Uchaguzi 2020 Ujumbe maalumu kwa vyama makini vya Upinzani hasa ACTWazalendo na CHADEMA kuelekea Oktoba, 2020

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Mada inahusika.

Napenda kuwapa ujumbe huu maalum kwenu mkiona inafaa kuuzingatia kuelekea uchaguzi wa Oktoba, 2020.

i. Senario za Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2019 na kilichotokea , ziwape mbinu mia moja zaidi mbele kuhakikisha mnakwepa mitego yote ya CCM, NEC, ZEC na mawakala wao ndani na nje ya serikali.

ii. Hakikisheni mnaingia kwenye uchaguzi mkiwa wamoja. Epukeni njama ZA KUBAMIZWA KWA PAMOJA KWENYE HATUA YA MAPINGAMIZI, LAZIMA MUWEKE MBINU MBADALA. hii ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi huu.

iii. Unganeni kimkakati kwa maslahi mapana ya vyama vyenu kwa njia za kumpoteza adui yenu kisiasa. Acheni vihoja vidogo vidogo, tangulizeni maslahi ya jumla kwa kila upande mkitilia maanani zama zilizopo wameweka ahadi ya kufuta upinzani. Hiyo kauli MSIISAHAU.

iv. Msifanye makosa kwenye maamuzio yenu ya ushirikiano, msithubutu kutoa mwanya kwa adui, naamini mnao wataalamu wa kutosha wa kuyapima mambo na kuweka hatma yenu.

v. Kamati zenu za ufundi ziwe sawa kuanzia KWENYE ILANI NA SERA, CHAGUZI NA KULINDA USHINDI, MAWASILIANO NA HABARI, MAHUSIANO NA MAMBO YA NJE N.K. hUU NI WAKATI WA UELEDI ULIOPITILIZA. Msifanye makosa ya kimkakati kwenye hayo maeneo.

vi. Msisahau zama mnazopita na mziandalie uwiano ulio sawa na nguvu iliyo sawa. UMOJA WENU ndio silaha kubwa.

vii. Kuweni Makini na MSAJILI , NEC na ZEC , chimbueni kilichopangwa nyuma ya pazia mapema , toeni taarifa kwa umma na dunia kwa muda muafaka na muwe na mbadala wa mapigo tayari kibindoni, Juweeni mnayekwenda kushinmdana naye HATAKI UPINZANI. hilo mlijuwe. Na aminini hizi TAASISI ndizo nyenzo zitatumika kuwaondoeni kwenye Reli.

viii. Jiepusheni kulumbana wenyewe hadharani, hasa kipindi cha kampeni, jitahidini kuvumiliana kuepuka kuyasema hadharani mnayotafautiana wenyewe kwa wenyewe.

ix. Mje na mkakati wa kuwapa matumaini wana mageuzi kipindi hiki cha dhoruba kutoka kwa mtawala asiyetaka kuhojiwa, kupingwa wala asiyevumilia mtazamo tofauti.

x. Fanyeni maamuzi sahihi kwa wakati sahihi na imarisheni vitengo vyenu vya intelijensia ndani na nje ya taasisi.

Ni hayo tu.

Kishada
 
Asante.
 
Kwa mfano pimeni vitendo viwiili za Msajili hivi karibuni.

Kitendo cha kuwaandikia barua ACT juu ya kusudio la kuwachukulia hatua ACT kwa kile kilichoitwa kuvunja sheria na kwenda mbali kwamba sheria haitazami kipindi cha uchaguzi tu.

Kitendo cha kuitisha Media na kuionya CHADEMA hadharani.

Bila shaka kuna jambo linaandaliwa. Zidisheni umakini
 
Hapo kwenye kujaza fomu na mapingamizi ndio usipime. jiandaeni na kila kibweka
 
Back
Top Bottom