Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mwanakijiji unapenda sana mada hizi kumbuka miaka 2 iliyopita ulianzisha mada gani iliyokuwa inahusiana na masuala haya leo unaruka unatakiwa kuomba radhi kwa mada ile na maneno uliyoporomosha wakati ule
Mambo ya ajabu sana kuhusuYonamaro:
1.Huyu ameingia JF 2010, lakin anajua mambo yalioandikwa hapa 2yrs ago!
2.Hajaweka link ya hiyo thread ya Mkjj iliyoonge tofauti na hii(ili ku'substantiate hoja yake)
3.Radhi huombwa inapothibitishwa kuwa mtu kakosea kweli!
 
Tukipita kila ofisi serikalini,binafsi,uwiiiii
wachaga tena wako post za juu jamani
inatia moyo lakini ndugu zetu tuwaachie na wengine naona watu wameanza kukasirika najua tofauti za shule ndio sababu basi msisome sana wengine tuingie huko.....wasije wakawalalia bagamoyo dunia mbaya hii..
Wakwe mmenisikia lakini

Mi nadhani umekosea ungesema wachaga wamejazana kila mkoa wakitafuta pesa yaani wafanyabiashara hapo ingetulia...ila maofisini sijui ila tujadili hebu tuanzie kwenye mawaziri...wabunge...na mashirika ya uma makubwa makubwa inakuwaje..ni wachaga....
 
Hakuna kabila wala watu waliokatazwa kusoma au kujielimisha. Elimu ndio msingi wa maendeleo. Way to go Wachagga na wasomi wote!!!
 
Mimi sioni tatizo na wachaga
mimi napenda watu wasio zubaa na maisha...
Natamani na wakikuyu wangekuwa tz........
Labda nchi hii ingepunguza ubwegebwege
 
Bi Mkongwe,
Usiseme uwongo. Katika awamu ya kwanza Wachagga tayari walikuwa mbele kielimu. Kulikuwa hakuna haja ya kuwapa average marks kuliko wengine. Kuanzia enzi za ukoloni Wachagga, Wahaya, wanyakyusa, walikuwa mbele sana katika elimu, thanks to missionary schools in their areas. Kulaumu awamu ya kwanza kwa upendeleo ni uwongo wa mchana.

Sasa uwongo uko wapi? Hebu soma vizuri uelewe nilichoandika. Wao walikuwa na average mark kubwa kwa sababu wameamka kielimu mapema ukilinganisha na makabila mengine. Na ndio maana average pass mark ikawekwa kubwa kwa mkoa ule ili wanaoingia sekondari wawe wachache. Na hiyo ndio ilileta msukumo wa wao kuwa mbele katika secondary na high school na vile vile kujenga private schools.

Hiyo tuliambiwa na mwalimu mmoja katika kusoma Development Studies na huyo mwalimu wala hakuwa Mchaga bali ni wa kutoka kusini ya Tanzania. Na hivi karibuni tulikuwa na mjadala huo na Wachaga wa ofisini walilisema tena hilo.

Hawakupendelewa na Nyerere bali ni jitahada zao wenyewe.
 
Hii naitazama kwa jicho la 3, ina maana kubwa zaidi ya hivyo uionavyo! OK..na tuijadili!
Yes JP!!!!
Hapa kwenye Green ndio kuna kiini na jambo flani la kujifunza tena kwa kina na umakini sana, maana ipo tofauti kubwa sana kati ya (Wajibu na Kujituma), (Kusaka na Kutafuta)na hata (Fanani na Mkunga)

Nadhani kipo kitu kikubwa sana cha kujifunza juu ya hili na hakuna cha kushabikia hata kimoja katika hili. Nasema hivi kwasababu ipo tofauti kubwa kati ya yule awazaye juu ya kesho yake itakavyokuwa na yule awazaye juu ya jana yake ilivyokuwa.
 
