Ujumbe wa Sabodo Nyerere Day unatisha

Mwana CCM halafu tena anakipinga CCM, mbona sielewi?

Kwani haiwezekani mwanaccm akaipinga CCM kama inafanya madudu!? Mbona Mwalimu alifanya hivyo akiwa bado ni mwanachama hai ndani ya CCM!?
 
Huyu mzee anatafuta umaarufu kwa kupitia matatizo yetu.

Tumechoka na hizi kelele, tunachotaka sasa ni maamuzi magumu yatakayotuondoa ktk huu umaskini.

Matamko yanatosha. Tunahitaji vitendo sasa.
 
Huyu mzee anatafuta umaarufu kwa kupitia matatizo yetu.

Tumechoka na hizi kelele, tunachotaka sasa ni maamuzi magumu yatakayotuondoa ktk huu umaskini.

Matamko yanatosha. Tunahitaji vitendo sasa.

we unataka afanyaje zaidi?hata tamko tu linasaidia!
 
sabodo kashaona upepo unaenda wapi wa siasa kwaiyo kaanza mapema kujipendekeza kwa cdm kwani anajua watachukua nchi ivi punde,na kamwe cdm wasije msahau ktk ufalme wao! JAMAA MJANJA
 
ofrey Nyang’oro

KADA wa CCM, Mustafa Sabodo ameahidi kuchimba visima 200 katika majimbo yote ya wabunge wa Chadema nchini, huku akieleza
kuwa angependa kuona upinzani unachukua nchi mwaka 2015.Sabodo ambaye ni kada wa CCM tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyarere, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akipokea mpango wa uchimbaji visima hivyo kutoka kwa Katibu wa Chadema, Dk Willibrod
Slaa.Kauli hiyo ya Sabodo ambaye tayari katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana aliisaidia Chadema Sh100 milioni za kampeni, imekuja
kipindi ambacho CCM, inakabiliwa na mpasuko kutokana na siasa za makundi. Wakati CCM ikikabiliwa na kipindi hicho kigumu kisiasa, jana Sabodo ambaye aliahidi kuendelea kukisaidia Chadema, alisema “Ningependa kuona upinzani ukichukua nchi mwaka 2015”. Jana Saa 4:00 asubuhi, Dk Slaa akiongozana na Mkurugenzi wa Mambo ya Bunge wa Chadema,

John Mrema walifika nyumbani kwa Sabodo kwa lengo la kukabidhi mchakato wa utekelezaji wa mradi huo wa visima na pia kumshukuru kada huyo wa CCM kwa misaada yake kwa chama hicho.Katika mazungumzo hayo, Sabodo alimhakikishia Dk Slaa kwamba ataendelea kusaidia chama hicho katika miradi mbalimbali, inayohusu wananchi hususani suala la maji na elimu. Sabodo alisema elimu ni muhimu katika maisha ya binadamu, lakini maji pia ni uhai, kwakuwa bila maji hakuna mtu anayeweza kufanya chochote. Mradi wa Sh2.5 bilioni Sabodo alisema ametenga Sh2.5 bilioni kwa ajili ya kuchimba visima vya maji virefu na vifupi 700 katika maeneo yenye ukame, huku visima 200 kati ya hivyo vikielekezwa katika majimbo 23 wanakotoka wabunge wa Chadema na Jimbo la Igunga. Chadema kina jumla ya wabunge 48 na 25 kati yao ni wa Viti Maalum.

Alifafanua kwamba anatoa msaada wa maji kwa sababu anatambua umuhimu wa huduma hiyo kwa jamii huku akisisitiza kwamba maji siyo anasa bali ni hitaji la lazima. Kuhusu sababu ya kujenga urafiki na Dk Slaa Sabodo alisema: “Mimi siyo kwamba navutiwa na wewe Dk Slaa hata nikaona umuhimu wa kutoa msaada kwa Chadema, ninavutiwa na Principle (Kanuni) zako na chama chako,”alisema Sabodo. Michango hiyo ya Sabodo kwa Chadema iliwahi kuibua manung'uniko kwa baadhi yamakada wa CCM, lakini aliyekuwa Katibu Mkuu, Yusuph Makamba, aliwahi kuliambia gazeti hili kwamba, "Siyo vibaya Mkristo kumsaidia Mwislam, ndiyo ubinadamu," hivyo haoni tatizo kwa Sabodo kusaidia upinzani.

