwingine hujawahi kuona mtu anaenda kwenye mgodi wa dhahabu anapambana hata miaka 30 hapati kitu zaidi ya hela za kula tu,halafu mwingine anaenda huko huko anakaa miezi michache tu anaokota jiwe la mamilioni.
Na katika huo mfano wako wa soka hujawahi kusikia au kuona kwenye mechi timu A imeshambulia Sana timu B lkn kila wakipiga mashuti kwenye goli la timu B mpira unagonga mwamba halaf timu B ilikuwa haishambulii lakini wakapiga shuti moja tu kwenye lango la timu A na goli linaingia na kuwapa ushindi.
Hiyo ndio maana ya bahati Kama ulikuwa hujui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bahati is simply when an opportunity finds you ready prepared. Huwezi kupata bahati kama hukujiandaa. Bahati tunayozungumzia hapa ni ile tofauti na ya michezo ya kubahatisha.
 
BAHATI UNAZUNGUMZIA AFRICA? Hebu tuambia mwanzilishi wa Alibaba Jackma kakutana na bahati gani.Je Henery Ford wakati ana vumvua Gari alikutana na bahati gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mazingira waliyozaliwa peke yake ni bahati tosha,
Wakati waliozaliwa pia ni bahati.
Ukisoma kitabu cha OUTLIERS, mwandishi ameonesha mabilionea walionufaika na viwanda marekani (kina ford, rockerfeller, carnegie) walizaliwa miaka ya 1830s hivyo wakati wanafikia umri wa kuanza kazi na biashara ndiyo ufuaji wa chuma ulikuwa umeanza na hivyo wakanufaika sana.
Pia ameonesha mabilionea walionufaika na teknolojia (kina Gates, Jobs na wengineo) wamezaliwa miaka ya 1950s, wakati wanafikia ujana ndiyo kompyuta zilikuwa zimeanza na hivyo wakawa watu wa kwanza kuingia na kunufaika.
Kadhalika ukiangalia sasa, mabilionea wanaonufaika na mitandao ya kijamii wamezaliwa 1980s kipindi wanafikia ujana ndiyo mitandao ya kijamii imeibuka na wao kuwa wa kwanza kunufaika nayo.
Hivyo mazingira na hata kipindi cha kuzaliwa ni bahati pia.
Hivi unafikiri Mark Zuckerberg angezaliwa Afrika hiyo miaka ya 80 angeweza kuwa mwanzilishi wa FACEBOOK?
Look closely, you will see the hidden role of chance in every success.
 
Waswahili wana semi zenye mantiki kwelikweli kama vike 'Asiyebahatisha habahatiki', 'Mtembea bure si sawa na mkaa bure' n.k.
Bahati huweza kujitokeza zaidi kwa idadi kubwa ya majaribio kuliko idadi ndogo ya majaribio.
Mara nyingi timu ya mpira wa miguu inayoshambulia mara nyingi ina uwezekano zaidi wa kupata goli kuliko inayo shambulia mara chache.

Mkulima anayejaribu kulima nyanya au mahindi miaka mitano mfululizo ana fursa zaidi ya kukutana na mwaka au msimu wenye bei nzuri kuliko yule anayeingia na kutoka.

Mfanyabiashara wa wakati wote ni rahisi kupata wateja wengi kuliko mfanyabiashara wa kuvizia.

Hesabu za yamkini hapa zinahusika. Jinsi matukio ya jambo yanavyokuwa mengi ndivyo uwezekano wa matokeo chanya au hasi yanavyozidi kuwa makubwa.

Wanaosema mafanikio yanategemea bahati hawajakosea iwapo tu wanazingatia kuna majaribio ya kubahatisha kwa kiwango gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante mkuu, umeongeza mifano mizuri sana.
Na hii ndiyo dhana nzima, kwamba bahati inamfikia yule aliye kwenye mchakato, lakini kukataa kwamba hakuna bahati ni kujidanganya.
 
Back
Top Bottom