Huo ni wivu. Je wanapata nafasi hizo kwa mlango wa nyuma? Wengi Shule imepanda. wakati wengine tunaendekeza kuchunga ng'ombe, kusoma madrasa wao wanasoma. Je unategemea nini. Sio wachaga tu.Kuna Nshomile, kuna mwaki...., kuna thithi hapa. Pelekeni watoto wenu shule!!!
 
ee wachagga mpaka mnawajadili hapa? inabidi mchunguze kiini cha wao kuwa maofisini kwa wingi ila kabila hili wanajali elimu sana, wakati nikiwa chuo pale mji kasoro bahari basi karibu nusu walikua wachagga maana cku ya mikutano yao utasikia warombo, waoldmoshi yani hawawezi kukaa mkutano mmoja wote maana ni wengi mno. makabila mengine tunyanyuke kielimu jamani!
 
Wahaya wako wapi? Mbona wao ndiyo inshomile kuzidi wachaga! Sema nafasi nyeti na muhimu na kupigiana pande ndiyo kunawafanya waonekane hivyo! Nilipomaliza chuo nilisota sana kupata ajira lakini wachaga wote niliomaliza nao walipata kazi mapema (kupigiwa pande la fasta) na wengi walikuwa kwenye umeneja though they were fresh from school
 
Huu muda wa kulaumu wachaga mngetumia kusoma kama wao au kushawishi makabila ambayo yanajiona nyuma yapige buku. Pia hao mnaowaita wachaga wana moyo wa kudhubutu..."life is either daring or doing nothing " kila kazi wao wanapiga. Wengine ni kujisifu tu kwa mavazi na kidhungu huku wengine wanaendelea.
 
MIMI NILIDHANI HAO ANAOWAITA wACHAGA HAWANA sIFA KTK NAFASI ZAO...........wakati jamii nyingine zikihamasishwa leo kujenga shule kila kata, baadhi ya Wilaya za Wachaga kule mkoani Kilimanjaro kufikia miaka ya mwishoni mwa 90 zilikua tayari na shule, sasa fikiria mkoa wa lindi ambao kufikia mwaka 2003 ulikua na shule pungufu ya kumi za sekondari, hii iliathiri pia Pwani, Kigoma, Tabora, na shinyanga....
sasa usitegemee utaweza kupambana na wachaga hawa ni wasomi sana, wapambanaji sana.....wito wangu ni jamii kuamka na kuamini shule ni msingi wa maendeleo.
 
Bi Mkongwe,
Usiseme uwongo. Katika awamu ya kwanza Wachagga tayari walikuwa mbele kielimu. Kulikuwa hakuna haja ya kuwapa average marks kuliko wengine. Kuanzia enzi za ukoloni Wachagga, Wahaya, wanyakyusa, walikuwa mbele sana katika elimu, thanks to missionary schools in their areas. Kulaumu awamu ya kwanza kwa upendeleo ni uwongo wa mchana.


Jasus, Bi Mkongwe is right. Ilikuwa inaitwa 'positive discrimination'. Hii ilihusu pasi za kuingia form one kwa mkoa wa Kilimanjaro. Positive Discrimination imekuwa ikitumika pia katika mambo ya Gender. 1974 ilipopitishwa Azimio la Musoma, kina dada walikuwa wanapewa nafasi za upendeleo za kuendelea moja moja chuo kikuu baada ya form 6 lakini wavulana tulikuwa tunalazimika kwenda kufanya kazi miaka 2 kabla ya kujiunga na Chuo; wavulana waliokuwa na masomo ya sayansi walipendelewa sawa na kina dada! Na hata leo kina dada wana nafasi za upendeleo kujiunga na Chuo Kikuu, kwenda bungeni, na hata kuchaguliwa kuwa maCEO. Sidhani kama ni zana mbaya lakini lazima kuwepo na kikomo.

Kwa hili la Moshi, wakati ule kila mkoa ulikuwa na mgao wake kwa nafasi za sekondari, Moshi walipewa chache mno ingawaje walikuwa wengi mashuleni. Matokeo yake nakumbuka wazazi wengi wa Moshi waliwapeleka watoto wao kusoma shule za msingi mikoa mingine na hata kuwapa majina yasiyoashiria walikotoka. Leo hii wapo maofisini ambao wanatumia majina bandia hasa wale waliokwenda kusomea mikoa ya Lindi na Mtwara ambako ilikuwa rahisi mno kushinda kwenda form one. Siwezi kukutajia majina, licha ya uhuru wa kusema nilio nao.

Ila sioni tija yeyote kwa kujadili mada hii, imekaa kiwivu wivu!
 
Back
Top Bottom