Binafsi kama Mtanzania wa kawaida kabisa nilichukizwa sana na maneno aliyoyaporomosha Gwajima dhidi ya Karidinali Pengo Kimsingi tu hata kama kweli Pengo angekuwa na makosa hakistahili matusi ya namna ile wote tunajua Gwajima ni mdogo sana kwa Karidinali Pengo na kwa desturi ya Kitanzania mkubwa wako akikukosea kuna namna ya kumweleza na siyo kuporomosha matusi kama aliyoporomosha Gwajima
Sasa tumesikia Kauli ya Pengo akisema amemsamehe Gwajima. ni jambo la kiungwana kabisa kwa hadhi ya Pengo alichokifanya ndio kilitakiwa kufanywa na muungwana yeyote yule nina Imani atakuwa amemsamehe kiroho safi kabisa na ni matumaini yangu Gwajima naye atafanya hivyo pindi akipata nafuu Mungu amsaidie apone upesi
Kuhusu Viongozi wa UKAWA Slaa na Lipumba kumtembelea Gwajima sioni kama kuna tatizo kama watakuwa wameenda kumsalimia Gwajima kama Kiongozi wa dini na Mtanzania pia ila Shida itakuwepo iwapo wamefanya hivyo kwa ajili kumsapoti Gwajima sababu ya kumpromoshea maneno Pengo ambaye Kimsingi wanaona kama hayuko upande wao kama watakuwa na mtazamo huo wajue qamepotea ila kama wameenda kumsalimia bila kuchukua upande wowote basi mimi sioni tatizo
Hawa Chadema na Cuf kwa style hii watakosa kura kwa wakatoliki kabisaa,hii njia wanayotumia itawapeleka pabaya hawaoni Ccm wamekauka kimya coz wanajua implication zake kwa jamii
Pengo ndie Mkuu wa Kanisa Katoliki kwa hapa Tanzania!. Anatokea mtu aliyekuwa Mkatoliki, akaasi na kuanzisha kijikanisa chake cha uchochoroni, kisha amtukane Mkuu wa Kanisa Katoliki, kisha anatokea memba mpya wa jf na kumsifu huyo mtukanaji kuwa ni shujaa!. Karibu jeiefu!.
Pasco
Wewe nae sijui unafikiri kwa kutumia nini,kumtembelea mgonjwa hospitalini ina maana kuwa unakubaliana na yote aliyoyasema??ndugu yako akikamatwa ugoni akajeruhiwa hutaenda kumsabahi hospital?na ukienda ina maana unakubaliana na ugoni?.Think big kijanaMkuu usitufanye sisi ni watoto na hatujasikia kilichosemwa na Gwajima.
Ukawa wangejituliza vyumbani na kuacha jambo hili lipite kimya kimya.kumtembelea Gwajima ina maana mnakubaliana na yote aliyosema Gwajima kitu ambacho si sahihi.
Tusiwe wanafiki.
Si makosa hata kidogo kujuliana hali.Lipumba au Slaa hajakatazwa kumjulia hali ila kwa wadhifa wao na hali ya mambo ilivyo haikuwa sahihi na haitakuwa sahihi kumjulia hali mtu aliyeropoka matusi hadharani tena dhidi ya kiongozi mkuu wa kanisa hapa nchini.Wewe nae sijui unafikiri kwa kutumia nini,kumtembelea mgonjwa hospitalini ina maana kuwa unakubaliana na yote aliyoyasema??ndugu yako akikamatwa ugoni akajeruhiwa hutaenda kumsabahi hospital?na ukienda ina maana unakubaliana na ugoni?.Think big kijana
Hapo upo sawa hata mi mkatoliki sijafurahishwa na kitendo cha pengo kutukanwa n ukawa wajue wakatoliki ni wingi na wanasikiliza viongozi wao wa dini so wakifanya ujinga kwa hilo kweli watapoteza
Kanisa Katoliki linaongozwa kwa majimbo, ambapo Jimbo Kuu la Dar es Salaam ndilo linaloongoza ikiwemo ku host Baraza La Maaskofu Katoliki pale Kurasini, na kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ni Muadhama Polcarp Karninali Pengo, akisaidiwa na maaskofu wawili wasaidizi.Pasco kwa hierachy gani Pengo ni mkuu wa kanisa katoliki Tanzania?
Nani anaripoti kwa Pengo zaidi ya Maaskofu na Mapadri wa Jimboni kwake Dar es Salaam?
Pasco usiwe mpotoshaji ...alafu unayo hii habit
Najitambulisha kama mkatoliki kindakindaki...na sio mara ya kwanza kufanya hivi.niliwahi kufanya hivi hapo awali na nilimtuhumu Askofu Pengo kwa tamko lake kuhusiana na mashambulizi dhidi ya mapadre wetu.inawezekana kipindi kile sikumuelewa Kadinali Pengo...nilikurupuka kumtuhumu kama alivyokurupuka Gwajima.
