Ujue ugonjwa wa Mba na tiba yake

mba nidalili ya ngoma/HIV pia kwa hiyo kapime kwanza ili ujue unamba wa ngoma au unao ule wa kawaida
 
Dawa ya mba..
1. Ndimu/Limao
kabla ya kwenda kuoga chukua limao kisha jisugue nalokichwani na baada ya hapo tia maganda ya limao katika maji ya kuoga hakikisha yanakuwa dafidafi halafu ukoshe kichwa kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yalio safi.
2. Fenugreek(uwatu)
ipo kama vijiwe vidogovidogona rangi yake ni ya brown

Matumizi;
-chukua vijiko viwili vidogo vya fenugreek
-loweka kwenye maji kwa usiku mzima
-kisha ziponde
-paka kichwani na uache kwa muda wa saa moja
-osha nywele zako

ukiweza fanya hivi siku zote mba wataondoka bila taabu yoyote.

Copyright: MziziMkavu
 
Nenda duka lolote la dawa wambie wakupe WHITEFIELD kachupa kadogo kama babycare ndogo na yenyewe ni mafuta ya mgando nenda katumie utakuja kunipa matokeo.ila ili dawa ifanye kazi vizur unatakiwa unyoe nywele ili upake vzuri
 
papaya.jpg

Mbegu za papai tiba ya mba

Pia mapapai yaliyoiva yanatibu mapunye (ringworm), mabichi yanatibu msukumo mkuu wa damu (high blood pressure), mapapai yanatumika kama mkuyati (aphrodisiac), yanatumika kama kituliza maumivu (analgesic), mbegu za mapapai zinapunguza maumivu ya tumbo (stomachache)

Mba au mabaka mabaka kwenye ngozi ni miongoni mwa mambo yanayosababisha ngozi kukosa muonekano mzuri na hata kumfanya mhusika mwenye matatizo kujikuta akijikuna kila wakati.

Kitaalamu mba ni aina mojawapo ya magonjwa yanayoambukizwa na fangasi ambao husababisha muwasho.

Wanawake wengi wanakumbana na matatizo haya ya mba, kutokana na kupaka aina ya vipodozi vinavyowaletea athari katika ngozi zao.

Unapokumbana na tatizo la namna hii ni vizuri kujipaka dawa zinazofaa badala ya kutafuta krimu ambazo ni hatari zaidi. Mbegu za papai ni tiba nzuri na ya asili ambayo haiwezi kukuletea madhara zaidi.

Jinsi ya kuondoa mba kwenye ngozi ya uso

Mbegu za papai ni dawa ya asili inayoweza kutibu ngozi yako na kukuondolea tatizo la kuwashwa au mabaka yanayokukabili.

Namna ya Kutumia kama ni Dawa Mbegu za Papai.

Unachotakiwa kufanya ni kuzipondaponda na kujipaka kwenye eneo lililoathirika na mba. Hii itasaidia kuondoa ugonjwa huo na kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye afya nzuri.

Unaweza kutumia krimu maalum za kuondoa mba hizo, zinapatikana katika maduka ya dawa, lakini unachopaswa kufanya ni kufuata masharti na kupaka kwa umakini kwenye sehemu ilioathirika.

Waweza pia kutumia sabuni maalum ya maji, shampoo, poda na hata baadhi ya losheni zote hizi zinaweza kuisafisha ngozi yako na kuifanya iondokane na muwasho unaokukera na wakati huo kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye kuvutia. tumia kisha unipe feedBack Mkuu.@Bob Fern
 
Wanajamvi habari zenu? Kwa takribani miaka 15 ninasumbuliwa na mba mwilini, tiba hospitali nimepata mara kadhaa ikiwemo kupewa dawa ya mba ile ya maji ya kijani, dawa ya tube ya kupaka na vidonge vya kumeza, hivi mara ya mwisho oct 2012 nilienda hospitali nikapewa tube ya kupaka na nikaambiwa nitumie sabuni ya detal siku zote japo paka saizi natumia sabuni ya detal lakini nikijiangalia kwenye kioo sehemu za mgongoni naona mabaka ya mba yametoka tena...wanajamvi tafadhali mwenyekuweza kunisaidia maana sio siri nakereka sana mwenzenu kwani kipind fulani huwa nawashwa mwilimzima.
 
