Ujumbe wa Sabodo Nyerere Day unatisha

Ujumbe wa Sabodo Nyerere Day unatisha

Mwana CCM halafu tena anakipinga CCM, mbona sielewi?

Mkuu, kipi kisichoeleweka, Mwl. Nyerere aliwahi kusema "mpinzani wa kweli atatoka ndani ya CCM". Hakuwa na maana kwamba lazima atoke ili awe kiongozi wa upinzani, la hasha. Hata anavyofanya Mzee wetu mzalendo Sabodo, ni aina ya kuonesha upinzani pia. Yeye ameamua kuipinga akiwa ndani ya CCM.
 
Huyu mzee anatafuta umaarufu kwa kupitia matatizo yetu.

Tumechoka na hizi kelele, tunachotaka sasa ni maamuzi magumu yatakayotuondoa ktk huu umaskini.

Matamko yanatosha. Tunahitaji vitendo sasa.

Wewe unadhani anatafuta umaarufu ili awe nani ? Yaani umaarufu zaidi ya hapo alipo au mie sijakuelewa ? Yeye ni maarufu kwa njia ya usafi ndiyo maana kaachana na CCM .Kama CCM wanadhani wanaweza kumkata koo kwa kodi ma uzushi waanze tuwasikie .Walianza kwaa Slaa na wizi sijui wa nini wakakwama .Haya nieleweshe wewe unadhani anautaka umaarufu awe nani ?
 
Huyo mzee ndo nimesikia akitamani nchi ichukuliwe na chama kingine tofauti na chama chake ifikapo mwaka 2015. Na ameahidi kutoa shs 0.5 bln kwa mgombea uraisi wa CHADEMA.
Huyo mzee naona anakiu ya mapinduzi ndani ya hii nchi, Mungu amsaidiye ayashuhudiye yakitokoea akingali hai.
 
Magamba watamlambisha sumu huyu, awe muangalifu sana kwenye tafrija mbali mbali za Magamba au asihudhurie kabisa.
 
Kada wa CCM na muumini wa falsafa za Baba wa Taifa, Mwl. JUlius Kambarage Nyerere, amechapisha matangazo ya kurasa mbili katika gazeti la Daily News la leo yakiwa na ujumbe mkali na kuonyesha kuchoshwa na baadhi ya mambo. Nina nukuu baadhi ya mambo aliyochapisha:
1. Corruption is an Ocean in Tanzania
2. Poor people are becoming poorest
3. I advise the Government to take more tough and prompt decisions
4. Unless we export atleast 59% of import value we always devalue our currrency
5. May I kill myself by fasting because I love my country?

Sabodo yuko sahihi kabisa.

Hata Baba wa Taifa ALIWAHI KUSEMA KUWA CCM SIYO MAMA YAKE! Kwa hiyo hata Sabodo CCM si mama yake. Leo yuko CCM na kesho akaamua kuhamia CHADEMA!

Kwa kweeli tu nisema kuwa HII CCM ya sasa ya kina NAPE NNAUYE imekwisha yaani ile tunasemaga KWISHNE! Sabodo ni mtu makini na mwenye PESA SAAFI(siyo ya UFISADI) na yeye anaitumia hasa kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Wa-tz.

Namwomba Sabodo ahamie CHADEMA haraka iwezekanavo kabla ya 2015 ILI MIKAKATI YA KUUNDA SERIKALI MPYA YA CHADEMA MWAKA 2015 ianze kuandaliwa mapeeema!!!

CCM BYE BYE 2015.
 
Cdm wanachekesha kweli,kwakua kawapa pesa watamsifu mpk watakufuru,hata rostam huyo wanaemtukana kila ainaya tusi hapa duniani akiamka kesho akatanga kuipa chadema 1billion tshs watamsifu na atakua msafi nawala hawatamwita tena fisadipapa ataitwa malaika mwema,kweli pesa hupasua milima namajabali,penye udhia penyeza rupia,wote tunapenda pesa ila wachaga mmezidi.
 
Heko Bw. Sabodo kwa kuzungumza kweli tupu........
 
Huwezi kuwa tajiri Tanzania bila kuwa fisadi.
Mtazamo wako sikubaliani nao. Kwa nchi yenye rasilimali kama hii kufikiria unavyofikiri ni dhambi. Unamuangusha Tintin kwa kutoangalia mbali zaidi ya urefu wa "pua" yako.
 
SI wana ccm wengi ni mafisadi kutoka moyoni wao kuiba, kutofata maadili yao wenyewe... kuuana wenyewe kwa wenyewe na mambo mengi yanayofanana na hayo yako ndani ya chama hiki... Ndiyo maana ktk ccm hakuna mwenye uchungu wa dhati kwa mtanganyika wanataman watoto wao watawale badala yao, waendele kutunyonya... Hawa ni mafisadi wa kuzaliwa na manafiki wakubwa ndiyo maana dada anashangaa maana c tabia yao kupenda haki wala ukweli.
kwa hiyo ccm wote wanakubaliana na kupenda ufisadi..thats what you want?
 
Namuombea huyu Mzee Mungu amsaidie aendelee kusema kweli daima, na wasimfanye tu naye akaanza kuvimba mwili.
 
huyo mzee ndo nimesikia akitamani nchi ichukuliwe na chama kingine tofauti na chama chake ifikapo mwaka 2015. Na ameahidi kutoa shs 0.5 bln kwa mgombea uraisi wa chadema.
Huyo mzee naona anakiu ya mapinduzi ndani ya hii nchi, mungu amsaidiye ayashuhudiye yakitokoea akingali hai.

atalishwa sumu very soon
 
namkubar sana sabodo coz sio muoga na nimzalendo wa kweli kunamizee kibao inaujua ukweli ila aifunguki kisa inakiogopa chama ccm ilikuwa ya nyerere wengine hawa wezi tu
 
Salaam wana jf, ninapendekeza tuwe na sikukuu ya kitaifa itakayo julikana kama nyerere day.kazi kubwa au madhumuni ya siku kuu hii iwe ni kufanya kazi za kujitolea sehemu mbalimbali kama vile mashuleni,vyuoni,mahospitalini,mitaani nk.pia siku kuu hii iwe ni siku ya kuendesha mijadala kwenye midahalo na makongamano mbalimbali juu ya mwenendo wa taifa letu kiuchumi,kisiasa,kielimu,maadili,kiuongozi nk.hii itatusaidia sana kama taifa kujitambua,kujsahihisha,kujipongeza hata kusimamia tunu zetu za taifa hili lililoasisiwa na mzalendo hayati mwalimu julius kambarage nyerere.nawasilisha
 
Napendekeza iwe siku ya kuzaliwa kwa Nyerere na si siku aliyofariki kama ilivyo wekwa sasa kama sikukuu ya kitaifa.
 
Hii ni tunu nyingine ya taifa letu.
Viva mzee sabodo!
Ni ukweli usiopingika kuwa c.c.m ya baba wa taifa siyo kama hii ya leo ya majambazi na machumia tumbo na yaliyo tayari ku kill any kiumbe kwaajili ya kulinda maslahi yao.
 
Back
Top Bottom