Ujue Mti chonganishi

Aisee sasa kweli nimeanza kuamini. Kuna jamaa yangu Dodoma aliikata hii miti akidai haifai inaleta migogoro. Mimi nina mji Dar na niliotesha hii miti mitatu nyumbani na kuna jirani yangu alikuwa anayo na muda mwingi nipo nje ya Dar kwakuwa kazi nafanyia nje na Dar. Safari hii nimekuja likizo nakuta ile miti imekatwa kwangu na kwa jirani. Baada ya kuwauliza wanasema hii inaleta ugomvi sana nyumbani na jirani yangu anasema sasa ugomvi hakuna.
Ajabu sana.
 
Kuna watu wamekakamaa shingo wakipinga hii kitu
 
Kuna taasisi moja naifahamu, nyumba ya bosi imezungukwa na miti hii kila ajaye hupoteza ubosi kwa kugombana na wafanyakazi wenzie. Wamebadilisha sana mabosi. Naamini hiki kitu.
Na kwasababu ya usomi wao wa darasani wanaweza kukubishia kabisa kuwa hakuna kitu kama hicho
 
Mti wowote unaopandwa karibu na nyumba wakati wa upandaji inabidi shimo lichimbwe refu.

Ili mmea uanzie chini na mizizi yake itasambaa kuelekea chini na kusambaa bila kuja juu wengi wanakosea saana upandaji wa miti karibu na nyumba.
Unaupanda ukiwa mkubwa ama ukiwa mche? Kumbuka pia kuna miti ya kupanda karibu na nyumba, hii mizizi yake huelekea chini na kuna miti hujulikana kama tambazi yani mizizi yake haiendi chini bali hutambaa
 
Wajinga ndio huamini mambo ya uchawi/ushirikina......hata wakiwashwa makalio watajua ni uchawi uliotokana na uwepo wa mipapai
Yaani waTanzania,bado tuna safari ndeefu sana ...mti upandwe na mtoto asife yeye aje afe baba?
By the way kuna family nyingi tu hawana miti kama hiyo lakini matatizo na vifo havikauki nyumbani!
Tumieni akili kutatua changamoto zenu sio pesa imekosekana nyumbani muanze kutafuta nani mchawi!
Wewe huna tofauti na wale wapumbavu wanaoamini usipojengea makaburi ya wazazi wako hutafanikiwa katika maisha!
 
Unaupanda ukiwa mkubwa ama ukiwa mche? Kumbuka pia kuna miti ya kupanda karibu na nyumba, hii mizizi yake huelekea chini na kuna miti hujulikana kama tambazi yani mizizi yake haiendi chini bali hutambaa
Unapanda, ukiwa mche, chimba shimo refu, mche uwe ndani ya shimo mizizi itachukua himaya yake kama kawaida, itasambaa chini, itajitutumua lkn itakuwa level bila madhara.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…