Dk Slaa anenaKwa upande wake, Dk Slaa alisema chama hicho kinatarajia kuchimba visima vya maji 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora ikiwa ni wiki takriban mbili tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika Oktoba 2. Dk Slaa alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kukabidhi mchanganuo wa namna walivyogawa mradi wa utekelezaji wa visima 200, vilivyotolewa na Sabodo kwa lengo la kuchimbwa katika majimbo tofuati wanakotoka wabunge wa Chadema. Alisema lengo la kutekeleza mradi huo wa maji katika Jimbo la Igunga limetokana na ziara aliyoifanya katika vijiji 98, vilivyopo katika jimbo hilo na kugundua wananchi wake wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji.

“Katika mpango kazi wetu, tumepanga kuchimba visima 11 katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, hii imetokana na ziara yangu katika vijiji 98 ambapo niligundua kuwa wakazi hao wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji,”alifafanua Dk Slaa. Chadema kilishika nafasi ya pili katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, kwa aliyekuwa mgombea wake, Joseph Kashindye kupata kura 23,260 sawa na asilimia 44.3, nyuma ya mgombea wa CCM, Dalaly Kafumu aliyeshinda kwa kura 26,484 kati ya 52,487 halali zilizopigwa, sawa na asilimia 50.4. Dk Slaa alimshukuru Sabodo kwa msaada wake wa kukusudia kuchimba visima vya maji katika maeneo mbalimbali nchini, yanayokabiliwa na uhaba akisema kitendo hicho ni cha utu kwa kuwa maji ni uhai.

“Nitoe shukrani kwa niaba ya wabunge ninaowawakilisha kufuatuia msaada wako wa kukusudia kuchimba visima 200 vya maji katika majimbo yao, ni maelfu ya watu watanufaika na msaada huu,”alisema Dk Slaa na kuongeza:,

“Sisi tumekuja kukushukuru kwa niaba ya wabunge wetu na wananchi, lakini pia wabunge wangu watakuja mmoja mmoja kukushukru wewe ni baba yao. Ushindi walioupata ulitokana pia na msaada wako mkubwa wa kifedha wakati wa kampeni,”alisema Dk Slaa. Kwa upande wake, mchumba wa Dk Slaa, Mushumbushi, alishukuru msaada huo wa maji kutoka kwa Sabodo akisema utawasaidia wanawake na watoto.

“Watu wanaopatwana athari nyingi kutokana na tatizo la maji ni wanawake na watoto, ni wanawake ndio hupatwa na matatizo ya kubakwa wanapokwenda umbali mrefu kuteka maji. Pia ukame wa maji umevunja baadhi ya ndoa,”alisema Mush

Mzeee huyu anawatesa CCM ni kishenzi, anapotoa msaada huku kavaa johoo la ccm
 
Huyu mzee anatafuta umaarufu kwa kupitia matatizo yetu.

Tumechoka na hizi kelele, tunachotaka sasa ni maamuzi magumu yatakayotuondoa ktk huu umaskini.

Matamko yanatosha. Tunahitaji vitendo sasa.
Usitumi kichwa chako kama sanduku la macho, pua na mdomo peke yake..........kuna ubongo humo pia!!

Unataka Sabodo afanye maamuzi?? yeye kafanya katika level yake, kawaambia viongozi wake kuwa mnaboronga, na amewapa wananchi katika majimbo ya CHADEMA huduma ya maji kuonyesha kwa vitendo kuwa hakubaliani na yanayotokea CCM.

Sasa kazi ni kwa viongozi wa CCM.
 
Ujumbe wa Sabodo ni kielelezo tosha na anao uhakika kwa ilo alisemalo kwamba mwaka 2015 CDM itashinda uchaguzi na
kuongoza Serikali ya Taifa jipya la Tanzania. Ambayo itakuwa ya Kidemokrasia na haki na kwa maksudi watayaopoa maisha
ya Watanzania ambayo yamezama katika kina kirefu cha umasikini. Tusemee ardhi sio kitu cha uwekezaji bali uboreshaji
kwa ukulima wa kisasa kwa wazalendo, mikakati ipo ya kufanikisha kwa wakulima wote na kutokomeza njaa na hata kulisha
Afrika nzima na kwingineko.
 
Huyu mzee mjanja sana na ninamwaminia kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu huku akiwa makini na magamba ambao wana historia ya kumaliza watu kwa njia mbali mbali.Huyu mzee amemzidi hata Mengi kwasababu yuko frontlines bila woga.

Ni ukweli kabisa tunaweza kupata matajiri wenye uchungu na nchi hii na wenye huruma na masikini.Huyu mzee ni mmojawapo.Maneno aliyosema yamenisuuza moyo,kwamba si wananchi masikini peke yao wenye kuona huu ufisadi na hali mbaya ya nchi kwa ujumla.

Ni wazi yuko very concerned kwani kwa utajiri alionao angeweza kula bata tu kama kina RA.
 
Back
Top Bottom