Nilimtuhumu kwa kupingana na msimamo wa wengi dhidi ya nani muhusika wa mashambulizi yale.nilimtuhumu kwa kutoelekeza wakatoliki tufanye nini dhidi ya ufirauni waliofanyiwa mapadre na waumini wa Kanisa katoliki,nilikasirika na kumuona ni msaliti na anasimama na serikali inayotuudhi!
Mambo yalivyoendelea nilijikuta naanza kuelewa zaidi kauli za kadinali Pengo na kuziona ni sahihi na zinazingatia ukweli au uchunguzi wa mambo.
Ndio maana kwa kauli hii ya juzi sikutaka kukurupuka.
Nimeanzisha thread zipatazo mbili kuhusu sakata na kauli ya hivi karibuni ya kadinali Pengo lengo ni kujua uhalisia na ukweli wa kile alichokisema Askofu Pengo..zote zimeishia kapuni.
madhumuni ya uzi huu ni kuwatahadharisha Ukawa juu ya kukurupuka!
Nawasihi na kuwatahadharisha Ukawa juu ya kumdharau Pengo kisa porojo na matusi ya Gwajima.
Nawatahadharisha Ukawa kutojifungamanisha na Gwajima mtu ambaye amewakosea adabu wakatoliki ...hakuna mkatoliki anayefurahishwa na matusi dhidi ya Kadinali Pengo na haitatokea kamwe hata kama angeshikwa ugoni!
Ukawa jihadharini sana!hapa ndipo mtakapopoteza!
Nawasilisha kwa uchungu!
Pengo ndie Mkuu wa Kanisa Katoliki kwa hapa Tanzania!. Anatokea mtu aliyekuwa Mkatoliki, akaasi na kuanzisha kijikanisa chake cha uchochoroni, kisha amtukane Mkuu wa Kanisa Katoliki, kisha anatokea memba mpya wa jf na kumsifu huyo mtukanaji kuwa ni shujaa!. Karibu jeiefu!.
Pasco
Kanisa Katoliki linaongozwa kwa majimbo, ambapo Jimbo Kuu la Dar es Salaam ndilo linaloongoza ikiwemo ku host Baraza La Maaskofu Katoliki pale Kurasini, na kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ni Muadhama Polcarp Karninali Pengo, akisaidiwa na maaskofu wawili wasaidizi.
Hivi ndivyo mimi nijuavyo toka enzi za Muadhama Laurian, Kardinari Rugambwa ndio mkuu wa Kanisa akifuatiwa na Wahashamu Maaskofu wa majimbo mbalimbali.
Ni huyu pekee anayekwenda Rome kumchagua Papa na ndiye pekee mwenye daraja ya kuweza kuwa Papa.
Pasco.
Hapo upo sawa hata mi mkatoliki sijafurahishwa na kitendo cha pengo kutukanwa n ukawa wajue wakatoliki ni wingi na wanasikiliza viongozi wao wa dini so wakifanya ujinga kwa hilo kweli watapoteza
Acha uchonganishi wewe! Side wakatoliki tunapenda wema na upendo, ningekuelewa ungemuomba mhashamu amtembelee gwajima hospital na sio kutaka watu wasiende kumuona! Nawaomba wakatoliki wenzangu tumuombee afya njema gwajima, kazi ya kuhukumu watu sio yetu. Mungu halali anaona kila kitu. Amri kuu kuliko zote ni upendo, natamani kumsikia gwajima mahubiri yake punde tu akiwa na afya yake, long live gwajima. Tutetee kondoo wa bwana.
Mnakuza mambo na kumuwekea maneno mdomoni mwa Mtu...
Wote tulimsikia Gwajima, akieleza kumuheshimu Ngalikumtwa.
Sasa huo ugomvi wa Catholic na Gwajima unatokea wapi??
Ngalikumtwa ni nani?
Mkuu hii thread yako imejaa hisia tu na hujaonyesha mashiko yoyote zaidi ya kutaka kutia hofu ambayo kimsingi haipo...
Kanisa Katoliki linaongozwa kwa majimbo, ambapo Jimbo Kuu la Dar es Salaam ndilo linaloongoza ikiwemo ku host Baraza La Maaskofu Katoliki pale Kurasini, na kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki ni Muadhama Polcarp Karninali Pengo, akisaidiwa na maaskofu wawili wasaidizi.
Hivi ndivyo mimi nijuavyo toka enzi za Muadhama Laurian, Kardinari Rugambwa ndio mkuu wa Kanisa akifuatiwa na Wahashamu Maaskofu wa majimbo mbalimbali.
Ni huyu pekee anayekwenda Rome kumchagua Papa na ndiye pekee mwenye daraja ya kuweza kuwa Papa.
Pasco.