Mc,Hee,vipi umeambiwa uwakampenie huku?
Wakuu,
Yaelekea kuwa Wembe wa CCM ni uleule wa 2005, utanyoa Vichwa vya zamani na kipya cha CCJ. gonga Gogo usikie mlio: ngomaafrica - 04 April 2010 - The Ngoma Africa Band Presents song:Jakaya Kikwete 2010(Rumba)
Kwa hisani ya "NGOMA AFRICA BAND"...
CCJ wanajua hawana nguvu katika uchaguzi wa mwaka huu hata wakiruhusiwa kugombea ubunge na uraisi.
Ikiwa kuna vigogo katika CCM ambao wanataka kujiunga na chama hicho, kukipa nguvu na jina kubwa, wanangojea nini? Miezi mingapi imebaki kabla ya uchaguzi? Watajiunga baada ya uchaguzi? Wakishinda katika uchaguzi wa mwaka huu, watakuwa wamechaguliwa kama wana CCM. Baada ya kuchaguliwa, nani anategemea wataondoka CCM, chama kilichowaweka na kuwatunza madarakani, mara tu baada ya kuchaguliwa au hata baada ya muda, na kwenda kujiunga na CCJ?
Msingojee CCM kupasuka.
Pia kuna dalili gani zinazo onyesha kwamba CCJ ni tofauti na vyama vingine vya upinzani vilivyoanzishwa kupambana na CCM? Kuna wananchi waliovutiwa sana na party manifesto ya CCJ. But the manifesto itself is not enough. Haitoshi!
Ikiwa vyama vya upinzani haviungani kuwa chama kimoja kikubwa na chenye nguvu bara na visiwani, au ikiwa havishirikiani katika uchaguzi kama opposition alliance, visahau kabisa kwamba wataking'oa Chama Cha Mapinduzi kutoka madarakani. Kuna wapinzani wanaoweza kuongoza nchi yetu vizuri kuliko CCM, kwa mfano, Dr. Slaa na wengineo, lakini hawana solid base at the grassroots level, katika kila wilaya, na katika kila mkoa, kama CCM kuweza kushinda katika uchaguzi mkuu na kuingia Ikulu.
Pia, CCJ, jiangalieni na mikoba yenu! The Kariakoo incident was just a warning. Ni onyo kubwa. You are dealing with a ruthless enemy.
As an opposition party, you need all the help you can get kutoka kwa wananchi na vyama vingine vya upinzani kuweza kupambana na CCM. Mkiungana, kama vyama vya upinzani, labda mtafanikiwa 2015 au 2020.
Mwaka huu, mtakuwa mnawasindikiza tu wana CCM mtakapokwenda kupiga kura. Ushindi ni wao mwaka huu. Ni jambo la kusikitisha lakini huo ndiyo ukweli. Jitayarishe kuongozwa, au niseme kupotezwa kama taifa, na CCM kwa muda wa miaka mitano ijayo.
Walaumu viongozi wa upinzani na waulize kwa nini wameshindwa kuungana au kwa nini hawataki kushirikiana ili wawe na nguvu ya kutosha kuweza kupambana na CCM kila mahali bara na visiwani.
Mapambano hayo siyo katika uchaguzi tu, wa halali, bali pia katika wizi wa kura. Nani hajui CCM wanaiba kura mara nyingi au labda katika kila uchaguzi? Kwa mfano, hawajawahi kushinda katika uchaguzi wowote visiwani. Kungekuwa na uchaguzi wa haki na halali visiwani, CUF wangekuwa madarakani.
Lakini mkiungana, kama wapinzani, you can dislodge CCM from power, ingawa siyo katika uchaguzi huu.