Ujue ugonjwa wa Mba na Tiba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujue ugonjwa wa Mba na Tiba yake

Discussion in 'JF Doctor' started by JamiiForums, Feb 19, 2009.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,091
  Likes Received: 2,230
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Tunaomba ushauri wenu, wapi kwa Dar anapatikana Daktari ambaye ni specialist wa magonjwa ya ngozi.

  Tunauliza hivi kwa niaba ya watu wengi sana ambao wamekuwa wanatupigia simu wakitaka kujua ni wapi watapata mtaalam wa magonjwa ya ngozi na hili la MBA likiwa mojawapo.

  Shukrani

  ========

   
 2. Willy

  Willy Member

  #2
  Feb 19, 2009
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 78
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Hi Pole, ugonjwa huo wa ngoyi no common sehemu yenze unyevunyevu mwingi( high humidity, ndyo maana unatoweka ukikaa sehemu za baridi na kurudi sehemu za joto.

  Kwanza tumia dawa kwa muda mrefu ie 6-12 weeks. Pili zingatia usafi kwa kupasi nguo mara kwa mara, tatu usivaliane nguo. La mwisho ambalo ni muhimu, sehemu zenye mikunjo kama chini ya maziwa, kwenye mapaja (groin utumie powder ya kupunguza unyevu, usitumie dawa za uhakika kutoka kwa daktari wa ngozi.

  Kama wewe ni mnene kama ninavyohisi punguza unene. Nenda kamwone daktari wa ngozi kama hali itaendelea.

  ===================

  Je, ni vipi hushambulia ngozi?

  Maeneo yenye mabaka yanayoletwa na fangasi wa aina hii hubadilika rangi yake na kuwa na rangi hafifu au inayoonekana zaidi (kama ni mtu mwenye rangi ya maji ya kunde basi ngozi iliyoathiriwa hubadilika na kuwa nyeupe au nyeusi sana.

  Hali hii hutokana na uwezo wa fangasi wa aina hii kusimamisha shughuli za uzalishaji wa homoni na kemikali inayoipa ngozi rangi yake. Hii husababisha upungufu wa kemikali na hivyo mabadiliko ya rangi ya ngozi.

  Upungufu huo ya rangi ya ngozi si wa kudumu, bali ngozi hurudi kwenye hali ya kawaida ya rangi yake baada ya muda mrefu kidogo tangu maradhi halisi yalipokomeshwa. Bila matibabu maradhi haya huchukua muda kupona hivyo dawa ni muhimu ili mwenye maradhi aweze kupona upesi.

  Namna ya kuyatambua

  Maradhi haya ni rahisi kuyagundua ila kutokana na kufanana kwake na maradhi mengine yenye dalili kama hizi uhakiki wa vimelea vinavyosababisha maradhi haya ni muhimu.

  Sehemu ya ngozi kutoka kwenye eneo lenye maambukizi huchukuliwa na kupelekwa maabara ambako sehemu hii ya ngozi huwekwa kwenye darubini maalum kwa ajili ya kuangalia vimelea hivi vya fangasi.

  Nini matibabu yake?

  Maradhi haya huweza kutibika kirahisi, ila mara nyingi hurudia kushambulia ngozi hasa eneo ambalo liliwahi kushambuliwa kabla.

  Kutokana na uwezo wake wa kurudia kuambukiza ngozi huwa inashauriwa kwa aliyewahi kupata maradhi haya kurudia kutumia dawa ya kuua vimelea vya fangasi mara kwa mara ili kuondoa uwezekano wowote wa maradhi kurudia kushambulia.

  Matibabu ya maradhi haya huhusisha dawa za kupaka zinazoua vimelea hivi vya fangasi.

  Dawa za kuua vimelea vya fangasi za kunywa pia hutolewa kwa ajili ya kutibu aina hii ya fangasi lakini hushauriwa zitolewe tu kama dawa za kupaka zimeshindwa kuua vimelea hivi vya fangasi.

  Maradhi yanayofana nayo:

  Kuna magonjwa ambayo hufanana na maradhi haya. Mfano ;

  -Pumu ya ngozi

  -Vitiligo

  Maradhi haya tutayazungumzia kwenye makala zijazo kwenye mtiririko huu.

  Matokeo baada ya matibabu

  Kama nilivyoandika hapo juu maeneo ya ngozi yaliyobadilika rangi huweza kubaki hivyo hata baada ya vimelea vya fangasi kuondolewa na dawa.

