Ukabila utawaangamiza UDART (Mwendokasi)

Ukabila utawaangamiza UDART (Mwendokasi)

Mtoa Post Nafikili Ni Mhanga Wa Kukosa Ajira Pia Sio Msukuma , Hv Nikuulize We Ungekua Msukuma Ukipewa Kaz Pale Utakataa , , , Pole Bna Ajira Zitatoka Huu Mwaka Wa Neema
 
Hivi Huyu [HASHTAG]#Archbishop[/HASHTAG] Kinacho kukera Ni Huduma unayo tolewa au unakerwa na lugha inayo tumiwa na Wafanyakazi wa UDART...
Kwa sababu Kama Ni kilugha maranyingi wanaongea wakiwa peke yao ,Lakini mteja anahudumiwa Kwa lugha ya Kiswahil ......huo ulionao na upofu wa fikra.... Pale Hakuna ukabila
 
Dhamu yao wasukuma sasa kuneemeka. Mshazoea makabila yale yale kila kona. Muache na wenyewe waingie Serikalini, uzuri wa wasukuma sio wezi sana kama makabila mengine
 
Pole Kiongozi lakini rekebisha maneno haya chini yenye rangi nyekundu yasomeke fasaha kama ilivyorekibishwa.
kutuudumia == kutuhudumia

unamirikiwa == unamilikiwa
selikari, == serikali

ukabira= = ukabila

rakini == lakini
wamiriki= = wamiliki.
Umekuwa ikivubhu sio kwa umakini huo
 
Ndugu wana JF, niwatakie kheri ya Mwaka mpya 2018.

Kwanza kabisa niwapongeze walioshiriki katika ununuzi wa mabasi haya, ninawapongeza kwa sababu ni magari yenye injini za uhakika(Cummins) tena Euro four ambazo ni environmental friend. Mbali na hizo engine gari hizi zina gear box za Voith, wanaojua magari watanielewa.

Itakapofika mwezi wa Tano mwaka huu, mradi huu wa mwendo kasi utakuwa umefikisha miaka miwili kutuhudumia wananchi. Ikumbukwe mradi huu unamilikiwa asilimia zaidi ya 50 na Robert Kisena(SIMON GROUP), asilimia 10 umoja wa wamiliki daladala na zinazobaki ni serikali, kwa kigezo icho hapo juu, Kisena anapata mamlaka ya kuamua nani amuweke kwenye management na nani amwajiri, Pia anapata upenyo wakutoweza kuwa audited.

Kinachonipa ukakasi nijinsi alivyoamua kuuendesha mradi huu, katanguliza ukabila mbele, ukifika Kurasini kwenye ofisi za Simon Group ni kisukuma kuanzia getini mpaka ghorofani,

Ukija Jangwani ni kisukuma kuanzia getini, madereva, workshop, stores mpaka kwenye management. Jambo hili wala nisingeona tatizo kama angeweka wasukuma lakini walio makini, lakini kajaza watu wasiojua nini wanafanya, wanangojea kila kitu yeye atoe maelezo muda wote wanagonga kisukuma ofisini.

Wapo watu ambao hawafai kuwa hata supervisors lakini unakuta wanaitwa C.E.O

Jambo la mwisho linaloleta ukakasi ni, jinsi alivyoamua kuanzisha vikampuni ndani ya mradi kwa ajili yakuwaibia wadau wenzake ambao ni wamiliki wa daladala na serikali.(Jambo hili liko sensitive sana sitaliweka hapa mpaka hapo baadae.)
Zamu Yao hii tutulie tu
 
Acha wivu na wewe ongea lugha yako?
Kiswahili ndio lugha ya taifa, nakumbuka baba wa taifa alisema panakuwa na makabila tofauti hususani maeneo ya mijini ni marufuku kuongea lugha za kwenu huko kijijini
 
Hawa jamaa Wanahitaji mshindani "competitor, ". Maana naona wanaamua tu kufungia magari jangwani wakati watu wanapata shida ya usafiri.

Nakumbuka mvua iliwaumbua vibaya pale gari zaidi ya 40 ziliingia maji zikiwa zimepakiwa tu jangwani.


Ukitaka watu wawe serious na kazi watafutie mshindani Ili wajue kupata pesa sio lelemama
 
Sasa wao walijuaje kama hao ni wasukuma wenzao had wakawapa kaz
Saili zinafanyika kma formality tu kuonyesha taratibu zilifuatwa Ila uhalisia tayari wanakuwa wameshawaweka watu wao au hao watu unakuwa nao kwenye michakto but wakiwa wanajua kili kitu nikimaanisha maswali na mjbu. Nafikiri umenielewa kma bdo suburi shule zifunguliwe uje darasn
 
Back
Top Bottom