Maoni Ushauri na Mapendekezo kwa mabasi ya mwendo kasi (DART): Nini changamoto, nini umefurahia?

Al-shabaab

JF-Expert Member
Aug 24, 2013
1,791
619
1462878637380-jpg.346324
Habari wanajamvi.
leo ndo siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu sana na wakazi wa DAR kuanza kutumia mradi huu wa mabasi. Jumanne na kesho jumatano itakua bure kusafiri.tupeane updates za mabasi hayo hapa
Habari za asubuhi wakuu?

Ninapenda kuwashirikisha jambo ambalo limenitokea leo wakati naelekea kibaruani. Siku tatu zilizopita hawa jamaa wa Dar es Salaam Rapid Transport (DRT) walianza kuuza kadi ambazo wateja wanatumia badala ya tiketi ambazo zimekuwa zikitumika tangu kuanza kwa mradi.

Leo nikiwa njiani kuelekea kibaruani nilishukia kituo cha Nyerere square, karibu na kanisa la St. Joseph mjini kati kisha nikasema wacha nimuone mhudumu ili anitazamie na pia kuniongezea balansi ktk kadi yangu. Mbele yangu kulikuwa na wateja wengine wawili ambao walikuwa na lengo hilo hilo. Baada ya wale kuhudumiwa, ikafika zamu yangu. Nilipompatia pesa, akaniuliza iwapo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuweka pesa ktk kadi, nikamjibu ndio. Alirudia swali hilo mara tatu mpaka nikakereka. Baadae aka print risiti ya kwanza akataka kunipa lakini akaiweka pembeni kisha akaprint nyingine akasema hiyo ni ya kuonyesha pesa imeingia. Nikaipokea na kuiangalia lakini sikuona kama kuna kiasi cha shilingi 10,000 kimeandikwa popote.

Nikaamua kwenda kituo cha jirani ili kuomba kujua balansi katika kadi yangu. Cha kushangaza nikakuta balansi ni shilingi 1.250 tu. Ikabidi nirudi kwenda tena kwa yule mhudumu wa awali. Nikamuuliza kama ananikumbuka akakiri. Nikamwambia mbona nimeangalia kupitia mhudumu wa kituo kingine na inaonyesha pesa haijaingia? Akaniambia oops samahani nlidhani nilikupa risiti ambayo sio licha ya kuiprinti. Akasema alishaichana na hiyo ndio ilikuwa na ile pesa niliyoweka hapo awali. Akaomba tena kadi yangu kisha akaprinti na kunipa risiti mbili, moja ya kuwekewa ile 10,000 na nyingine ya kuonyesha balansi ya 11,250.

Angalizo kwa watumiaji wa huduma hii ni kwamba tunapaswa kuwa makini maana baadhi ya wahudumu hawa kama huyu niliyemkuta hapa wana take advantage ya ugeni wa huduma hii kujinufaisha kwa kuwaibia wateja. Nina imani huenda ameshawafanyia wateja wengi wizi wa namna hii. Wewe mteja hakikisha unapata risiti kwa pesa yoyote ambayo umelipia huduma na ionyeshe kiasi cha pesa uliyolipa.

Leo ilitangazwa kuwa tarehe rasmi ya kuanza kwa mabasi ya mwendokasi jijini Dar es Salaam. Nimeambiwa kuwa,hadi muda huu hakuna hata basi moja la DART lililoanza kazi. Ilitangazwa yangeanza alfajiri. Wengine,akina Kisena,wakasema yataanza saa nne.

Nimearifiwa kuwa kuna fukuto lisilo na mvuto kati ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Kampuni ya Simon Group inayodai kumiliki asilimia 51 ya hisa za UDA,mdau mmojawapo wa DART. Jiji linadai Simon Group hana hisa zozote na hivyo hawana mamlaka ya kujihusisha na DART.

Wananchi,huko Dar,wamekusanyika kwenye vituo vya DART huku daladala zikipaki. Hawana usafiri wa kwenda wala kurudi kazini. DART inatesa wananchi wanaopaswa kuhudumiwa!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Ruvuma)

Kwa taarifa niliyoipata sasa hivi ni Mabus ya mwendo kasi yamenza kazi rasmi.

View attachment 346284View attachment 346285

Kwanza napongeza wazo la kuanzisha mradi huu ila pamekuwa na hasara kadhaa kutokana na mradi huu. Mimi nikiwa mmoja wa wamiliki wa vyombo vya kubeba abiria leo nitazungumza machache kwakuwa nimepata muda wa kupanda gari hizi.

Kwanza Tanzania haikuwa tayari au haikujizatiti haswa kwenye mradi huu kwa kuzingatia kwamba abiria wanaohitaji usafiri ni wengi mno kiasi kwamba magari ya mwendo kasi pekee hayatoshi.

Huu imeongezaka ugumu zaidi pindi gari za Kibaha zilipozuiliwa kufika Mawasiliano huku serikali ikitambua kuwa hata kabla ya mwendokasi kuanza Mbezi inaongoza kutoa abiria wengi ambao wengi wao wanatokea Mlandizi na Kibaha. Hivyo abiria anaepanda daladala Mbezi alikua na uhakika wa kufika Mawasiliano kwa 400tsh, lakini mara baada ya hizi daladala kuondolewa inamlazimu abiria anayetoka Maramba mawili atumie 1000 tsh ya bajaji hadi afike Mbezi kisha alipe nauli mwendokasi ambayo itamfikisha hadi Kimara akifika Kimara alipe tena 650 tsh hadi Ubungo ndipo atembee kwa mguu kutoka Ubungo terminal hadi darajani au mawasiliano (mtacalculate huo mzunguko wa nauli kwa go and return).