  Hii inamaanisha inawezekana kabisa mgonjwa akabaki na mabaka yanayotokana na vimelea hivi vya fangasi muda mrefu hata baada ya kutumia dawa ambayo imefanikiwa kuondoa vimelea hivi vya fangasi. Hali hii mara nyingi huchanganya wagonjwa na kusababisha wagonjwa kudhani kuwa maradhi bado upo hivyo kuendelea kutumia dawa au kuanza kutumia dawa baada ya muda mfupi tangu kumaliza kutumia dawa zilizofanikisha uondoaji wa vimelea.

  Hali ya sehemu ya ngozi iliyoathiriwa na vimelea vya fangasi kurudisha rangi ya kawaida ya ngozi kama sehemu nyingine ambazo hazikua na madhara huchukua muda mrefu kidogo ingawa kama eneo husika lilikua na uvimbe basi uvimbe hupotea haraka.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Dawa ya kutibu Maradhi ya ugonjwa wa ngozi uchukuwe tango ulioshe vizuri kisha utengeneze juisi ya matango juisi hiyo uitengeneze lakini bila kumenya maganda ya matango na uwe unakunywa asubuhi kikombe kimoja mchana kikombe kimoja na jioni na pia uendelee kutafuna matango bila ya kumenya kwa uwezo wa Mwenyeezi Mungu ugonjwa wako utapona. tumia hii dawa kisha unipe Feedback

  Tiba ya mba kwa kutumia mbegu za papai

  Mbegu za papai tiba ya mba

  Pia mapapai yaliyoiva yanatibu mapunye (ringworm), mabichi yanatibu msukumo mkuu wa damu (high blood pressure), mapapai yanatumika kama mkuyati (aphrodisiac), yanatumika kama kituliza maumivu (analgesic), mbegu za mapapai zinapunguza maumivu ya tumbo (stomachache)

  Mba au mabaka mabaka kwenye ngozi ni miongoni mwa mambo yanayosababisha ngozi kukosa muonekano mzuri na hata kumfanya mhusika mwenye matatizo kujikuta akijikuna kila wakati.

  Kitaalamu mba ni aina mojawapo ya magonjwa yanayoambukizwa na fangasi ambao husababisha muwasho.

  Wanawake wengi wanakumbana na matatizo haya ya mba, kutokana na kupaka aina ya vipodozi vinavyowaletea athari katika ngozi zao.

  Unapokumbana na tatizo la namna hii ni vizuri kujipaka dawa zinazofaa badala ya kutafuta krimu ambazo ni hatari zaidi. Mbegu za papai ni tiba nzuri na ya asili ambayo haiwezi kukuletea madhara zaidi.

  Jinsi ya kuondoa mba kwenye ngozi ya uso

  Mbegu za papai ni dawa ya asili inayoweza kutibu ngozi yako na kukuondolea tatizo la kuwashwa au mabaka yanayokukabili.

  Namna ya Kutumia kama ni Dawa Mbegu za Papai.

  Unachotakiwa kufanya ni kuzipondaponda na kujipaka kwenye eneo lililoathirika na mba. Hii itasaidia kuondoa ugonjwa huo na kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye afya nzuri.

  Unaweza kutumia krimu maalum za kuondoa mba hizo, zinapatikana katika maduka ya dawa, lakini unachopaswa kufanya ni kufuata masharti na kupaka kwa umakini kwenye sehemu ilioathirika.

  Waweza pia kutumia sabuni maalum ya maji, shampoo, poda na hata baadhi ya losheni zote hizi zinaweza kuisafisha ngozi yako na kuifanya iondokane na muwasho unaokukera na wakati huo kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye kuvutia.  Kitunguu swaumu pia ni dawa ya fangasi

   
 4. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Skin fungus infections are hard to recognize. The itching, flaking, redness, and thickened skin of fungal infections can look just like other types of dermatitis or skin allergies.

  In fact, eczematous skin often becomes infected with fungi, so both are present simultaneously. Doctors use microscopes to help them diagnose skin fungus infections, so there’s no way you can really be sure at home.

  Tinea Versicolor. This fungus actually changes the color of the skin it infects; the patches may be lighter or darker than your normal surrounding skin. This spotted pattern and the fine scaly flakes at the margins make this fungal infection the easiest to identify. Since itching and irritation are mild, it’s also the least bothersome.

  Warmth, humidity, sweating, and poor air circulation all help bring about these fungal infections. But they are contagious, too. Athlete’s foot is believe to be passed on locker room and shower floors, and by sharing footwear and socks; you can acquire tinea versicolor from vinyl surfaces of weight lifting benches; and of course ringworm is contagious through direct contact (usually kids).

