Ijue nguvu ya mti huu "Kisamvu"

khamis kilo

JF-Expert Member
May 23, 2016
1,051
1,200
Duniani kuna miti mingi sana yenye nguvu za asili za miujiza

Katika miti hiyo mmoja wapo ni mti wa kisamvu

Kisamvu ni mboga, mizizi yake ni chakula na hata shina lake huweza kutumika kama kuni

Lakini siri kubwa iliyopo katika mti huu ni kuwa,majani yake yana uwezo mkubwa wa kukufanya uwaone wachawi live wakiwa kwenye kazi zao.

Kama na wewe ni mtu anayetamani sana kuwaona viumbe hawa basi fuata taratibu zifuatazo

Sharti
1.usiwe muoga
2.utakapowaona usikimbie wala kuonyesha mshtuko bali tulia mpaka watakapotoweka

Tahadhari
~ni vyema uwe na kinga dhidi ya nguvu zao hasi,hili pindi utakapovunja sharti lolote hapo juu usiweze kupata madhara yoyote

MAANDALIZI
~Ponda kisamvu mpaka kiive vizuri

~Kamua hili upate maji yake

~Chukua maji hayo nawa usoni huku unanuia

Ukimaliza hapo nenda sehemu ya soko ama panapokuwa na mkusanyiko mkubwa wa watu ama kasimame njia panda,pia hata ukiwa ndan umelala kama watakuja utawaona

Zingatia masharti
Kisamvu.jpg
 
Ukitaka kuwaona wachawi ni simple tu, weka mapumbu ya nguruwe mfukoni, popote utakapokuwa kama wapo utawaona.
 
Hizi elimu za spiritualism ni ngumu sana kueleweka kwa watanzaia walio wengi. Maana dini na tamaduni zao zimewaficha maarifa haya. Wajanja wanaofahamu wameendelea kuishika nchi na kutawala uchumi.

Wazungu wanafahamu vizuri sana kuwa huu ulimwengu wa nyama (physical world) si halisi, upo ulimwengu mwingine usioonekana unaotawala huu uliwengu wa nyama.

Ukitaka kulijua hili angalieni mazishi ya malikia wa Uingereza yalivyofanyika. Ingekuwa ni huku kwetu watu wangesema ni ushirikina.
 
Back
Top Bottom