Iweje ng'ombe auzwe kwa bei inayozidi ya gari la kifahari?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,694
6,396
Ukiwa na bilioni tatu, utanunua gari lipi la kifahari?

V8?
Range Rover?
Mercedes Benz S Class?

Nimeyataja hayo magari kwa kuwa ninayapenda. Na kama wewe ni mpenzi wa magari tajwa kama mimi, unaweza kuyapata yote ukiwa na bilioni tatu, na bado ukabakiwa na chenchi.

Kama kwa hela hiyo unaweza kununua hayo magari yote, inamaanisha kuna ng'ombe wenye thamani kubwa kuzidi magari kadhaa ya kifahari.

Mwaka 2019, ng'ombe dume
nchini Marekani aliuzwa kwa dola za Kimarekani 1.5 million, sawa na zaidi ya bilioni tatu hela ya Tanzania.

Mwaka 2023, ng'ombe mmoja aliuzwa nchini Brazil kwa Real 6.99m. Kwa hela ya Tanzania, hiyo ni sawa na zaidi ya bilioni tatu na nusu.

Mwezi June 2023, ng'ombe wa Kinyankole aliuzwa kwa Rand 1.65m nchini Afrika Kusini. Kwa Tanzania hiyo ni zaidi ya bilioni mbili.

Hao ng'ombe wana nini cha kipekee hata wauzwe kubwa Kaisi hicho? Bei ya ng'ombe inaizidi bei ya V8 mpya? Hilo linawezekanaje?
 
Ukiwa na bilioni tatu, utanunua gari lipi la kifahari?

V8?
Range Rover?
Mercedes Benz S Class?

Nimeyatajia hayo magari kwa kuwa ninayapenda. Na kama wewe ni mpenzi wa magari tajwa kama mimi, unaweza kuyapata yote ukiwa na bilioni tatu, na bado ukabakiwa na chenchi.

Kama kwa hela hiyo unaweza kununua hayo magari hotel, inamaanisha kuna ng'ombe wenye thamani kubwa kuzidi magari kadhaa ya kifahari.

Mwaka 2019, ng'ombe dume la nchini Marekani aliuzwa kwa dola za Kimarekani 1.5 million, sawa na zaidi ya bilioni tatu hela ya Tanzania.

Mwaka 2023, ng'ombe mmoja aliuzwa nchini Brazil kwa Real 6.99. Kwa hela ya Tanzania, hiyo ni sawa na zaidi ya bilioni tatu na nusu.

Mwezi June 2023, ng'ombe wa Kinyankole aliuzwa kwa Rand 1.65m nchini Afrika Kusini. Kwa Tanzania hiyo ni zaidi ya bilioni mbili.

Hao ng'ombe wana nini cha kipekee hata wauzwe kubwa Kaisi hicho? Bei ya ng'ombe inaizidi bei ya V8 mpya? Hilo linawezekanaje?
Wengi huwa wanatumiwa kuzalisha mbegu. Ng'ombe wa kuzalishia mbegu wanakuwa w kipekee na wanafugwa kwa upekee
 
Wengi huwa wanatumiwa kuzalisha mbegu. Ng'ombe wa kuzalishia mbegu wanakuwa w kipekee na wanafugwa kwa upekee
Labda, kwa sababu sidhani kama ni kwa matumizi ya kawaida kama maziwa na nyama. Lazima wana matumizi ya kipekee.
 
Back
Top Bottom