Ujue Mti chonganishi

Ujue Mti chonganishi

mshana jr nakukubali sana ila thread yako hii ni ya kupuuzwa
ukiamini sana mambo kama haya ndo mwanzo wa kuwa mshirikina

Hii habari ya mti niliambiwa kama miaka mitano iliyopita ya kwamba kama umeupanda kwenye kiwanja cha nyumba mifakano ya kifamilia haitaisha. Kwangu niiipanda na majirani zangu wawili waliipanda pia, kusema ukweli mifarakano kwenye familia yangu ilikuwa haiishi na majirani zangu wawili familia zao zilifarakana kabisa na wanaume wakawa wamekimbia familia lakini baada ya kupata taarifa kwa watu kuwa miti hii siyo mizuri niliikata mara moja na majirani zangu pia waliikata. Tangu tuikate hakuna tena mifarakano na majirani zangu nao waume zao walisharudi kwenye familia zao na wanaishi kwa amani. Jaribuni na nyinyi kuchunguza hii kitu mtupe mrejesho.
 
Mi najua tu ina mizizi mirefu inayoleta nyufa kwenye nyumba hii nlishashuhudia.Kwenye mafarakano ndo naskia leo.
 
Sina jinsi
IMG_20171019_072007.jpg
IMG_20171019_071940.jpg
IMG_20171019_071948.jpg
IMG_20171019_071929.jpg
 
Yale maingiliano ya dunia ya kiroho na dunia isiyoonekana huthibitishwa na matokeo yake na si mchakato unaoonekana Kwa wale ndugu zangu wanaotaka ithibati za kisayansi naomba watulie wasome kimyakimya tuu.

Kuna huu mti unaopendwa kupandwa kuzunguka nyumba zetu, ni mti mzuri wenye kivuli kizuri, hujulikana kama mti mwamvuli na matawi yake huota kwa mpangilio maalum
Ni mti wenye mizizi mirefu yenye nguvu ya ajabu kiroho katika ulimwengu uonekanoa Mizizi yake yenye nguvu huweza kupenya kwenye msingi wa nyumba na kusababisha ufa au nyufa na kuleta uharibifu mkubwa kwenye jengo lako.

Nyufa husika zisipodhibitiwa mapema huweza hata kusababisha nyumba kubomoka au hata kuanguka.. Nyufa hizi zina madhara ya moja kwa moja kiroho nyufa hizi huleta nyufa kwenye familia, mikosi na hata vifo wakati mizizi ikileta nyufa kwenye nyumba jengo, nguvu yake huleta nyufa katika familia.

Nyufa ndani ya familia husababisha mshikamano uliopo kukatika vipande vipande, watu kukosa ajira, biashara kuanguka, watoto kufeli masomo na vifo hasa vya wazazi
Sio mzi mzuri wa kupanda nyumbani na wengi sasa wanaukata Kama unao nyumbani kwako hebu linganisha na hiki nilichoandika hapa.
14b6c812d3da7967172acd3db2c429bf.jpg
Dah nimeukata juz tu
 
Mhhh!!
Kuna rafiki yangu mmoja kutoka nchi jirani aliwahi kiniambia kitu kama hiki miaka takribani 18 iliyopita, kwamba mizizi yake ikiingia kwenye nyumba na mwenye nyumba anakufa!
Sielewi inakuwaje pale unapokuwa umepandwa na jirani mshana jr!?

Jamaa ni wa kutoka Uganda? Maana kuna wakati miti ya aina hii ilipandwa na kukawa na vifo vingi vya wamiliki wa nyumba husika. Mwisho wa siku waka conclude kuwa miti ina mkosi, lkn wakati huo miti hii migeni katika nchi ya Uganda ilipandwa na vijana wenye kipato ambao wengi waliathirika na ujio wa AIDS na wakati huo matibabu yalikuwa hafifu hivyo wengi waliishia kufa na hitimisho likawa kuwa ni sababu ya MTI wakati siyo kabisa.
 
Back
Top Bottom