Ujio wa sheykh Sudeys Tanzania

Tunamwombea Sheikh. Abdulrahaman Al-Sudeis aweze kusafiri salama kutoka Makkah hadi Dar es salaam ili tuweze kujumuika naye katika mashindano hayo. Amiin
KARIBU TANZANIA SHEIKH. AL -SUDEIS; TUNAKUSUBIRI KWA SHAUKU SANA!
Ameshawasili salama mkuu, na kuna mtoto kamsomea qur an unaambiwa hadi sheikh sudeys alienda kumbusu na kumwambia iko siku nitasali nyuma yako kwenye msikiti wa makkha,
IMG-20170609-WA0000.jpg
IMG-20170609-WA0000.jpg
 
Alhikma wanachekesha sana wanamkalibisha mtu wasie mjua kama mwislaama au familia yake wote wakristo na yeye pia alafu et ndie mgeni rasimi na kumkutanisha na sheikhs mkubwa duniani inaniuma sana
Umeaminishwa kwamba Kassim Majaliwa sio Muislamu?
 
Na ukisikia jambo usiwe mbishi fanya uchunguzi ili ubaini ukweli wake
 
Sasa Masheikh huyu PM Mnanwalika kama Mgeni Rasmi atatoa nasaha gani za Dini? Kigezo gani mlichokitumia mpaka mkaona yeye ndo anaye fit Ugeni rasmi
Point, manake kwenye tukio lazima kuwe na mfikishaji Ujumbe kwa walengwa, sijui wametumia kigezo gani kumualika mtu ambaye hatoleta impact yoyote
 
Taasisi ya Alhikma Foundation chini ya usimamizi wa sheykh Nurdin Kishki inawaletea mashindano makubwa zaidi ya kuhifadhi Qur-an Afrika, mgeni rasmi akiwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa na mgeni maalum katika mashindano ya 18 mwaka huu ni Imamu Mkuu wa Makkah na Madina, Sheykh Abdulrahman Sudeys siku ya tarehe 11 June 2017,Uwanja mkubwa wa Taifa.HAKUNA KIINGILIO. NYOTE MNAKARIBISHWA
fd45d5620322ab793bf900bef65b5788.jpg
Mungu anijaalie SIHA/AFYA njema...kuifikia siku hiyo...Baarakallaah.

Hakika ni UGENI mzito...
 
Muombee na Amani kwa mungu wenu,Kibiti kusini mwa nchi,na nchi yote kwa ujumla msiishie kukariri tu na kutumia uwanja wataifa( wa watanzania) mka kung'uta miguu mkaenda.
Wakati ndg zetu wanauwawa na magaidi kibiti na vitongoji vyake.
Kama kuna mgeni maalumu basi na dua maalumu iwepo kuiombea kibiti,magaidi washindwe na wakakamae(maana wakinyong'onyea huenda wakapata nguvu;))
Kibiti kama kuna magaidi wa kiislamu wakemewe hali kadhalika wa kikristo ,waache kudhurumu nafsi za maskini wenzetu/wenzao
Hata wewe pia unayo kwann usiombe matatizo yakaisha mpaka uwatake watu waimani nyingine au umwaamini Mungu wako???
Siku utakayotolewa Roho ndo utajua kipi kilikuwa pumba na mchele ulikuwa wapi subiri tu!
 
Back
Top Bottom