  There are several effective OTC anti-fungal medications. Because different fungi affect different locations, medications are sometimes specific for those locations. The recommendations below should help you sort it out.

  Although not a Category I agent, selenium sulfide shampoo is universally recognized by dermatologists as an effective OTC remedy for tinea versicolor. Since it often affects large areas of the trunk, applying this shampoo once a day for five minutes, then washing off, is a lot easier and cheaper than using a whole tube of anti-fungal cream twice daily. Tinea versicolor also tends to recur easily, but this shampoo can prevent it if used once a week after the initial 2-4 week treatment cycle.

  Kim @ ire
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ASANTE BABA!
  hizi makala ndo zenyewe hizi..............!Wasiwasi wangu ni watu kuisoma na kuilewa.maanake wanajamii kwa sasa wanazipitia sana makala za mafisadi,wanasahau hata afya zao
   
 6. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Kwa ushauri na Tiba yenye akili, nenda pale LUTHER HOUSE kuna clinic ya magonjwa ya ngozi, utampata mtaalam aliyebobea (Dermatologist), au unaweza kwenda TUMAINI HOSPITAL upanga matatizo yako yataisha.
   
 7. Chocolate

  Chocolate Senior Member

  #7
  Feb 20, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Asante sana mkuu nitakwenda kama ulivyonishauri. God Bless you all!
   
 8. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Chocolate

  kuna baadhi ya watu wanatatizo kama hilo,naamisha hiyo hali tatizo hutokea katika hali ya joto na kupotea katika kipindi au maeneo yenye baridi,ila wao hutokea maeneo ya sehemu za siri.

  YAWEZEKANA IKAWA NINI?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana najua usumbufu wake.

  Kama yote uliyoshauriwa hapo juu yakishindikana na kama uko tayari kughalimia afya yako zaidi, kuna Specialist wa ngozi (Ni clinic ya ngozi tu)-kwenye kimtaa zinapopita dala dala kabla ya kuingia UN Road zikitokea Muhimbili.

  Pia Kuna cream na lotion za watu wa Forever Living, shida ni kuwa ni gharama sana lakini nilikuwa na tatizo kama hilo lilikwisha kabisa kabla hata ya kumaliza nusu dose. Na wakati ukiendelea na hizo njia zingine jaribu kutumia sabuni zenye aloevera zinaweza kukusaidia pia.
   
 10. Bibie

  Bibie Member

  #10
  Feb 24, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I think you need to see a dermatologist for sure. Hiyo Fluconazole si ya vaginal thrush sasa ni nani alikupatia kutibu mba?? Be careful nenda hospitali upate proper prescription. Pole sana
   
 11. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Dr Mgonda MD...PhD, Muhimbili ila sorry sina contact zake uliza tu MNH watakupatia
   
 12. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nenda pale Lutherhouse Azania Front yuko Drt ila sina simu yake
   
 13. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #13
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Asante, nadhani utampata tu.
   
 14. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #14
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ukiwa unaelekea muhimbili kwa daladala zinazotokea faya kwenye ule mtaa unaochepuka toka Umoja wa mataifa, kuna kitengo cha magonjwa ya ngozi.
   
 15. r

  ruma Member

  #15
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr mwinine yupo Rufiji kwenye Hosptal moja aitwa Rutete anaitwadr Rwamtonga
   
 16. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #16
  Aug 7, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Regency tel.2150500, Aga khan 2115151, pana skin specialists ukipiga simu watakueleza muda na kama utataka kufanya appointment.
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Rutete si kupita Kibiti unakunja kulia kuliko na makao makuu ya wilaya ya Rufiji? Duh, mbali sana mkuu ruma! Ndo kwetu mkuu hahahahahaha
   
 18. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2009
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Prof Massawe karibu na kona ya majeneza muhimbili. Prof Palangyo ambaye ni mkuu wa chuo pia ni dermatologist mzuri. Tiba asilia unafagilia pia nikupe wataalamu wake?
   
 19. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Namimi naunga hoja >100% kama wah. waliotangulia kwa ku-recomend Prof. Massawe (Upanga karibu na MUHIMBILI), Dr Mboneko (Luther House), Dr Mgonda (MNH), Dr Bakari (MNH), hao wataalam pia utawakuta ukienda TUMAINI HOSP. pale Upanga karibu na makao makuu ya JWTZ.
   
 20. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wanaJF hivi wapi naweza kumpata daktari mzuri wa magonjwa ya ngozi?
  msaada wenu pls...
   
Loading...