Mkjj,
Kwanza ninawapa pongezi wanajambo wote kwa kukata issue!.mimi nimsomaji wa siku nyingi toka bcs lakini si mchangiaji.Lakini hii maada imenikumba hata mimi katika harakati zangu za maisha ya kazi,nilipokuwa ndani ya mfumo wa serikali
Hili swala ni gumu kwa kuangalia kwa inje,nikiwa na maana ya kuwa kama mtu si mwajiriwa wa serikali au shirika la umma lolote.
unachokisema ni sahihi kwa wakati huo,lakini kwasasa hivi makabila mengi wamesoma,lakini kwa sababu waliotangulia ni wa makabila hayo,basi kazi zitakwenda kwa kuangalia kama muombaji anatoka kwenye kabila lake au laa.hapa ninamaana hakuna usawa,hata hizo nafasi za shule zitakwenda kwa mfumo huo.kwa hiyo labda tujadili nia mbadala lakini ukweli ndiyo huo kwa mtu ambaye yupo ndani ya mfumo wa serikali unaona hili,lakini kwa mtu ambaye haupo ndani ya mfumo huo unaweza usikubaliane na mtoa hoja.Ninaomba kutoa .01%
SIMPLY UNTRUE!
Mimi namuunga mkono mia kwa mia M-kijiji, kwamba kweli ajira ziko skewed kuelekea kwenye makabila fulani kwa sababu ambazo zimetajwa. Tunaona kwamba sasa makabila mengine nayo sasa yamo vizuri tu kwenye ajira kutegemea na uwezo wao.
Hata hivyo ni vigumu kumwondoa mtu ambaye tayari ni "insider". Kufanya hivyo kunahitaji matayarisho pamoja na level playing field.
Sasa kama una evidence ya kutokuwepo kwa usawa huo katika kinyanganyiro cha kazi, then unatakiwa kuyasema hayo.