Uchafu wa kiroho hunuka kuliko uvundo wa maliwato

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,889
Mapenzi ni ya wawili tuuu.. Haiwezekani mtu mmoja awapende watu wawili ilihali ana moyo mmoja ni wazi kuna mmoja atadanganywa hapo! Moyo hupokea hisia za mtu mmoja tu kwa wakati mmoja.. Umiliki wa hisia za mapenzi ndani ya moyo huwa na nafasi moja tu, nyingine zote ni wavamizi na wezi wasiotakikana!

Kuna kitu kinaitwa usafi wa kiroho.. Usafi wa kiroho una harufu yake nzuri sana pengine hata kuzidi marhamu ya bei ghali na mauaridi yanukiayo sana nyakati za adhuhuri tulivu..
Usafi wa kiroho huvutia, hutamanisha na huleta ladha ya kipekee mno! Usafi wa kiroho ni kichokoo muhimu cha usafi wa kimwili

Kuna kitu kinaitwa usaliti kwenye mahusiano.. Wasaliti nyuso zao zimejaa ukungu.. Hata awe msafi vipi kimwili, uso wake hauna nuru na macho yake hayana utulivu.. Ni mtu wa kuhamanika muda wote,mwenye tabasamu la kulazimisha.. Msaliti nyuma ya macho yake amebeba maumivu yaliyofichika

Mahusiano kama nilivyosema ni ya wawili tuu na kwakuwa yanahusika na kuingiliana kimwili basi yafaa via vya uzazi vya kila mmoja visiwe mali ya jumuiya ama visiwe chini ya umiliki wa zaidi ya mtu mmoja.. Na ndio maana vinaitwa sehemu za siri

Usaliti kwenye mahusiano ni kitendo cha kuruhusu muingiliano na mtu asiye wako, kumruhusu kukuona utupu wako na kukuingilia kingono.. Moyo wa mtu ni kiza kinene sana.. Lakini kwakuwa usaliti kwenye mahusiano ni kama wizi huwa kuna arobaini yake

Sasa uchafu wa kiroho hutokeaje? Uvundo wa harufu yake hujaje? Ni pale unapofumaniwa na mwenzi wako
Aliyekupenda sana
Aliyekuamini sana
Aliyekuheshimu sana

Baada ya fumanizi kila kitu hubadilika.. Ni kama bilauri ikipasuka hata uungeje nyufa zitaonekana..
Kule kunukia kote ulikokuwa nako kunageuka uvundo mkali kama ule wa choo cha jiji
Utaanza kuonekana mchafu kichwani hadi miguuni
Utaonekana unanuka nywele zako
Utaonekana unanuka kikwapa
Utaonekana unanuka mdomo
Utaonekana unanuka sehemu za siri
Utaonekana unanuka miguu

Na harufu aliyokukuta nayo siku ya fumanizi ni harufu ambayo haitakaa imtoke na itamnukia vibaya kuliko chochote! Harufu hiyo ataioanisha nawe na kusababisha haya

Akukuangalia sura yako nzuri atakuona kama kinyago
Akiangalia macho yako ataona kama ya zimwi
Ulimi wako ataona kama wa nyoka mwenye sumu kali
Mwili wako atauona kama tutusa!

Hakuna jema lolote utakalomfanyia afurahi
Mbusu, mkumbatie, mpe atavuta hisia na kukumbuka kuna mwingine unamfanyia yote hayo..
Akikumbuka hayo ile harufu kali humjia na mwili wake kukosa msisimko na kubaki wa baridi kama maiti ndani ya jokofu

Kuna wanandoa haya ndio maisha yao! Hawawezi kuachana kwasababu mbalimbali lakini hawana hisia za upendo tena kati yao.. Na maranyingi chanzo ni usaliti katika mahusiano
faadb711d0c2d3944b393f5a6dfad874.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom