UDART: Tunaleta heshima ya usafiri wa umma Dar es Salaam

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameelekeza ije mvua liwake jua, mradi wa mabasi ya mwendo kasi lazima uanze Januari 10, 2016. Raia Mwema, limefanya mahojiano na Mwenyekiti wa Kampuni za Simon Group, Robert Kisena, ambao ni wanahisa wa UDART, kampuni yenye jukumu la kutoa hudma ya usafiri huo wa mabasi ya mwendo kasi, pamoja na mambo mengine anazungumzia uwezekano wa mradi huo kuanza kama ilivyoelekezwa na Waziri Mkuu.

Raia Mwema: Ziara ya Waziri Mkuu kwenye mradi wa Mabasi yaendayo kasi imeongeza msukumo gani katika kuharakisha kuanza kwa mradi huo?
Kisena: Kwanza tumefurahi sana kwa ziara hiyo. Hii inaonyesha sasa kwamba serikali imeupa kipaumbele mradi huu, maana yake kiongozi wa nchi kama Waziri Mkuu anapofuatilia jambo kwa karibu kama alivyofanya kwenye mradi huu wa DART inatia moyo, na ni dalili ya wazi kuwa mradi huu sasa unakwenda kuanza na wananchi wategemee ufanisi mkubwa.

Raia Mwema: Kutembelewa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano, si jambo ambalo watu wengi wanaliomba, wewe unasema umefurahi, nini msingi wa furaha hiyo?

Kisena: Tumefurahi kwa sababu sisi ni wadau muhimu katika mradi huu. Kwenye mradi wa DART kuna mambo mawili makubwa, la kwanza ambalo ndiyo msingi ni miundombinu ya barabara na vituo vya mabasi na jingine kubwa ni mabasi yenyewe. Kwenye haya mawili sisi tunahusika na mabasi, ambayo tayari yapo mabasi 140. Tulichokuwa tunasubiri ni msukomo wa serikali kwa maana ya kukamilisha barabara na vituo viwe tayari kutumika ili mabasi yaanze kufanya kazi kwa upande wetu hatukuwa na mashaka tumekamilisha kila kitu.


Raia Mwema: Awali mradi huu ulipangwa kuanza Mwezi Novemba, 201, tukaambiwa maandalizi yamekamilika kama inavyosemwa sasa, wananchi wana sababu gani za kuamini kwamba Januari 10, mwakani mradi utaanza?

Kisena: Sasa hivi mradi umefikia asilimia 99 kuweza kukamilika vimebaki vitu vichache sana. Kumbuka hii siyo mara ya kwanza Waziri Mkuu kutuita wadau wa mradi huu. Mara bada ya kuapishwa Dodoma moja ya kazi zake za kwanza ilikuwa ni kutaka maeelezo juu ya maendeleo ya mradi wa DART. Tuliitwa wadau wote, tukahudhuria kwake akatoa ultimatum ya kwanza pale kwamba mradi uwe umeanza ifikapo tarehe Januari 10, 2016.

Hii ziara yake ya wiki jana ilikuwa ni ufuatiliaji maelekezo yake tumefikia wapi, lakini pia umemhusisha Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Mwanzoni tulipokutana changamoto ilikuwa iko kwenye vituo, sasa kaamua kwennda kujionea mwenyewe pamoja na Waziri wa TAMISEMI, na sisi kama wadau (pamoja na Tanroads, Strabag na DART) tumedhamiria kwa dhati na kwa msukomo huo wa serikali, Januari 10 mabasi ya mwendo kasi yatakuwa barabarani.


Raia Mwema: UDA - RT mmewaandaje wananchi kuanza mfumo huu mpya wa usafiri jijini?

Kisena: Baada ya maandalizi ya vituo kukamilika, tunaanza kufunga mfumo wa utozaji nauli, mfumo wenyewe upo tayari, wiki hii umeanza kufungwa katika vituo ambavyo vimekamilika. Utakapokamilika mfumo huo kabla ya kuanza rasmi mradi tutakuwa na maeneo yaliyochaguliwa ya kuonyesha namna mfumo huu unavyofanya kazi, ambayo yatahusika pia na utoaji wa elimu kwa umma kuhusu namna ya kutumia vituo, namna ya kulipa nauli na jinsi ya kuyatumia mabasi. Nategema wananchi watafurahi na watakuwa wepesi kuuelewa kwa sababu ni mfumo bora na rahisi kuutumia.


Raia Mwema: Hali ya ubora wa mabasi ikoje?