Mtafute daktari maalum wa ALEJI. M-ba wako inaelekea pia unatokana na aleji ya vyakula fulani unavyokula. Mfano watu wengi wa group 0+ nikiwa mmojawapo wanasumbuliwa mno na aleji ya vyakula vinavyotoka baharini, yaani samaki na ect. So, tafutata mtaalamu wa masuala ya aleji anaweza kukusaidia. Zaidi ya hapo unaweza kutafuta wataalamu zaidi.
 
Nina tatizo kama lako hadi wakati mwingine naona aibu kutoa shati hata kama kuna joto vipi.

Nimetumia hiyo dawa ya kijani, tube, vidonge na zingine bila mafanikio yoyote.

Lakini baada ya muda nilishauriwa kutumia Brake Fluid ya magari (ziko aina mbili nijuavyo mimi, ya mkebe wa plastic na ile ya mkebe wa bati). Chukua hiyo ya mkebe wa bati jisugulie kote kwenye mba na mabaka mpaka usikie kama joto hivi.

Inasaidia kwanza inapunguza na kufuta mabaka kabisa, baada ya siku ya tatu ama nne utaona mabadiliko.

NOTE: Haitazitoa milele, ni Alergy the only way ni ujue chakula gani kibovu unatumia ukiache.
 
Kaka nashukuru kwa ushauri, lakini katika hatua zangu kabisa za matibabu kabla ya kwenda hospitali nilikuwa natumia mafuta ya brake tena kwa kupaka mwili mzima coz nilikuwa naletewa na kaka zangu, yalikuwa yananisaidia kwa muda zinarudi tena, possibly kama ulivyosema itakuwa aleji....lakin wapi kwa kumpata Dk huyo?
 
Wanajamvi habari zenu? Kwa takribani miaka 15 ninasumbuliwa na mba mwilini, tiba hospitali nimepata mara kadhaa ikiwemo kupewa dawa ya mba ile ya maji ya kijani, dawa ya tube ya kupaka na vidonge vya kumeza, hivi mara ya mwisho oct 2012 nilienda hospitali nikapewa tube ya kupaka na nikaambiwa nitumie sabuni ya detal siku zote japo paka saizi natumia sabuni ya detal lakini nikijiangalia kwenye kioo sehemu za mgongoni naona mabaka ya mba yametoka tena...wanajamvi tafadhali mwenyekuweza kunisaidia maana sio siri nakereka sana mwenzenu kwani kipind fulani huwa nawashwa mwilimzima.

Skin fungal infections are common especially in tropical areas. Nilikuwa na tatizo kama la kwako, nikiwa mdogo nilipata kichwani (mapunye)ilibidi ninyolewe nywele zote. Nilivyofikia puberty years ikatokea mgongoni, mara zote hizo nilitibiwa na whitefield ointment nikadhani tatizo limepotea. Miaka karibu kumi iliyopita nilikuwa ninawashwa mwili mzima, sehemu fungus walikuwa wanaonekana ilikuwa chini ya maziwa. Kichwani nilipata mba wa ajabu, sikuwa ninaweza kusuka nywele, especially nikisuka rasta baada ya siku mbili zinaonekana chafu kwaajili ya utando mweupe unaozunguka.

Nilikutana na Dr wa Kinageria, akaniambia atajitahidi mpaka hili tatizo linakwisha, ikiwezekana kuchuka skin sample na kuipeleka lab wajui ni type gani ya fungal infection. Alinipa vidonge (diflucan tablets) nitumie kwa miezi mitatu kila siku kidonge kimoja, aliniandikia (daktacort cream) nipake zile sehemu zenye mba nizoweza kufikia na aliniandikia (nizoral shompoo) ilibidi nikate nywele upara kabisa na kuna siku nilikuwa ninapaka shampoo bila kuosha na ninalala mpaka asubuhi nikiosha shampoo nilikuwa ninapaka dakttacort cream. Nilifanya matibabu haya kwa muda wa miezi mitatu bila kuacha. Ninashukuru kwangu sasa mba ni historia.
Sabuni ya detol ni kwa bacteria infections such as vipele na ukumbuke mba ni fungal infection.
 
