Ukweli gazeti la Rai la leo tarehe 26Aug2010 limeniboa sana. Kwamba ni mwendawazimu tu ndie atakayempigia kura upinzani. Hoja yenyewe sio ya kweli zaidi ya upotoshaji. Kwamba wapinzani wameshashindwa. Kisa hawana wabunge wa kutosha. Upotoshaji. Uingereza Labour walikuwa na wabunge wachache wakaunda mseto, ipo hapa kwetu na mataifa mengi yaliyoendelea. Lakini sishangai kwa kuwa wanaoandikia gazeti hili ni vibaraka wa Rostam Aziz, mtu liyekuja kuchuma kiharamu TZ
Martinez, nadhani sio sahihi kuliita Rai ni kibaraka wa CCM, ni sawa na kuliita gazeti la Uhuru ni kibaraka wa CCM, au Tanzania Daima ni kibaraka wa Chadema.
Kibaraka ni yule mtu ambae anadhaniwa kuwa siye, kumbe siye, hivyo magazeti yenye sifa ya kuitwa vibaraka, ni yale ambayo hayamilikiwa na wanazi wa CCM, ila yanajikomba komba ili angalau waambulie makombo.
Kwa vile Rai, linamilikiwa na fisadi mkuu wa CCM, na alilinunua kwa mabaki ya lile fungu la Kagoda, lazima alikuwa na malengo mpaka kulinunua gazeti hilo, hivyo kinachofanyika sasa ni kutimiza yale malengo makuu kusudiwa, hivyo huko sio kujikomba, ni kutimiza wajibu wake kulikopelekea likanunuliwas na kumilikiwa.
Katika kutimiza malengo hayo, issue ya fair, balance, objectivity, impartiality, right to privacy ambazo ni pillars muhimu kwa chombo cha habari, haziapply hapa ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa
Nilishasema kwenye thread fulani kule nyuma, familia ya magazeti ya Habari Corp, yako mkao wa kifo. Baada ya uchaguzi, mtalishuhudia hili, wenye kumbukumbu mtakumbuka ilishawahi kusemwa hapa JF..
Kama Kulikoni limekufa kifo cha mende, na This Day linapumulia mashine, uwezo wa mmiliki wake unajulikana, itakuwa Habari Corp!, baada ya kutimiza malengo, yatakuwa ni what for?, yataachwa yajifie kifo cha mende!.