UKAWA mnafanya kosa la kiprotokali

UKAWA mnafanya kosa la kiprotokali

Nyie wakatoliki mnatuuza sana nchi hii yule padre wenu kala mgao Wa escrow mil 80 mmepiga kimya pengo Leo kawasaliti wenzie mnaona poa semen kama mnafaidika na ccm
 
Mkuu meningitis tamaa ya urais ya hao jamaa wawili imeshawaweka pabaya bila wenyewe kujielewa.

Mingoi ni wengi wenye tamaa hiyo ya urais lakini katika hili wameshtuka.
hata mamvi mzee wa kupendwa amebana kimya kwani anajua madhara ya kumtembelea Gwajima katika muktadha huu.
 
Last edited by a moderator:
Hapo upo sawa hata mi mkatoliki sijafurahishwa na kitendo cha pengo kutukanwa n ukawa wajue wakatoliki ni wingi na wanasikiliza viongozi wao wa dini so wakifanya ujinga kwa hilo kweli watapoteza

Acheni ujinga nami ni mkatoliki, nasi hatumsikilizi pengo bali baraza la maaskofu Tanzania ambapo pengo ni mjumbe tu sio mwenezi.
 
Acheni ujinga nami ni mkatoliki, nasi hatumsikilizi pengo bali baraza la maaskofu Tanzania ambapo pengo ni mjumbe tu sio mwenezi.
Hoja ya hapa sio kumsikiliza au kutomsikiliza Pengo.Hoja ni matusi dhidi ya Pengo na sympath ya wanasiasa kwa Gwajima.

Gwajima amesababisha mchanganyo wa kihisia kwa jamii ya kikatoliki na hivyo sio muda muafaka kwa viongozi wa kisiasa kuwa au kutokuwa upande wake kwa sasa.
 
Ninauhakika Gwajima uko alipo anajutia mdomo wake.
 
Kumtembelea mgonjwa haimaanishi kuwa unashiriki matendo au uovu wake.... Papa John Paul II alimtembelea alotaka kumuua.. Yesu aliwatembelea waovu wangapi??

Ama kweli kanisani mnajipeleka ushahidi tu...mafundisho yanawapiga chenga sana!!
 
Pamoja na mapungufu ya Gwajima bado anao jamaa na rafiki wa hadhi mbalimbali.

Swala la kuumwa Gwajima ni lingine na Swala la kashfa dhidi ya Pengo ni tofauti.

Msishangae kesho Pengo akienda kumjulia hali gwajima.
 
Wakatoliki mmeanza mikwara na tisha toto. Mnaleta monopoly ktk siasa za Tanzania. Kumtembelea Gwajima ni siasa na Pengo nae ni mwanasiasa, ndio maana hakutaka kutumia busara ya kuongea hisia zake kwa wenzake, badala yake akawahukumu mbele ya waumini wao. Siasa za kutaka kulifurahisha kundi fulani ili ushinde sio endelevu. Tuleteeni siasa za kuwafurahisha watanzania wote, na sio vikundi.
 
kwa upuuzi wa pengo alistahili kabisa Yale matusi.Mimi ni mkatoliki na TEC ndiyo imetoa msimamo wa kanisa langu sio mpuuzi pengo
 
Hoja ya hapa sio kumsikiliza au kutomsikiliza Pengo.Hoja ni matusi dhidi ya Pengo na sympath ya wanasiasa kwa Gwajima.

Gwajima amesababisha mchanganyo wa kihisia kwa jamii ya kikatoliki na hivyo sio muda muafaka kwa viongozi wa kisiasa kuwa au kutokuwa upande wake kwa sasa.

kwa hio ulitaka mgonjwa asitembelewe?

Hata gaidi ana haki ya kuonwa akiwa mgonjwa.