Mtafute daktari maalum wa ALEJI. M-ba wako inaelekea pia unatokana na aleji ya vyakula fulani unavyokula. Mfano watu wengi wa group 0+ nikiwa mmojawapo wanasumbuliwa mno na aleji ya vyakula vinavyotoka baharini, yaani samaki na ect. So, tafutata mtaalamu wa masuala ya aleji anaweza kukusaidia. Zaidi ya hapo unaweza kutafuta wataalamu zaidi.

Bigbro nashukuru kwa ushaur wako, ni kweli kabisa hata mim blood group langu ni o japo sijui kama ni o+ au vinginevyo, jambo nalotaka unisaidie pia mkuu ni wap tampata Dr wa alergy?
 
Bigbro nashukuru kwa ushaur wako, ni kweli kabisa hata mim blood group langu ni o japo sijui kama ni o+ au vinginevyo, jambo nalotaka unisaidie pia mkuu ni wap tampata Dr wa alergy?

Nitaku-PM jina la daktari wa pale Muhimbili na contact ukamcheki.
 
Aisee. Pole sana. Mba unafedhehesha sana.
Jaribu kwenda kwa dr mwingine uone itakuwaje.
 
Pole sana but jipe moyo kwani naamini ipo siku zitaisha. Kikubwa ni kufuatilia ushauri uliopewa hapo juu coz naamini utakusaidia to some extent.
 
Wanajamvi habari zenu? Kwa takribani miaka 15 ninasumbuliwa na mba mwilini, tiba hospitali nimepata mara kadhaa ikiwemo kupewa dawa ya mba ile ya maji ya kijani, dawa ya tube ya kupaka na vidonge vya kumeza, hivi mara ya mwisho oct 2012 nilienda hospitali nikapewa tube ya kupaka na nikaambiwa nitumie sabuni ya detal siku zote japo paka saizi natumia sabuni ya detal lakini nikijiangalia kwenye kioo sehemu za mgongoni naona mabaka ya mba yametoka tena...wanajamvi tafadhali mwenyekuweza kunisaidia maana sio siri nakereka sana mwenzenu kwani kipind fulani huwa nawashwa mwilimzima.

poleni sana pengine akija MziziMkavu atasema neno.
Mkuu KITWANGAUTAM Dawa ya Mba Mafuta ya Habati sawda na Mafuta ya Nazi. Kinachotakiwa Kufanya ni kuwa Wakati ukienda Kuoga Kichwani Yakupasa Uoshe nywele kwa maji Ya uvuguvugu kisha Ukifute kichwa Uzuri sana kiasi Kisibakiwe na Maji maji mengi, Ila nywele ziwe zimelainika tu!.. na Sehemu zenye huo mba.

Kisha Unachukua Mafuta ya Nazi (coconut oil) unachanganya na Mafuta ya Habati sawda kisha unajipakaa kichwani na sehemu zenye huo Mba mafuta ya kutosha . Asubuhi na usiku.Haya bibie.@Mamndenyi Nimesha mpa hiyo dawa ya mba.

Inshallah Kwa dawa hiyo ndio itakusaidia Tumia kisha uje unipe Feedback.
 
Last edited by a moderator:
Kuna hospital moja arusha wilayani arumeru ya wajerumani wataweza kutatua tatizo lako vizuri kabisa.

Jina la hospital limenitoka lakini iko located maeneo ya ngarenanyuki juu kidogo ya hifadhi ya taifa ya wanyama momela (arusha national park).
 
ndugu wana jf, nimekua nikisumbuliwa na ugonjwa kwa muda mrefu. nimejaribu kuutibu lakini umekua ukipotea na kurudi baada ya muda. naombeni ushauri kuhusu dawa gani nitumie kuondokana na ugonjwa huu..
 
Back
Top Bottom