greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 786
- 1,219
MAKALA YA 3
Karibu katika Makala yenye kuelimisha mambo muhimu kuhusiana na ujenzi wa Majengo.Leo,tutaangazia juu ya DAMPNESS/Unyevu katika jengo.
Hili ni jambo linalokumba Majengo nchi nzima.
1.Dampness/ Unyevu jengoni: Hii ni hali ambayo sehemu za jengo huonekana na hali ya kulowana au ubichi.
Ambapo utaona:imelowa, ukijani ukijani,ukungu mweusi na hata chumvichumvi.
2.Aina za Dampness ni kuu tatu.
A.UNYEVU UNAOPANDA:huu ni unyevu wa maji unaopanda kutoka kwenye udongo kwenda kwenye jengo kupitia msingi wa jengo au slab ya sakafu.
-vitundu vidogo vidogo kwenye matofali ya kuchoma,block na zege huwezesha maji kupanda juu kutoka ardhini.
-Aina hii hutokea kwenye nyumba zilizo jengwa kwenye maeneo yenye Ardhi yenye kushikilia maji kwa mda mrefu. Mikocheni, Msasani(Bonde la mpunga)Mwanyamala,Mbezi Beach,
-maeneo ambayo ukichimba mita hata 2 unapata kisima cha maji.
3.Falling Dampness/Unyevu unaoanguka:Hii hutokana na kuchururizika kwa maji kutoka juu kutokana na ubovu wa mfumo wa paa,ambapo maji.
-Chanzo kikubwa ni Kuu kuvuja kwa bati,kuziba kwa gutter, ubovu wa mfumo wa gutter,angle ndogo ya kukimbilia maji ya mvua
-Hii hutokea sana kwenye majengo ya mtindo wa "Contemporary",mana mengi ya Majengo yana mfumo mbovu wa paa.
-Kwenye vibaraza vya Zege.
-Majengo yenye paa za zege.
4.PENETRATIVE DAMP/UNYEVU PENYEZI : Hii hutokea kwenye usawa wa ukuta.
-husababishwa na kuta kunyeshewa mvua na kuvuja kwa mabomba ya maji safi na maji taka
Ubovu wa uwekaji tiles vyooni au jikoni.
-miti kuwa karibu na nyumba
-ukuta wa fensi kuwa karibu na nyumba
-usanifu mbovu wa sehemu/Chumba cha jiko.
-Mafuriko
5.Athari za DAMP/UNYEVU
Amini au usiamini, chanzo kikubwa cha kuharibika kwa Majengo ni uwepo wa UNYEVU.
mojawapo ya athari zake ni.
-Kutu kwenye nondo.
-Kuharibika kwa zege...unyevu ndani ya zege huipa nondo kutu na kusababisha nondo kuvimba na mwishowe nyufa.
-chumvi kwenye matofali na plasta .
-Kuharibika kwa finishings za kwenye sakafu
Mf.tiles ubanduka,
6.Athari nyingine
Kulegea na kubanduka kwa plasta
-Kuvimba kwa mbao
-kumeng'enyuka kwa mbao
-huleta mazalia ya mchwa,na mbu
-kubanduka kwa rangi
- Kupunguka kwa rangi, utaona madoa meupe meupe au michizi meupe katika rangi, hasa kwenye kuta zilizo pakwa rangi ya kijivu.
-hitilafu ya umeme kwenye jengo.