Kisena: Watu wengi wanaamini kuwa vitu kutoka China vyote ni ?feki? siyo kweli. China vinatoka vitu bora kabisa kuliko hata vitu vingine vya Ulaya lakini pia vinatoka vitu duni kabisa, tofauti ni namna wewe unavyotaka. Kwa mabasi haya kampuni inayotuuzia sisi wao wanaunganisha tu mabasi haya (assembling) lakini vifaa vyake muhimu kama injini, gia box, diff na mfumo wa breki vinanunuliwa kutoka sehemu mbali mbali.

Injini zetu sisi ni Kemix engine, ni injini bora kabisa zinazotengenezwa na kampuni ya Kimarekani inayoongoza duniani kwa kutengeneza injini za magari makubwa, upande wa diff za mabasi yetu zinazotengenezwa Ujerumani na tuna mkataba na makampuni haya moja kwa moja, msaada wa kifundi wa mabasi haya utafanyika moja kwa moja na makampuni haya. Mabasi haya ni bora kabisa kwa viwango vya nchi zilizoendelea nawaomba tu Watanzania wayatumie vizuri.


Raia Mwema: Serikali kwa maana ya Wizara ya TAMISEMI wanawapa ushirikiano wa kiwango gani?

Kisena: Waziri wa TAMISEMI kwa kweli amehamasika sana kuhusu mradi, baada ya mazungumzo na Waziri Mkuu wiki jana, tulikwenda ofisini kwake kufanya majumuisho na akaagiza inyeshe mvua au lije jua lazima mabasi yaingie barabarani Januari 10 mwakani 2016. Hata kama kuna mambo fulani fulani yanakwamisha yasiruhusiwe kurudisha nyuma dhamira njema ya serikali. Kwa hiyo wizara wako makini kabisa na hii imetupa faraja sisi kwamba mradi huu sasa unakwenda kuanza.


Raia Mwema: Mradi ukishaanza utakuwa na mchango gani chanya kwa taifa?

Kisena: Foleni hizi kwa sasa tunaambiwa zinalifanya taifa kupoteza takribani shilingi bilioni 4 kwa siku. Sisi tunachokwenda kupeleka kwa wananchi katika mradi huu wa BRT ni speed na convenience (kasi na urahisi) ya kusafiri. Kwa hiyo wananchi watakuja kununua kasi lakini kwenye mabasi yetu pia watakuja kununua urahisi, watafiri bila bughudha, muda wa saa mbili ambao walikuwa wanautumia kutoka Kimara kwenda Posta na Kivukoni sasa watatumia dakika 40 tu, hapo mtu anaokoa saa moja na dakika 20, na utakuwa usafiri wa kuaminika, kutumianiwa na usio na bughudha.

Kwa hiyo tunatumaini wananchi wataacha kutumia magari ya binafsi watatumia mabasi yetu. Kwa kuwa mradi huu unaanza kwa sehemu tu ya Dar es Salaam (Kimara mpaka Kivukoni) ninaamini tutasaidia kuoko sehemu ya pesa hiyo inayopotea kila siku kutokana na foleni. Kwa mfano tukiokoa shilingi bilioni moja, hiyo itakwenda kwenye maeneo mengine ya kuinua uchumi lakini pia hata vipato vya watu binafsi vitaongezeka kwa sababu wale wanaotumia magari yao wanatumia sehemu kubwa ya vipato vyao kwenye mafuta, kukarabati gari, ile disposable income (pato la mtu baada kukatwa kodi) inapungua, mabasi haya yatapunguza hilo.


Raia Mwema: Mabasi mangapi yataigia barabarani mradi utakapoanza hiyo Januari 10?

Kisena: Tutaanza na mabasi yote 140 ili kuondoa usubufu kwa abiria, kama nilivyosema, tunapeleka wepesi wa kusafiri na kasi, tukianza na machache tunaweza kutengeneza mgogoro wa usafiri, ili kuondoa hiyo mabasi yetu yote yaanze kwa pamoja.


Raia Mwema: Utaratibu wa mabasi haya utakuwaje, kwa mfano yatakaa kituoni muda gani?

Kisena: Yatakaa kituoni kwa muda wa dakika mbili tu. Mfumo wetu utakuwa unatumia kadi, badala ya watu kupanga foleni na kulipa nauli mara uanze kutafuta chenji, huo usumbufu wote hautakuwepo. Mtu anakuja na kadi yake anaingia safari inaendelea.


Raia Mwema: Hizi kadi zitakuwa zinapatikanaje?