Sasa abiria huyu anapofika Mbezi inambidi apange msululu wa foleni ili akate ticketi kisha akifika hapo anaenda tena kupanga limsululu la foleni ya kusubiri mwendokasi huku muda mwingine inafika hadi dakika 30 bila gari kutokea. Na hata ikija inakuja moja tu hivyo abiria wanajaa mno kupindukia na vile madirisha ya gari hizi ni madogo kama jela hapo utapata picha humo ndani.

Saa nyingine umefika Kimara unapanga foleni nyingine ndefu ya kukata tiketi hapa utamaliza saa nzima hadi ukifika dirishani utaambiwa kadi au ticket zimeisha asubiri kuna mtu kazifuata. Hatimaye unapata ticketi mnajazana kwenye gari utafikiri mnapanda bure. Hapo bado hujakutana na wadada wahudumu wa vituo hivi wanavyobinua midomo sasa.

Nafikiri bado daladala zilikua zina umuhimu mkubwa na sio serikali kuzisimamisha ghafla bila kuangalia wamejipanga vipi. Pia napongeza japokuwa abiria hujaa sana kama DCM za Gongo la Mboto na Mbagala ila sasa kutoka Kariakoo hadi Kimara ni almost one hour japokuwa hata hizi daladala zingine nazo hutumia saa moja hiyohiyo.

View attachment 411455 View attachment 411459
1. Toka zianze kufanya kazi sijawahi kuona zile TV zikiwaka, sasa sijui ni urembo ama nini.

2. Hazina mfumo wa Air Condition(AC), nadhani hawakuzingatia hali ya hewa ya DSM .

3. Speed Limit. Nadhani kiwango cha mwisho cha kutembea ni 45km/hr, ukizidisha yanapiga alarm. Sasa sielewi mantiki kamili ya mwendokasi. Hii inaenda sambamba na basi kuchelewa kwenye vituo.
Mradi wa Mwendokasi bado una kero nyingi za msingi.

Tusitake kila kitu mpaka Mh Rais au Waziri Mkuu aongee ndio tuamke. Ni vema tuache mazoea. Viongozi wa mradi msiishie kukaa maofisini, ingieni field muone uhalisia ili malengo ya mradi yafanikiwe.

Mpaka sasa bado mtu anayeamua kutumia daladala kutoka Kimara kwenda Mjini anaweza kuwahi kuliko mtu anayetumia UDART.

Mtu anayetumia UDART anapoteza muda mwingi sana kusubiri gari kutokana na msongamano vituoni hasa kimara mida ya asubuhi na mjini mida ya alasiri.

Kimsingi baadhi ya dosari nilizoziona ktk uendeshaji wa mradi huu ni ;
1. Utaratibu mbovu wa kuregulate idadi ya magari jambo linalopelekea misongamano ya abiria vituoni.
Kuna mida magari yanarudishwa yard kwa kuangalia wingi wa abiria. Hili mbali ya kusababisha msongamano lkn linapoteza fursa ya kukuza mapato ya mradi. Ni sahihi kuregulate magari, lakini yasipungue mpaka ikawa kero kwa abiria. Mnapoteza potential customers, mnaondoa fursa ya kukua, mnadumaza mradi na kuongeza kero.
Ni vema mkajua kwamba kadri mnayoachia magari mengi ndivyo mnavyoongeza fursa ya kukuza mapato kadri siku zinavyoenda.
Msiwe kama daladala wanaotaka faida ya papohapo.
Kuweni strategic.
Muda wanaopoteza abiria vituoni ni hasara kwa mradi, hasara kwa abiria na hasara kwa taifa.

2. Hamjaweka mfumo wa mteja kujua salio la kadi yake. Mtu anaweza panga foleni muda mrefu na kuishia kuumbuka akifika kwenye mashine kwa kuambiwa insufficient balance ie huna salio.
Mteja angeweza kutumia simu kujua salio.
3. N.k ... n.k ...

IMG-20161018-WA0009.jpg
 
Habari wana jamvi
Siku kadhaa nyuma serikali ilitangaza siku rasmi ya kuanza mabasi ya mwendo kasi ambayo ni tar 10 may.

Matarajio yangu nilipoamka leo ni kutoona daladala kwenye barabara zote ambazo DART ilitakiwa ianze lakin hali ni tofauti daladala ziko kama kawaida na hakuna hata basi moja la mwendo kasi
 
Kuepusha vurugu kutokana uhaba wa usafiri,leo yataanza kufanya kazi kuanzia saa 4 asubuhi mpk watu watakapoanza kuyazoea kidogo kidogo yataanza safari za asubuhi


Kwani Yale yatazoeleka vipi bila kutumika Kwa wakati unaostahiki nashangaa Sana mauongo ya kuhusu hayo mabasi..unajuwa unapotangaza kitu isitoshe ni serikali inayotoa taarifa izo Nini maana yake.. Tafakari
 
Nimesikia Radio One kwamba yameanza na yameshafika katikati ya jiji. Mlioko along Moro road mtujuze zaidi.
 
Back
Top Bottom