Ujue mkoa wa Mbeya kwa ufupi

Ujue mkoa wa Mbeya kwa ufupi

Mwiboma hapo,Soko matola ..maeneo ya wahindi sisimba Hapo mpaka Azimio Bado kupo?Ama kulisha Badilishwa Matumizi.
 
Naipenda Mbeya kuliko mkoa wowote ule TZ ila Mby ni kijiji kikubwa. Mbeya inabadilika kwa speed ndogo sana kulingaisha na jina lake.

Mbeya mjini imechakaa zaidi kuliko miaka ya 2000, soko la mjini baada ya kuungua hawajajenga tena.

Isyesye makazi mapya ila nyumba zinajengwa hovyo hovyo.

Iwambi wamejitahidi, naona ni kwa watu wa kipato cha juu kiasi ila lami bado hazijafika. Vumbi kama lote.

Forest mpya kuzuri hadi kule kwa Mwamunyange kuzuri. Uzunguni bado ni uzunguni tu.

Mabatini, Sokomatola hakujawahi kuendelea.

Bujibuji unajua kwanini Rift valley pale Sokoine ilikufa? Ipo eneo zuri ila imekua ghofu sasa.

Mbeya huduma ndogo tu unaweza kuzunguka mji mzima ukaikosa.

Watu wanaopenda nightlife, Mby hakuna club ya maana, hiyo citypub pale Kabwe, kwetu pazuri kule Sae ni utopolo tu. New Maisha club baadaye The Vibe pale Mzumbe ilikufa nasikia wanataka kuifufua tena. Zamani kulikua na Pamodzi pale mjini karibu na TRA sijui kama bado ina-operate.

Speaking of Mzumbe, nitakua sijamtendendea haki Anania mpika kyepe kitamu bongo nzima. Kibanda kimechoka ila mchana hadi Sugu anakula pale na watumishi wa BOT. Kadhalika kuna watoto wabichi wa mzumbe unaweza waokota pale. Chimbo langu lile.

Nilipata kwenda Matema beach last December, mwenye nayo kajitahidi kufanya uwekezaji panapendeza. Landmark hotel ya pale ipo vizuri, and ni lami hadi Matema toka Mby.

Chunya naona kumefufuka tena, mji umekua, watu wameongezeka na nyumba nzuri zipo. Chunya kuna magari mazuri mengi kuliko Mbeya mjini.

Hapo sijaongelea wana-mbeya wenyewe.

Naweza kuandika all day kuhusu Mby.
 
Mkoa wa Mbeya ni moja kati ya mikoa sita (6) iliyopo katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mikoa mingine ni Rukwa, Iringa, Njombe, Songwe na Ruvuma. Mkoa wa Mbeya ulianzishwa mwaka 1961 na ulikuwa ukijulikana kwa jina la ‘Southern Highland Province’ kwa kujumuisha baadhi ya maeneo ya mikoa ya Iringa na Rukwa. Mkoa una eneo la km. za mraba 63,617 Kati ya hizo km. za mraba 61,783 ni za nchi kavu na km. za mraba 1,834 ni eneo la maji. Kulingana na Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 1967 mkoa ulikuwa na watu 969,053, Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 Mkoa wa Mbeya ulikuwa na jumla ya watu 2,063,328.

Kufikia mwaka 2010 mkoa ulikadiriwa kuwa na watu 2,662,156. Mkoa wa Mbeya upo kusini magharibi mwa eneo la Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania. Mkoa upo katika Latitudi kati ya 7º na 9º 31’ kusini ya Ikweta na Longitudo kati ya 32º na 35º mashariki ya Greenwich. Mkoa unapakana na nchi ya Malawi upande wa kusini, Mkoa wa Songwe upande wa magharibi, Mikoa ya Tabora na Singida kwa upande wa kaskazini ambapo kwa upande wa mashariki unapakana na Mkoa wa Njombe. Mji wa Kasumulu katika Wilaya ya Kyela, hufanya mlango wa kuingilia na kutokea nchini Malawi.

Katika enzi za ukoloni wa Waingereza, Mkoa wa Mbeya ulikuwa ukijulikana kwa jina la ‘Southern Highland Province’. Mkoa ulikuwa ukiunganisha baadhi ya maeneo ya mikoa mitatu ya sasa ambayo ni Iringa na Rukwa. Jina la Mbeya limetokana na neno la kisafwa."Ibheya" ambalo maana yake ni chumvi, kutokana na wafanyabiashara kufika.na kubadilishana mazao yao kwa chumvi.

Mji wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo mwaka 1927. Wakati huo dhahabu ilianza kupatikana katika milima iliyopo karibu na Mbeya hadi Chunya hivyo Mbeya ulikuwa ni mji wa mapumziko kwa Wazungu kutokana na hali yake nzuri ya hewa, hali iliyosababisha mji wa Mbeya kupewa jina la utani kama "The Scotland of Africa" baada ya kutambua kama uoto, hali yake ya hewa na muonekano wa milima (hills) inayouzunguka mji wa Mbeya kufanana na Scotland mfano uoto unaopatikana katika mlima Loleza. Mkoa huu ni moja kati ya mikoa mikongwe
iliyokuwepo mpaka wa kati wa uhuru mwaka 1961. Katika kipindi hicho, makabila makuu katika Mkoa wa Mbeya yalikuwa ni Wasafwa, Wanyakyusa, Wandali, Wasangu, Wamalila, Wanyiha, wakimbu na Wanyamwanga. Ambapo jamii hizo ni maarufu kwa kujishughulisha na kilimo na ufugaji mdogomdogo.

Scotland of africa
 
Back
Top Bottom