Kisena: Kadi hizi zitauzwa kwa wananchi, ni kadi ngumu ya kudumu kama zilivyo kadi za benki. Zitafanya kazi kama kadi zinazotumika maofisini kufungua milango kwa ?kuchanja?, hizi zitakuwa zinatumika kwenye geti za vituo. Tutakuwa na sehemu mbali mbali za kuuzia. Mtu akiwa na kadi hiyo anakuwa anajaza pesa (recharging) kutumia mitandao ya M pesa, Airtel Money, au Tigo pesa kwenda kwenye kadi yako, kwa hiyo kila inapoishiwa unaijaza na unaedelea hivyo hivyo. Kadi hizi tutaziuza siyo kwa bei ya faida, tutauza kwa bei tuliyonunulia (cost price) na mtu akiituza anaweza kukaa nayo hata kwa miaka mitano.


Raia Mwema: Wananchi wana wajibu gani katika mabadiliko haya?

Kisena: Niseme kwamba mradi huu ni wa wananchi. umeletwa na serikali kwa ajili ya wananchi, kwa hiyo waupende na kuutunza kwa sababu ni wa kwao na unakuja kusaiidia maisha yao.

Mabasi haya ni ya wananchi, na kwa kuwa katika kila kitu lazima kuwe na mtu anayesimamia na kuendesha, sisi waendeshaji tumeyaleta haya kwa niaba ya wananchi, tumepewa jukumu hilo tukayaleta, ni jukumu lao kuyatumia vizuri ili hata vizazi vijavyo viweze kunufaika na huu mradi. Mradi huu utakapokamilika utahusisha mabasi 350, baada tu ya mawamu ya kwanza ya mradi kuanza tutaanza mchakato wa kuagiza mabasi mengine 210 ya mwendo kasi yaliyobaki, katika hili utaona ni kwa namna gani uwekezaji huu utakuwa na manufaa kwa wananchi.

Raia Mwema
 
Waone tu waswahili wanayataka yaje lakini ukianza tu utaona watavyoyafanya haya magari ..sisi hatuna uzalendo wa kuthamini vitu vyetu watanzania
 
Hizo barabara mlivyozibomoa bomoa! Michoro haijulikani. sehemu za U - turn bado hazina alama. Najua mtalipua lipua muanze lakini badooo sana sio barabara tuliyoitegemea. Hata maeneo ya kuvukia ndio yanaonyeshwa sasa kwa kuvunja vunja. uKWELI badoooo.

Tuambieni daladala mwisho lini kuonekana barabarani
 
Hakuna haja kuhojiana na wezi wa mali ya umma.
Wanataka kuhalalisha ujambazi waliofanya wa kunyakua shirika la umma na kujimilikisha mali zake kifisadi ili waweze kufanyia biashara miundombinu iliyojengwa pia kwa fedha za umma.
They are just criminals.
Serikali ya awamu ya tano inatakiwa kuchukua hatua bila kuchelewa juu ya hii habari ya UDA.
Kuna habari pia kwamba wameingiza hayo mabasi bila kulipia ushuru kama vile ni ya serikali wakati ni mradi binafsi wa kibiashara.
 
Hakuna haja kuhojiana na wezi wa mali ya umma.
Wanataka kuhalalisha ujambazi waliofanya wa kunyakua shirika la umma na kujimilikisha mali zake kifisadi ili waweze kufanyia biashara miundombinu iliyojengwa pia kwa fedha za umma.
They are just criminals.
Serikali ya awamu ya tano inatakiwa kuchukua hatua bila kuchelewa juu ya hii habari ya UDA.
Kuna habari pia kwamba wameingiza hayo mabasi bila kulipia ushuru kama vile ni ya serikali wakati ni mradi binafsi wa kibiashara.

Mkuu umefikiri sawa na mimi. Iweje hawa tunaowalalamikia kupata kampni ya umma kwa njia ya wizi leo tuwapatie tena mradi mwingine wa umma, uliojengwa kwa fedha za umma?. Je ni mradi sahihi? tatizola dar ni magari kukosa mwendo au kasi kama ambavyo tunataka kuaminishwa?
 
Hakuna haja kuhojiana na wezi wa mali ya umma.
Wanataka kuhalalisha ujambazi waliofanya wa kunyakua shirika la umma na kujimilikisha mali zake kifisadi ili waweze kufanyia biashara miundombinu iliyojengwa pia kwa fedha za umma.
They are just criminals.
Serikali ya awamu ya tano inatakiwa kuchukua hatua bila kuchelewa juu ya hii habari ya UDA.
Kuna habari pia kwamba wameingiza hayo mabasi bila kulipia ushuru kama vile ni ya serikali wakati ni mradi binafsi wa kibiashara.

Imekaa kiuchunguzi uchunguzi zaidi hii. Hebu wenye ujuzi wa mambo ya habari za kiuchunguzi fanyieni kazi hili hasa la kutumia mradi wa umma kujinufaisha na piua kukwepa kulipia kodi alhali ni mradi binafsi...
 
Back
Top Bottom