ofrey Nyangoro
KADA wa CCM, Mustafa Sabodo ameahidi
kuchimba visima 200 katika majimbo yote ya
wabunge wa Chadema nchini, huku akieleza
kuwa angependa kuona upinzani unachukua
nchi mwaka 2015.Sabodo ambaye ni kada wa
CCM tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyarere, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa
akipokea mpango wa uchimbaji visima hivyo
kutoka kwa Katibu wa Chadema, Dk Willibrod
Slaa.Kauli hiyo ya Sabodo ambaye tayari katika
Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana aliisaidia
Chadema Sh100 milioni za kampeni, imekuja
kipindi ambacho CCM, inakabiliwa na
mpasuko kutokana na siasa za makundi.
Wakati CCM ikikabiliwa na kipindi hicho
kigumu kisiasa, jana Sabodo ambaye aliahidi
kuendelea kukisaidia Chadema, alisema
Ningependa kuona upinzani ukichukua nchi
mwaka 2015.
Jana Saa 4:00 asubuhi, Dk Slaa akiongozana na
Mkurugenzi wa Mambo ya Bunge wa
Chadema, John Mrema walifika nyumbani kwa
Sabodo kwa lengo la kukabidhi mchakato wa
utekelezaji wa mradi huo wa visima na pia
kumshukuru kada huyo wa CCM kwa
misaada yake kwa chama hicho.
Katika mazungumzo hayo, Sabodo
alimhakikishia Dk Slaa kwamba ataendelea
kusaidia chama hicho katika miradi mbalimbali,
inayohusu wananchi hususani suala la maji na
elimu.
Sabodo alisema elimu ni muhimu katika
maisha ya binadamu, lakini maji pia ni uhai,
kwakuwa bila maji hakuna mtu anayeweza
kufanya chochote.
Mradi wa Sh2.5 bilioni
Sabodo alisema ametenga Sh2.5 bilioni kwa ajili
ya kuchimba visima vya maji virefu na vifupi
700 katika maeneo yenye ukame, huku visima
200 kati ya hivyo vikielekezwa katika
majimbo 23 wanakotoka wabunge wa
Chadema na Jimbo la Igunga. Chadema kina
jumla ya wabunge 48 na 25 kati yao ni wa Viti
Maalum.
Alifafanua kwamba anatoa msaada wa maji
kwa sababu anatambua umuhimu wa huduma
hiyo kwa jamii huku akisisitiza kwamba maji
siyo anasa bali ni hitaji la lazima.
Kuhusu sababu ya kujenga urafiki na Dk Slaa
Sabodo alisema: Mimi siyo kwamba navutiwa
na wewe Dk Slaa hata nikaona umuhimu wa
kutoa msaada kwa Chadema, ninavutiwa na
Principle (Kanuni) zako na chama
chako,alisema Sabodo.
Michango hiyo ya Sabodo kwa Chadema
iliwahi kuibua manung'uniko kwa baadhi ya
makada wa CCM, lakini aliyekuwa Katibu
Mkuu, Yusuph Makamba, aliwahi kuliambia
gazeti hili kwamba, "Siyo vibaya Mkristo
kumsaidia Mwislam, ndiyo ubinadamu," hivyo
haoni tatizo kwa Sabodo kusaidia upinzani.
Dk Slaa anena
Kwa upande wake, Dk Slaa alisema chama
hicho kinatarajia kuchimba visima vya maji 11
katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora ikiwa
ni wiki takriban mbili tangu kumalizika kwa
uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika
Oktoba 2.
Dk Slaa alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya
kukabidhi mchanganuo wa namna
walivyogawa mradi wa utekelezaji wa visima
200, vilivyotolewa na Sabodo kwa lengo la
kuchimbwa katika majimbo tofuati
wanakotoka wabunge wa Chadema.
Alisema lengo la kutekeleza mradi huo wa maji
katika Jimbo la Igunga limetokana na ziara
aliyoifanya katika vijiji 98, vilivyopo katika
jimbo hilo na kugundua wananchi wake
wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji.
Katika mpango kazi wetu, tumepanga
kuchimba visima 11 katika Wilaya ya Igunga
mkoani Tabora, hii imetokana na ziara yangu
katika vijiji 98 ambapo niligundua kuwa
wakazi hao wanakabiliwa na tatizo kubwa la
maji,alifafanua Dk Slaa.
Chadema kilishika nafasi ya pili katika
uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, kwa aliyekuwa
mgombea wake, Joseph Kashindye kupata
kura 23,260 sawa na asilimia 44.3, nyuma ya
mgombea wa CCM, Dalaly Kafumu aliyeshinda
kwa kura 26,484 kati ya 52,487 halali
zilizopigwa, sawa na asilimia 50.4.
Dk Slaa alimshukuru Sabodo kwa msaada
wake wa kukusudia kuchimba visima vya
maji katika maeneo mbalimbali nchini,
yanayokabiliwa na uhaba akisema kitendo
hicho ni cha utu kwa kuwa maji ni uhai.
Nitoe shukrani kwa niaba ya wabunge
ninaowawakilisha kufuatuia msaada wako wa
kukusudia kuchimba visima 200 vya maji
katika majimbo yao, ni maelfu ya watu
watanufaika na msaada huu,alisema Dk Slaa
na kuongeza:,
Sisi tumekuja kukushukuru kwa niaba ya
wabunge wetu na wananchi, lakini pia
wabunge wangu watakuja mmoja mmoja
kukushukru wewe ni baba yao. Ushindi
walioupata ulitokana pia na msaada wako
mkubwa wa kifedha wakati wa
kampeni,alisema Dk Slaa.
Kwa upande wake, mchumba wa Dk Slaa,
Mushumbushi, alishukuru msaada huo wa maji
kutoka kwa Sabodo akisema utawasaidia
wanawake na watoto.
Watu wanaopatwana athari nyingi kutokana
na tatizo la maji ni wanawake na watoto, ni
wanawake ndio hupatwa na matatizo ya
kubakwa wanapokwenda umbali mrefu
kuteka maji. Pia ukame wa maji umevunja
hzbaadhi ya ndoa,alisema Mush