Kama pengo ni mkristo kweli na amesamehe akamtembelee gwajima hospitali
 
hapo upo sawa hata mi mkatoliki sijafurahishwa na kitendo cha pengo kutukanwa n ukawa wajue wakatoliki ni wingi na wanasikiliza viongozi wao wa dini so wakifanya ujinga kwa hilo kweli watapoteza

mabadiliko yanapokuja hayaangali hadhi na nafasi ya mtu kwasababu wananchi wameshawajua viongozi wa dini nao hutumika kisiasa zaidi kwa kurubuniwa.jee pengo ametowa tamko juu ya marafiki zake walipopewa mgao wa escrow?
 
Gwajima kweli ni shujaa, mpiganaji, msemakweli bila kuogopa, bora ukamuacha kuliko kumchokoza binafsi nampenda na ni mfano wa kuigwa swala la kutumia maneno ambayo hata muhusika hayamuumi. It's shame kabisa.
Pengo ndie Mkuu wa Kanisa Katoliki kwa hapa Tanzania!. Anatokea mtu aliyekuwa Mkatoliki, akaasi na kuanzisha kijikanisa chake cha uchochoroni, kisha amtukane Mkuu wa Kanisa Katoliki, kisha anatokea memba mpya wa jf na kumsifu huyo mtukanaji kuwa ni shujaa!. Karibu jeiefu!.
Pasco
 
nani hajui kuwa pengo ni ccm damu damu wewe kama unataka kumfuata mawazo yake yafuate hata hvo rc si huwa mnawaabudu sana mapdre wenu utafkr ni Yesu hafu wanawambia mfuate anachosema siyo matendo yao.Zero in faith!!!!# " IMANI bila MATENDO IMEKUFA"
 
Yesu alitufundisha siyo tu kwenda kuwatazama wagonjwa kama Gwajima, bali hata wafungwa magerezani: MATHAYO 25:36,"....nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia."
 
Kwahiyo turudi kwa CCM kwavile tu UKAWA wameonyesha kumuunga mkono Gwanyima na CCM wameonekana kuwa kimya ktk hili sakata?Kwahiyo tuichague tena CCM inayolazimisha kutuletea katiba tusiyoitaka kisa Pengo?

Kama mnapanga kufanya hivi basi ndo itathibitika kwamba wengine mmepewa akili lkn zipo likizo ya muda mrefu usiojulikana,hata Mungu anawashangaa kwa kuamua kuabudu binadamu wenzenu na kuwafuata kwa upofu hata pale wanapowapotosha,mnajichimbia kaburi wenyewe wala hamtamkomoa Dr Slaa wala Prof Lipumba.
 
Mkuu usitufanye sisi ni watoto na hatujasikia kilichosemwa na Gwajima.

Ukawa wangejituliza vyumbani na kuacha jambo hili lipite kimya kimya.kumtembelea Gwajima ina maana mnakubaliana na yote aliyosema Gwajima kitu ambacho si sahihi.

Tusiwe wanafiki.

Sasa kama wote tumesikia si ni vyema kuacha kila mtu aamue kwa utashi wake kwa kupima alichosikia badala ya wewe kujipa mamlaka ya kuelekeza nini tumfanye huyo mtu.

Msikuze mambo wakuu,
Gwajima hana mgogoro na kanisa Katoliki!!
Acheni kununua porojo za kututoa kwenye hoja ya msingi.

Hoja ya msingi ni TAMKO LA KANISA.
 
Mnakuza mambo na kumuwekea maneno mdomoni mwa Mtu...
Wote tulimsikia Gwajima, akieleza kumuheshimu Ngalikumtwa.
Sasa huo ugomvi wa Catholic na Gwajima unatokea wapi??
Ngalikumtwa ni nani?

Mkuu hii thread yako imejaa hisia tu na hujaonyesha mashiko yoyote zaidi ya kutaka kutia hofu ambayo kimsingi haipo...
Unapaswa kutukanwa matusi yote yanayojulikana hapa duniani kwani nani hajasikia wakati gwajima anamtukana pengo kwenda zako na mhuni wako gwajima.
 
Back
Top Bottom